Hotuba ya upinzani - wizara ya mawasiliano, sayansi na teknolojia

The Conquerer

Member
Aug 16, 2012
79
94
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENIMHESHIMIWA SUSAN JEROME LYIMO (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YAFEDHA KATIKA WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA MWAKA WA FEDHA2013/2014
MheshimiwaSpika, napenda kuchukua nafasi hii kwa mujibu wa Kanuni ya 99, kanunindogo ya 9 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la 2013, kutoa maoni ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni, kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha,katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, kwa mwaka wa fedha 2013/2014.Mheshimiwa Spika,Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inawajibu wa kusimamia utafiti,utungaji na utekelezaji wa Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEKNOHAMA). Wizara hii pia, ina jukumu la kusimamia mawasiliano ya posta, naya njia ya simu. Vilevile inajukumu la kupata na kutumia teknolojia, kuendelezawataalamu wa ndani katika fani za sayansi na teknolojia; kufanya utafiti wamawasiliano, sayansi na teknolojia, kusaidia uvumbuzi, na kuongeza ufanisi. Muheshimiwa Spika,Diraya wizara hii ni kuwa na jamii ya watanzania wenye maarifa na uwezo wakisayansi, kiteknolojia na wa ki-uvumbuzi,kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi nahivyo kuweza kukabiliana na ushindani wa kimatifa.Mheshimiwa Spika, licha ya tamkozuri la dira ya wizara hii, Kambi Rasmi ya Upinzani inasikitika kwamba,Serikali hii haitekelezi kwa vitendo tamko hili jambo ambalo limeifanya nchiyetu kuendelea kuwa nyuma katika medani za sayansi na technolojia na hivyokuendelea kuwa soko la "mawazo yakisayansi" na bidhaa zinazotokana na uvumbuzi wa kisayansi na technolojia.Nia aibu kwa taifa kwamba wakati elimu ya mataifa yaliyoendele inalengakuwawezesha watu wao kuvumbua vitu mbali mbali vya kumpunguzia binadamu ugumuwa maisha kupitia sayansi na teknolojia, sisi elimu yetu inalenga kumfundishamtanzania namna ya kutumia vifaa vinavyotokana uvumbuzi kisayansi na teknolojiaya nchi zilizoendelea. Jambo hili linamfanya mtanzania aendelee kuwa tegemezi kifikrakwa kuwa elimu yake ni katika kutumia tu na si katika kugundua vitu vipya.Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwauchungu mkubwa kwa kuwa sioni jitihada za makusudi zikichuliwa ili kubadilitaifa letu kutoka hali duni tuliyo nayo sasa, na kulipeleka katika hali nzurizaidi kwa njia ya sayansi na teknolojia. Sina hakika pia kama teknolojia yamawasiliano tuliyo nayo sasa, na iliyoenea sehemu kubwa ya nchi, inatumikakatika kuleta mapinduzi ya kiuchumi ili kulinusuru taifa na umasikiniuliokithiri. Hii ni kwa sababu, katika hotuba ya Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzaniya mwaka wa fedha 2012/2013, Kambi Rasmi ya Upinzani ilibaini mapungufu katikaWizara hii muhimu na kuitaka Serikali kuchukua hatua ili mawasiliano, sayansina teknolojia viweze kutumika katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo hapanchini lakini mwitikio wa Serikaliumeendelea kuwa ni ule wa kusua . Miongoni mwa masuala muhimu ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani illitaka Serikalikufanya kwa mwaka wa fedha unaomalizika ni pamoja na yafuatayo: 1. Kuibua vipaji vya ubunifu na uvumbuzi wa ki-teknolojia miongoni mwa wanafunzi nawananchi wenye vipaji maalumu, na kuweka mkakati wa kuviendeleza vipaji hivyoili kuondokana na utegemezi wa teknolojia za kigeni, 2. Tuliitaka Serikali kutoa taarifa(progressive report) juu ya utekelezaji wa Mtandao wa Taifa wa Elimu na Utafiti(National Education and Research Network-NERN),3. Tuliitaka Mamlaka ya Udhibiti waMawasiliano Tanzania (TCRA) kuongeza wigo wa mapato yanayotokana na makampuni ya simu nchini, na kuitakaserikali