'House girl' amnyonga mtoto, ajinyonga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'House girl' amnyonga mtoto, ajinyonga

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by JS, Jul 30, 2010.

 1. JS

  JS JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Habarini za leo!! Leo katika uchambuzi wa magazeti nimesikia kuwa huko Morogoro msaidizi wa kazi za nyumbani (famously known as housegirls) kamnyonga mtoto wa miaka wa miaka 2 na yeye kaishia kujinyonga pia. Sababu haijajulikana na uchunguzi unaendelea.

  Hii si mara ya kwanza kwa hawa wadada kufanya vitendo vya aina hii. Kuna mwingine hapo nyuma alikuwa na virusi vya ukimwi. mama wa mtoto akitoka asubuhi kwenda kazini yule dada huku nyuma anamnyonyesha mtoto mwishowe mtoto akaathirika.

  Zamani pia miaka ya 90 nilisikia kuwa kulikuwa na mtindo wa watoto wadogo kuwekwa kwenye fridge/freezer wengine kwenye ovens ikiwa ni njia ya kulipiza kisasi kwa waajiri wao kutokana na sababu mbalimbali.

  Hii kwa kweli inatisha na inasikitisha. wakati mwingine unakuta dada anaishi vizuri na waajiri wake lakini baadae mambo yanaharibika kwa upande wa dada na wanaokuwa victims ni watoto ambao wanashinda nao nyumbani.

  Nini kifanyike kuzuia mambo kama haya yasiendelee?? ina maana mioyo ya hao wadada wanaofanya hivyo ni mikatili kiasi hicho au???
  Sijawahi kusikia cases za wakaka (houseboys) na ningependa kufahamishwa kama ziko.
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi nawaombeni akina mama ishini vizuri na hawa wafanyakazi wa ndani maana wanabeba dhamana kubwa ya nyumba zenu wengi wenu mnawanyanyasa kana kwamba hana kwao au hana wazazi waleeni kama mnavyo walea watoto wenu vilevile mjitahidi kuwathamini haya yote mabaya wanayo fanya ni kutokana na ukatili wa akina mama wenye nyumba.
  Poleni sana wafiwa wa Moro.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,266
  Likes Received: 22,024
  Trophy Points: 280
  MTUMISHI nyumbani kwa mkazi wa Uwanja wa Ndege, Kihonda mkoani Morogoro amemnyonga mtoto wa 'tajiri yake' mwenye umri wa miaka miwili na nusu.

  Binti huyo mwenye umri wa miaka 16 alimnyonga mtoto huyo, Seth Steven, jana saa 2.45 usiku na yeye akajinyonga.

  Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro,Thobias Andengenye, amesema, mtoto huyo amenyongwa nyumbani kwa, Steven Kapombe, alipokuwa akifanya kazi binti huyo.

  Kwa mujibu wa Kamanda huyo, msichana aliyemyonga mtoto huyo anaitwa Zaina, na kwamba alikuwa anafanya kazi nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo.

  Kwa mujibu wa Andengenye, alitumia kipande cha kanga kumyonga mtoto huyo na alitumia nguo ya aina hiyo kujinyonga.

  Alisema, chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana na kwamba, polisi wanaendelea kuchunguza.

  Wakati huo huo, mkazi wa uwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, Farida Athumani (34), anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kutaka kujiua.

  Msichana huyo alikunywa sumu ya panya jana saa 5 asubuhi, na kwamba, mkazi wa eneo hilo, Ahmed Omary (63), alitoa taarifa Polisi.

  Andengenye alisema, polisi wanaendelea kuchunguza tukio hilo na kwamba, msichana huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hawa mahouse girl jamani sina sijui tufanye nini katika hali hii?
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Jul 30, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Mimi bora niajiri mtu wa kuniangalizia mtoto kuliko kuajiri mtu wa kunisaidia kazi za nyumbani. Hakuna kazi ya nyumbani ambayo siiwezi na kama sina muda wa kutosha basi nitatengeneza muda.