ufute misamaha ya kodi kwa makampuni ya simu nchini.4. Tuliitaka TCRA itoe bei elekezi kwamakampuni ya simu, ili wananchiwasiendelee kunyonywa gharama kubwa za matumizi ya simu,5. Tuliitaka Serikali kuthibitishakama ni kweli Jeshi la Polisi lilinunua mtambo Gi2 unaotumika kufanya "smsspoofing'' na madhumuni ya kufanya manunuzi hayo. Aidha, tuliitaka Serikalipia kuweka sheria ya kuthibiti matumizi ya taarifa za "smsspoofing" hapa nchini, kama zilivyofanya nchi ya Australia na Uingereza.6. Tuliitaka Serikali iandae utaratibuwa kisheria wa kupata mapato kutoka katika mifumo ya malipo ya kieletroniki kwa mfano "MobileMoney Transfer" kama vile M-PESAkwa Kampuni ya Simu ya Vodacom, Tigo Pesa kwa Kampuni ya simu ya Tigo, AirTel Money kwa Kampuni ya Simu ya Air Tel.7. Tuliitaka Serikali kuiongezea pesa Tume yaSayansi na Teknolojia ili iweze kufanya kazi zake kwa ukamilifu na kwa ufanisi.Mheshimiwa Spika, kabla ya kujielekeza katika masuala mahususi yamwaka mpya wa bajeti wa 2013/2014 unaotarajiwa kuanza mapema tarehe 1 Julai,2013, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, inaitaka Serikali kutoa taarifa(progressive report) ya utekelezaji wahoja za Kambi Rasmi ya Upinzani (zilizoorodheshwa hapo juu), ilizoitakaSerikali itekeleze tangu mwaka uliopita wa bajeti.HAKI YA MAWASILIANO NA KUPATAHABARIMheshimiwa Spika,Kupata habari na mawasiliano ni moja ya haki za binadamu. Mikataba ya Kimataifaya Haki za Binadamu inatoa haki ya kupata habari na mawasiliano. Kwa mujibu waIbara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (TheInternational Covenant on Civil and Political Rights)1966 "wananchi wanahaki ya kupata habari na mawasiliano". Mheshimiwa Spika,sio mikataba ya kimataifa peke yake inayotambua haki hii, bali pia Ibara ya 18(b)(c)na (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, inatamka wazi kwamba "kila mtu anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila kujalimipaka ya nchi. Mwananchi ana haki yakuwasiliana bila kuingiliwa, na ana haki ya kupewa taarifa kuhusu matukioyanayogusa maisha yake na shughuli muhimu za maisha yake".Mheshimiwa Spika,Pamoja na haki hii kutamkwa wazi na Katiba ya nchi yetu, na Mikataba yaKimataifa, Serikali imekuwa ikiwanyima wananchi haki hii kwa makusudi kupitia "hila"mbalimbali kama ifuatavyo: i. Kuhama Kutoka kwenye Mfumo waAnalojia kwenda kwenye Mfumo wa Dijiti.Mheshimiwa Spika,Mamlaka ya Uthibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliamuru vituo vyote vyaTelevisheni nchini kuzima mitambo ya analojia na kuvilazimisha kuingia kwenyemfumo mpya na wakisasa wa Digitali ambao unatumia Ving'amuzi kupata mawimbi ya "Televisheni". Mheshimiwa Spika,uamuzi huo uliwaathiri sana wananchi na taifa kwa ujumla kwani kulikuwa hakunamaandalizi ya kutosha, na pia wananchi wengi hasa wa vijijini wameshindwakununua ving'amuzi hivyo na kwa jinsi hiyo kukosa haki yao ya kikatiba yakupata habari. Mheshimiwa Spika,TCRA imechangia sana tatizo hili kwa kuwa mpaka sasa haijaweka udhibiti wa beiwala usambazaji wa Ving'amuzi na hivyo kuacha hali ya ushindani usio na afya kwawatumiaji wa huduma za ving'amuzi. Ving'amuzi vimekuwa vikiuzwa kwa bei ya juuambayo inafanya watanzania masikini kushindwa kununua na hivyo kuwakosesha hakiyao ya Kikatiba ya kupata mawasiliano. Aidha, TCRA haidhibiti usambazaji waving'amuzi jambo ambalo limesababisha kutokupatikana kwa ving'amuzi katikabaadhi ya maeno, na hivyo kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wanaotaka kununuVing'amuzi hivyo.Mheshimiwa Spika,Mbaya zaidi, baadhi ya ving'amuzi kwa muda mrefu tangu kuzimwa kwa mitambo yaanalojia vimekuwa havirushi matangazo ya vituo vya televisheni vya ndani yanchi, na cha ajabu katika taarifa ya Wizara kwa umma, Wizara iliwataka wananchiambao hawapati matangazo ya vituo vya television vya ndani ya nchi wawasilianena wauza ving'amuzi hili wapate suluhisho;Mheshimiwa Spika,kwa msisitizo naomba kuinukuu sehemu ya taarifa hiyo kama ifuatavyo: "Serikaliinapenda kuwakumbusha wananchi kuwa katika maeneo ambayo tayari kuna matangazoya televisheni katika mfumo wa dijitali, watumiaji wa televisheni wanatakiwakuhakikisha kuwa wanapata matangazo ya televisheni zote zenye leseni za kitaifabila gharama yoyote ile ya ziada mbali na gharama ya kununua king'amuzi(kisimbuzi) ambacho kinawezesha kuona matangazo katika mfumo mpya wa utangazajiwa dijitali. Stesheni hizo ni TBC1, ITV, Star TV, Channel 10, na East AfricanTV. Endapo matangazo ya televisheni ya vituo hivyo hayapatikani, wananchiwawasiliane mara moja na watoa huduma za ving'amuzi ili kuwasaidia kupatiaufumbuzi'' Taarifa hii ilitolewa na kutiwa siani na Mhe. Profesa MakameMbarawa Waziri Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tarehe 2 Aprili, 2013. Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inasikitishwa sana na tangazo la Wizara kwamba wananchiambao hawaoni matangazo ya vituo vya televisheni za ndani wawasiliane nawasambaza ving'amuzi. Hii ni kwa sababu Serikali ndio iliyotoa leseni kwawasambazaji wa ving'amuzi, na ndio inayojua masharti ya leseni hizo. Hivi Mwananchi masikini wa kijijini kwa mfanowa kijiji cha Mwamgongo, kule Kigoma au yule wa Liwale kule Lindi atapa wapinguvu na mamlaka ya kuyaambia makampuni ya usambaziji kwamba king'amuzi chake hakioneshimatangazo ya kituo cha televisheni cha ndani ya nchi?Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inaitaka Serikalikupitia Wizara hii kuacha mara moja kufanya mzaha na haki ya wananchi ya kupatahabari. Aidha Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa agizo leo hiikwa Makampuni ya usambazaji waving'amuzi kuhakisha kwamba vituo vyaTBC1, ITV, Star TV, Channel 10, na East African TV ambavyo vina leseni yakitaifa vinaendelea kurusha matangazo yake bure kupitia ving'amuzi kamailivyokuwa katika makubaliano ya wasambazaji wa vin'ngamuzi, wamiliki wa vituotajwa vya televisheni na TCRA. MAWASILIANO YA SIMU ZAVIGANJANIMheshimiwa Spika,Pamoja na TCRA kuzitaka kampuni za utoaji huduma za simu Tanzania kupunguzagaharama za kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno, makampuni hayo badoyana bei ya juu, hasa kupiga simu toka mtandoa mmoja kwenda mwingine, (interconnection charges) haliinayosababisha wananchi kumiliki simu au line zaidi ya moja. Mbaya zaidimakampuni ya simu yamekuwa yakiwatoza wateja pale wanapopiga simu kwenda hudumakwa mteja (customer care service) nahakuna viwango vyenye mlingano kati ya kampuni moja na nyingine. Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka Serikali kupitia mdhibiti wa mawasiliano ya simu TCRAkukataza mara moja makampuni ya simu kuwatoza wateja pale wanapo piga simu ilikupata huduma kwa wateja (customer careservices) kwakuwa wateja wanapofanya hivyo huwa wana jambo aidha lakiufundi au la kiutaratibu wanalotaka kusaidiwa na kampuni husika, na hakunafaida yoyote ya kifedha mpiga simu anayopata kwa kuomba msaada wa maelezokutoka kwa customer care.UTANGAZAJI REDIONI NA KWENYELUNINGAMheshimiwa Spika,Kwa mujibu wa Sheria ya Utangazaji ‘the Broadcasting Services Act', TCRAinawajibu wa kusimamia pamoja na mambo mengine maudhui ya matangazo kamailivyoainishwa na kanuni za udhibiti wa maudhui ya utangazaji za mwaka 2005 [theBroadcasting Services (Content) Regulations 2005]. Mheshimiwa Spika,kwa mujibu wa kanuni hizo, vituo vya redio na television vinakatwazwa kurushamatangazo yenye maudhui ya kibaguzi kam vile rangi, kabila, dini na aina zoteza ubaguzi. Aidha kanuni hizo zinakatazavyombo vya utangazaji kuibua chuki baina ya makundi tofauti katika jamii, nawakati wote kulinda umoja, uhuru, na maslai ya Taifa, na kudumisha maadili yakitaifa.