  Unapomtumikisha mtu (kufua nguo, kupiga pasi, kusafisha nyumba, kupika, kumwangalia mtoto na kadhalika) itafika mahali huyo mtu ataanza kuona ananyanyaswa kitu ambacho kinaweza kumfanya afanye yasiyopaswa kufanywa.

  Niangalizie mtoto wangu nikirudi kutoka kazini unaanza....
   
 6. JS

  JS JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  True Fidel manyanyaso yanakuwa mengi sana yani mpaka unaona huruma. Hivi kwa nini usimtendee tu wema mwenzio anayekuangalizia mtoto/nyumba yako/kazi zako?? Nina uhakika kuna kina mama ambao wamo humu JF wanasoma hii na wananyanyasa wasaidizi wao
   
 7. kaitlynne

  kaitlynne Member

  #7
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa mahousegirl ni kama wamevamiwa na roho gani sijui kila mzazi analalamika.Jamani haya makampuni tunayofanyia kazi waangalie jinsi gani ya kutusaidia wafanyakazi wake. Kama ni kuanzisha day care centre eneo la kazi ili tuwe na amani. Hali inatisha. Kweli ni janga la taifa.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,266
  Likes Received: 22,024
  Trophy Points: 280
  Ishini nao vizuri.
  Anapika yeye halafu unamwambia asile chakula hicho, apike chakula kingine kwa ajili yake.
  Mnawatesa, kuwanyanyasa na kuwasimanga.
  Hamuuthamini mchango wao hata kidogo
   
 9. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Houseboys? Kuna mmoja UDSM alikua kila siku wakiondoka tu wazazi anampa mtoto "koni" basi mtoto wa watu kifua hakimuishi...

  Nimekuja kugundua mambo matatu yanasababisha malezi ya watoto yawe magumu.

  Kwanza, wazazi "wanajidai" wapo busy sana kukaa watoto waliowazaa wenyewe.

  Pili, baadhi ya kinamama kuwa wakatili sana kwa wasichana wa kazi. Unamchapa makofi wa nini? Kisa kavunja glasi? Kina baba pia huchangia katika hili, maana "hawaaminiki" kwa hawa watoto kwa hiyo mama anatoa ukali kama kutoa tahadhari - ole wako wewe!

  Tatu, kuna wasichana vichwa maji tu au wakatili. Au may be wamekuzwa vibaya, alikotoka au alipokua wao mtoto anapigwa kama ngoma kwahiyo anashangaa wako huwapigi ipasavyo!!!

  Kwa hiyo yeye anaanza kudunda. Kazi zinawazidia (kupika, kufua, watoto) kiasi kwamba anakuwa hana patience tena na mtoto aliaye, anapiga, ukija kuambiwa unapiga na wewe. Hapa sahau mambo ya mtoto kukua vizuri psychologocally kwa kupata mapenzi - zero. Mama na baba wanasaka shilingi.

  Someni post ya Ngabu hapo juu, wazazi mkiamua mnaweza, acheni kutafuta sababu za kutokukaa na watoto wenu.
   
 10. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160


  Kudos Nyani, Kudos!!!
   
 11. kaitlynne

  kaitlynne Member

  #11
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri mtoa mada ameangalia upande mmoja tu, kuna upande mwingine ambapo unakuta hgirl anapendwa na kutunzwa kama ndugu kabisa lakini bado haishi vituko.Binafsi siwezi nyanyasa mtu ambaye anakaa na mtoto wangu , anampikia , anamlisha n.k wakati sipo,na naamini kuna kina mama wengi tu ambao wako hivi.

  Kama anataka kumnyonga mtoto atanyonga tu hata kama halali hapohapo. Atakuja asubuhi atamyonga ataondoka zake. mtu mwenye uwezo wa kunyonga au kuua tayari iko ndani yake hata umfanyie nini siku akijisikia kunyonga atanyonga.
   