Mheshimiwa Spika, kanuni hizo piazinavitaka vyombo vya utangazaji kuwalinda watoto katika matangazo yao dhidi yalugha za matusi, na picha zisizofaa. Adhabu inayotolewa na Kanuni ya 28 yakanuni hizi kwa kituo kitakachokiuka kanuni hizi ni faini kiasi cha milliontano tu.
Mheshimi wa Spika,pamoja na kuwepo kwa kanuni hizi tangu mwaka 2005, vyombo vya utangazaji, rediona luninga vimekuwa vikivunja kanuni hizo, kwa kuonesha picha na kurusha matangazo yenyelugha ya matusi, zenye kuchochea chuki za kidini, na kisiasa, zinazo zoroteshamaadili na kutishia umoja wa kitiafa. Hivi karibuni kituo cha redio cha CloudsFm kilipigwa faini kwa kosa la kushabikia mambo ya ushoga, jambo amabalo nikinyume na maadili ya Taifa letu. Vituo vingine viwili vya redio Imani FM naKwa Neema FM navyo vimefungiwa. Kambi Rasmi ya Upinzani inahoji; ni liniSerikali ‘sikivu' ya CCM itaanza kuona kwamba vituo vingi vya televisheni naredio nchini vinaonesha picha na kurusha matangazo yaliyojaa maudhui yaliyopotoka kimaadili ilikuchukua hatua stahiki? Mheshimiwa Spika,kwa hali ilivyo sasa kwenye vituo vyetu vya redio na televisheni ni ushahidimwingine unaodhirisha ni namna gani Serikali ya CCM ilivyoshindwa kusimamia maadiliya Taifa letu, imeshindwa kusimamia maadili ya kisiasa, na sasa inaacha watotowetu waharibiwe kimaadili kwa kuviachia vitu vya redio na television kurusha picha na matangazo ambayo yanachocheammomonyoko wa maadili. MALIPO YA TOZO ZA MINARA YASIMU KWA HALMASHAURI Mheshimiwa Spika,katika taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Miundombinu kwa mwaka wafedha unaomalizika, ni kwamba, Wizara ilitakiwa kuwasiliana na TAMISEMI kuhusu kutofautiana kwa tozombalimbali za minara ya simu (land levy) zinazotozwa na Halmashauri hapa nchinikwa lengo la kuwianisha tozo hizo ili zifanane.Mheshimiwa Spika,pamoja na Wizara kuandaa mwongozo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI ambaoutaweka viwango vya kufanana vya tozo, Wizara imeenda mbele zaidi kuwekautaratibu wa kuwa na taasisi moja itakayo kusanya tozo kwa niaba ya Halmashaurizote kisha kuzigawa kwa Halmshauri husika. Mheshimiwa Spika,kwa utaratibu huu ni wazi kwamba taasisi (agency) itakayokusanya tozo kwa niabaya Halmashauri itahitaji gharama za uendeshaji na hivyo ni dhahiri itafanyamakato toka kwa tozo zinazokusanywa na matokeo yake ni kupunguza kiasi chamapato ambacho Halamshauri ingekusanya moja kwa moja. Kambi Rasmi ya Upinzaniinayoongozwa na CHADEMA inaitaka Serikali, kurekebisha Mwongozo uliotolewa na TAMISEMI kwa kuwa na kiwango kimoja cha tozo,na kuondoa taasisi moja ya ukusanyaji mapato kwani, kwa utaratibu wa kisheriauliopo Halmashauri inaweza kukusanya mapato yake yenyewe; na makampuni ya simuyanazo ofisi mikoani na hivyo wanaweza kulipa tozo hizo bila usumbufu wowote.MICHEZO YA BAHATI NASIBU KWENYE MITANDAO YA SIMUMheshimiwa Spika,Makampuni ya simu yamekuwa na utaratibu wa kufanya "promosheni" zinazohusishakuwakata pesa wateja wanaoshiriki promosheni hizo. Hata hivyo kumekuwa namalalamiko toka kwa watumiaji wa simu za mkononi kwamba mara kadhaa wameingizwakwenye promosheni hizo bila ridhaa zao na hivyo kukatwa pesa hali inayopelekeakupata hasara na usumbufu mkubwa. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kupitia TCRA na Bodi yaKusimamia Michezo ya Kubahatisha yaTaifa kuyataka makampuni ya simu kuweka utaratibu mzuri wa kucheza michezo hiyoili kuondoa usumbufu kwa wateja.Mheshimiwa Spika,Baadhi ya makampuni ya simu yamekuwa yakitoa huduma duni sana, na hivyo kuletausumbufu kwa wateja. Mathalani kuna wakati kampuni fulani inaweza kupotezakabisa "network" katika mkoa, au mji fulani na hivyo kukwamishakabisa mawasiliano, bila kutoa taarifa wala kuomba radhi wateja wake.Mheshimiwa Spika,katika zama, hizi ambazo mawasiliano yasimu yanawezesha shughuli karibu zote, kiuchumi, kijamii na kiusalama hali yakukatika kwa "network" ina hatarisha usalama wa maisha ya watanzania,ukizingatia mtandao wa simu unawezesha sio tu mawasiliano bali pia huduma za kibenki za watumiaji wake.UHIFADHI,NA UTUMAJI PESA KWA NJIA YA SIMU
Mheshimiwa Spika,Maendeleo ya sayansi na teknolojia yametufikisha mahali simu za kiganjanizimekuwa benki na makampuni ya simu yamekuwa taasisi za kifedha hapa nchini. Malipomengi yanafanywa kupitia huduma za M-pesa,Tigo-pesa, Airtel-Money, Z-pesa nakadhalika.Pamojana mamillion ya pesa yanayotumwa kila siku kupitia njia hii, na makato ambayomakampuni ya simu na mawakala wao wanayapata na kujichumia faida isiyo nakifani kupitia miamala hiyo Serikali haipati hata senti tano (5 Cent) kama kodikutokana na biashara hii, lakini wakati huo huo Serikali hii imekuwa ikitozataasisi nyingine za kifedha kama benki kodi chungu mzima. Kambi Rasmi yaUpinzani inayoongozwa na CHADEMA inaishangaa Serikali hii ya CCM inayojiita makini, kwa kushindwa kuandaa utaratibu utakaoiwezesha Serikali kupata faida kutoka na miamala ya pesa kwa njia ya simu ilikuchangia ongezeko la pato la taifa. Na katika hili Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inasisitiza sheria ya tozoitakapotungwa isilenge kuwapa mzigo watumiaji/ wateja wa mihamala hii, badalayake makampuni ya simu ndio walipe kodi na ushuru kwa serikali, bila kuathiriwateja.Mheshimiwa Spika,izingatiwe kwamba leseni za utoaji huduma za mawasilaino ya simu hutolewa kwamakampuni na TCRA, lakini leseni za utoaji huduma za pesa kwa njia ya simu hutolewana Benki Kuu ya Tanzania kwa mujibu wa Sheriaya Benki na Taasisi za Kifedha ya mwaka 2006 (Banking and FinancialInstitutions Act 2006). Hivyo Serikali lazima ielewe kwamba biashara hizi mbili nibiashara tofauti, watoaji leseni wake ni tofauti; hivyo serikali lazima ipatemapato tofauti kutoka makampuni haya, katika biashara ya mawasiliano, nabiashara ya pesa kwa njia ya simu.UHALIFU WA MITANDAONI (CYBERCRIME)MheshimiwaSpika, Kumeibuka wimbikubwa la uwizi kwa njia ya mtandao. Mamilioni ya pesa yameibwa kwenye taasisimbalimbali, hasa mabenki, machine za kutolea pesa (ATM) na miamala mingineinayofanyika kwa njia ya kompyuta vimeendelea kuzitia hasara taasisi za kifedhanchini. Kwa mfano, tarehe 14 mwezi Febuarimwaka 2013 watuhumiwa wa wizi wa fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kupitia kwenye ATM, walikamatwa mkoani Mwanza. Huu ni mfano mmoja tu, lakini kesi za uwizikwa njia ya ATM zimekuwa zikiripotiwa kila mara katika maeneo tofuauti nchini.MheshimiwaSpika, pamoja na wizi,kuna uhalifu mwingine unaofanyika kwa njia ya mtando kwa mfano, ubadhirifu kwanjia ya kompyuta (computer fraud), kuingilia mawasiliano (haking) nakadhalika.MheshimiwaSpika, waathirika wauhalifu huu ni pamoja na taasisi za kiserikali, mabenki, biashara binafsi, vyuovya elimu, wanasiasa wanaofanyiwa ushushushu, na jamii kwa ujumla. Pamoja nahali hii, Tanzania haina Sheria mahususi inayodhibiti uhalifu kwa njia yamtandao. Mabadiliko madogo yalifanywa kwenye Sheria ya Ushahidi (the Lawof Evidence Act) na Sheria ya Kanuniza Adhabu (the Penal Code) hazitoshi kudhibiti aina zote za uhalifu kwanjia ya mtando; hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali ilete muswada waSheria mahususi kwa madhumuni ya kudhibiti uhalifu huu wa kimtandao.Mheshimiwa Spika,katika hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani tulihoji juu ya kuwepo kwa taarifa zaJeshi la Polisi kuhusika na ununuzi wa mtambowa kijasusi wa Gi2 unaotumika kufanya ''sms spoofing'' yaani kutuma ujumbemfupi wa maneno kwa kutumia namba ambayo kiualisia mwenye namba hiyo hajatumaujumbe huo, isipokuwa ni kuingilia kihalifu mawasiliano (cyber trespass) ambapomtumaji anafanya " impersonation".Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya upinzani inataka kujua ni lini Serikali itaweka sheria ya kudhibiti matumizi ya taarifa za "smsspoofing" hapa nchini ama kukubaliana na matumizi yake au kupigamarufuku kama walivyofanya nchi ya Australia na Uingereza.KUONGEZA PATO LA TAIFA KUPITIAMAWASILIANOMheshimiwa Spika,katika hotuba ya bajeti ya Wizara hii ya mwaka 2012/13 Wizara iliahaidi kuanzakutumia mtambo wa kuhakiki mawasiliano (Tarrif Monitoring System-TMS) ilikuhakiki mapato yanayotokana na mawasiliano ya simu. Wizara ilijinadi kwamba imeanza mchakoto huomwezi juni mwaka 2012. Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kujua ni hatua ganimchakato huo umefikia?Mheshimiwa Spika,katika kiambatanisho namba 2. cha hotuba ya bajeti ya mwaka jana ya Wizara hiichenye kichwa UWEKEZAJI NA MCHANGO WAWATOA HUDUMA ZA SIMU ZA MKONONI KUPITIA TEKNOLOJIA YA GSM TANZANIA, Wizara ilishindwa kutoa taarifa za kikodiza kampuni za simu za TIGO,AIRTEL, ZANTEL kwenye baadhi ya aina ya kodi.Taarifa ya kodi ya Makampuni (Corporate tax) iliyolipwa na Kampuni ya TIGOhazikupatikana, taarifa ya malipo kwenye mfuko wa mawasiliano kwa wote(2009-2011) za kampuni ya Zantel hazikupatikana, taarifa za kiasi cha fedhazilizotumwa (mobile money transaction) cha kampuni ya AIRTEL, na Zantelhazikupatikina, Taarifa za mchango wa kijamii (Corporate Social Responsibility)wa kampuni ya Zantel hazikupatikana.Mheshimiwa Spika,Kitendo cha Serikali hii ya CCM kushindwakupata takwimu ambazo nyingine zinatakiwa kutolewa na makampuni kisheria nimuendelezo wa uthibitisho wa kushindwa kwa Serikali hii kutawala Taifa hili.Kitendo cha Serikali kushindwa kupata taarifa hizi kuna ashiria uzembe narushwa. SERIKALIKUMILIKI TTCL KWA 100%Mheshimiwa Spika,Serikali imeanza mchakato wa kumiliki Shirika la Mawasiliano ya Simu la Taifa (TTCL)kwa asilimia mia moja (100%) kwa kununua asilimia 35% ya hisa za M-bia mwenzakampuni ya AIRTEL. Kambi Rasmi ya Upinzani inakubaliana na hatua hii kwakuzingatia umuhimu wa Wananchi kupitia Serikali kumiliki sekta ya mawasilianoya simu kwa umuhimu na unyeti wake. Hatahivyo Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Serikali kuweka wazi tathimini ya bei yahisa za AIRTEL kabla ya ununuzi wa hisa hizo na mkataba wa mauzino hayo uwekwe wazi na uridhiwena Bunge lako tukufu, ili kuziba mianya ya ufisadi, na kulipa Bunge haki yakeya kuisimamia Serikali.UVUMBUZI WA KISAYANSIMheshimiwaSpika, naomba kunukuu sehemu ya hotuba ya Kambi Rasmiya Upinzani iliyowasilishwa ndani ya Bunge hili tukufu katika mwaka wa fedha2012/13 kuhusu rai ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuibua na kuendeleza vipajimaalumu vya kisayansi na teknlojia miongoni mwa wanafunzi wetu na wananchiwengine wenye vipaji hivyo. Sehemu ya hotuba hiyo inasema hivi: "Mheshimiwa Spika, hakuna mkakati wa kuibuana kuwendeleza wabunifu katika kuibua na kuendeleza Teknolojia hapa nchini.Pamoja na nchi yetu kuonekana kuwa na vijana wenye uwezo wa hali ya juu katikakubuni na kuendeleza Teknolojia itakayoweza kuinua uchumi wa nchi, serikaliimeshindwa kutambua fursa hiyo na kuwaendeleza wabunifu hao. Mfano ni kijanaFrank Waya kupitia kipindi cha Jenerali on Monday kinachorushwa na Televisheniya Channel Ten ameonyesha uwezo mkubwa katika kubuni Teknolojia ambayoikiendelezwa itasaidia sana taifa katika kuleta maendeleo.Mheshimiwa Spika,kupitia