 12. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nikisema mtasema mtasema yaleyale ya mfumo dume...bora ni:shut-mouth:
   
 13. T

  Taso JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi wanakuwa abused, oppressed, repressed, and suppresed. Underpaid, overworked, caged, molested, uneducated, impregnated, talked-down, raped, muzzled... akichoka ananyonga katoto kako anaanza.
   
 14. JS

  JS JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkeshahoi sema tu watu angalau tupate ufumbuzi wa kuzuia mambo haya yasiendelee usikae kimya
   
 15. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani hizi kesi za housegirls mpaka lini?
  Tujifunze kuishi na watu hawa kama wafanyakazi wenzetu wengi wao wananyanyaswa kupita kiasi na mwishowe huishia kujikuta wako frastrated sana depressed sana na kutenda mambo ya ajabu. tuishi nao kama ndugu zetu na si watumwa
   
 16. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kaitlynne, huyu kamnyonga mtoto naye kajinyonga je inawezekana akaamua tu kunyonga bila sababu? katika cases nyingi nilizoona mm mahousegirls walikua wanaishi maisha ya utumwa sana, wanatumikishwa na adhabi juu. kuna nyumba jirani nami, housegirl huamka sa10 asbh utamsikia anafagia huko nje na usiku sa6 pia utamsikia anasugua masufuria binti huyu hazidi 17 yrs na wakati wote analalamika mama hataki kunipa mshahara! je huyu atatenda yapi siku yakimzidi?
   
 17. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Hizo ndio mbaya zaidi afadhali hata wadada...

  Kuna jamaa alimuharibu mtoto wa mwenzie hivi hivi, wazazi wakiondoka anamvua suruali... wazazi wamekuja gundua too late... almost three years kijana anakula tigo ya mtoto....

  These stories are sad, lakini waajiri wanachangia haya matatizo kwa asilimia 90.

  Mama unatoka asubuhi, unarudi saa 4 usiku, hujui mtoto kashindaje, kala nini, mara unataka msichana wa kazi akufanyie kazi zote hadi kufua kufuli zako... akupikie, akupakulie (wewe na mumeo)...

  Kwanza shughuli ya kuangalia mtoto pekee ni kazi ngumu kuliko zote...
   
 18. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Uchunguzi wakaufanye kwa mama mwenye nyumba lazima alikwa anamtesa sana huyo binti au amemnyima mshahara wake. au baba mwenyenyumba kambaka huyo binti. na yeye ndo kumaliza hasira zake kamalizia kwa mtoto. Kuna kipindi walilipoti juu ya mama wa kihindi alikuwa hawalipi house girl wake, mmoja alimtolea uvivu kwa kumbanika mtoto. mama aliporudi akakuta maiti imekauka na housegirl hayupo!

  Lakini mara nyingi mie huwa najiuliza hizi inakuudhi nini kula na house girl? kumfanyia shopping na mengine? hata kumsomesha kama atapenda? kwa sababu anaweza kuua familia nzima kama akiamua. Wanabeba sana uhai wetu ila hatujui tu>
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Yaani wasichana wa ndani wananyanyasika sana nimeshuhudia.
  Wengine wanaambiwa wasile chakula pamoja na watoto wa boss wengine wanalishwa makombo chakula walicho bakiza maboss wengine wanakula msosi tofauti na maboss wao yaani anaanda misosi miwili tofauti yaani manyanyaso wengine hata TV marufuku kugusa yaani utafikiri sio binadamu. Fikiria ww ndo uwe unafanyiwa hivyo utajisikiaje?
   
 20. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  As a parent I'm touched by the sad demise of Baby Seth! Nimemkumbuka jr ghafla na namwomba Mungu atulindie wanetu popote walipo!

  NN utamaduni huo unaousema hapa nyumbani bado haujazoeleka na kwa kiasi kubwa ni hatari zaidi kiusalama na hat kiafya kwa mtoto mwenyewe cha muhimu ni kuona kunakuwepo day cares za kutosha ili zipunguze hili tatitzo!

  Poleni wazazi wa Seth!
   
Loading...