kipaji alichonacho, ameweza kuonyesha jinsi Teknolojia ya simuinavyoweza kutumika katika kutengeneza mfumo wa kuzuia vyombo vya motokutoungua kutokana na shoti ya umeme na hata kutumia simu kwa ajili yaumwagiliaji wa bustani na shamba kwa kutumia pampu ya maji hata mtu akiwa mbalina shamba au bustani. Pia ameonyesha uwezo wa kutengeneza inventor inayowezakukaa na umeme kwa siku 7 baada ya umeme wa Tanesco kukatika. Hiki ni kipajicha hali ya juu ambacho kikitumiwa vizuri na kuendelezwa, kitasaidia taifa hilikupiga hatua ya kimaendeleo.Kambi ya Upinzaniinataka kupata majibu kuna mkakati gani wa serikali wa kuhakikisha kuwa vipajikama hivi vinaendelezwa katika nchi yetu, na je wenye vipaji kama hivi ni nanimwenye wajibu na jukumu la kuviendeleza na kuvikuza?"Mheshimiwa Spika, nimwaka mmoja umepita sasa tangu Kambi Rasmi ya Upinzani itoe rai hii kwaSerikali kuibua na kendeleza vipaji vya namna hii. Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inataka kujua Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, imeibua nakuendeleza vipaji vingapi ili kutimiza dira na dhima ya wizara hii yakuwajengea uwezo wananchi wa kisayansi, kiteknolojia na ki-uvumbuzi ilikukabiliana na ushindani wa kimataifa na hivyo kuleta maendeleo endelevu yakiuchumi?Mheshimiwa Spika,Katika muhtasari wa taarifa ya utekelezaji (Perfomance Review 2012/2013) Wizarailieza kuwa Serikali inatumia Tume ya Sayansi na Tekinolojia kufanya tathiminiya ugunduzi ili kuweza kurasimisha ugunduzi huo, na kwamba inaanda sera yaSayansi, Teknolojia na Ubunifu, na kwamba kuna sheria inaandaliwa ili kuwahamasisha,kuwasimamia na kuwalinda wagunduzi. Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutumia sheria ambayo tayari ipo,Sheria ya Usajili wa Uvumbuzi, ya mwaka 1994, Sura ya 217 ya sheria zetu. [the Patents (Registration) Act, 1994 Cap217] ambayo kwa mujibu wa jina refu (long title) ya sheria hiyo, madhumuniya sheria hiyo ni; Sheria ya kusajili uvumbuzi, kuweka mazingira bora ya kuhamasishauvumbuzi na ugunduzi ili kuwezesha kupata teknolojia katika misingi ya usawakupita, kutoa na kuratibu uvumbuzi, kutoa vyeti vya bidhaa gunduliwa, na vyetivya ugunduzi. kwa kiingereza "AnAct to provide for the Patents Registration so as to make better provisions forthe promotion of inventivity and innovation for the facilitation of theacquisition of technology on fair terms through the grant and regulation ofpatents, utility certificates and innovation certificates". Mheshimiwa Spika,kama serikali inaona vifungu vya sheria hii ambayo tayari inatumika havitoshi,ni vyema ikaileta sheria hii Bungeni ili tuifanyie marekebisho kwani ni wazikusubiri mpaka mchakato wa maandalizi ya sera na sheria mahususi unacheleweshauendelezaji wa vipaji vya wabunifu wetu, hasa kwa kuzingatia kuwa Serikalihii imekuwa madarakani kwa miaka zaidiya 50 na haijawahi kuona umuhimu wa kuwa na sheria hii kwa wakati wote huo.TEKNOLOJIAYA BIO METRICK VOTERS REGISTERMuheshiwa Spika,Dunia imeshuhudia mikanganyiko na migongano iliyohatarisha amani na utulivu wanchi kadhaa zilizojaribu kutumia mtambo wa Bio Metrick Voters Register katikachaguzi zake mbali mbali, mifano ya hivi karibuni ni ya Nchi za Ghana na Kenya.Mitambo ya aina hii inatumia teknolojia ya juu inayotaka mazingira mazuriyaliyoandaliwa. Katika mazingira ya nchi masikini, yenye kitekinolojia duni na ambayo hata robo ya eneo la nchi hainaumeme kama Tanzania, ni jambo linaloshangaza kuona tunataka kutumiateknolojia hii. Ni lazima tukumbuke msemo usemao, ukiona mwenzio kanyolewa,wewe tia maji.Mheshimiwa Spika,Bila kujali hali duni ya kiteknolojia inayoikabili nchi yetu, Serikali ya CCMkupitia tume ya uchaguzi imeanza mchakato wa kununua mtambo wa Biometrick VotersRegister (BVR) kwa mabilioni ya fedha za wahisani. Kambi Rasmi ya Upinzaniinayoongozwa na CHADEMA inaitaka serikali iache mara moja mpango huo na badalayake ifanye marekebisho kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.Mheshimiwa Spika,ninayasema haya kwakuzingatia kuwa, ukiacha riporti kadhaa zinazoelezea uduni wa maendeleo ya kisayansi nateknolojia nchini, sisi wote humu ni mashaidi kwamba asilimia 80 ya maeneotunayotoka hayana umeme.TUME YA TAIFA YA SAYANSI NATEKNOLOJIAMheshimiwa Spika,Tume ya Sayansi na Teknolojia inawajibu wa kusimamia na kuratibu tafiti zakisayansi na teknolojia. Pamoja na tafiti nyingi zilizifanywa na wanasayansimbalimbali nchini. Matokeo ya tafiti hizo zimekuwa haziwafikii walengwa.Mathalani tafiti zinazogusa sekta ya kilimo, zimeendelea kuishia kwenye vitabu,na kushindwa kuwafikia wakulima vijijini. Hili linatokana na kukosekana kwauratibu kwa upande wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).Mheshimiwa Spika,katika mwaka wa fedha 2012/2013 Serikali ilitenga kiasi cha bilioni 26 namilioni 476 na 961 elfu (26,479,961,000), kwa ajili ya utafiti. Hata hivyo,kiwango hicho cha fedha kimepungua katika bajeti ya mwaka 2013/2014 ambaposerikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 16.5 tu kwa ajili ya utafiti.Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo mbele ya Bunge hili nikwa nini fedha za utafiti zinapungua wakati jukumu kubwa la Tume ya Sayansi naTeknolojia ni kufanya utafiti? TAASISI ZA MAFUNZO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIAMheshimiwa Spika,kuna ulazima wa kupandishwa hadhi kwa Taasisi za mafunzo za Sayansi naTeknolojia nchini. Kupandishwa hadhi kwa taasisi zetu na kuwa vyuo vikuuvinavyotoa shahada za ngazi mbalimbali sio tu itaongeza fursa za kujiendelezakimasomo kwa wanasayansi wetu nchini, lakini pia itakuza wigo wa maendeleo ya sayansina teknolojia nchini na hivyo kuleta maendeleo ya kiuchumi, na kukuza ustawi wawananchi, ukizingatia kuwa tunahitaji wataalamu wa ndani katika sekta yasayansi na teknolojia ili kulisaidia taifa kujitegemea.Mheshimiwa Spika,Taasisi ya Sayansi na Teknolojia-Mbeya bado haijapata ithibati ya kudumu tokaTume ya Vyuo vikuu, ili kuwa Chuo kikuu kamili, Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwana CHADEMA inaitaka Serikali kutamka mbele ya Bunge hili kuwa ni lini taasisi hiyo itapata ithibati ya kudumu, kwakuzingatia umuhimu wa kuwa na Vyou vingi vya Sayansi na Teknolojia nchini kamanilivyoeleza hapo juu.Mheshimiwa Spika,Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) ni moja ya taasisi kongwe nchini. Hata hivyo, pamoja na taasisi hii kuwepo kwamiaka mingi, kasi ya kukua kwake sio ya kuridhisha, ukilinganisha na umri wake.Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuongeza kasi ya ukuaji na kuiwezeshaDIT kuwa na matawi kila mkoa, kama zinavyofanya taasisi nyingine za kitaalumanchini, husasani vyuo vikuu.Mheshimiwa Spika,taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela-Arusha ni taasisi mpyakiumri. Ili kukuza na kuiendelezataasisi hii serikali inao wajibu wa kuitengea fedha za kutosha katika bajeti hii ili kuijengea uwezo wa kiutendaji.Mheshimiwa Spika,maendeleo na mafanikio katika taasisi za taaluma za sayansi na teknolojianchini zinategemea kwa kiasi kikubwa maandalizi ya wanafunzi yanayo paswa kufanywakatika ngazi za chini za elimu yao. Kwa hali hilivyosasa ambapo wanafunzi washule za msingi wanasoma masomo ya sayansi bila kuwa n mahabara wala maktaba,wanasoma somo la TEHAMA bila kuwa na kompyuta- na asilimia zaidi ya 90 ya shuleza msingi hazina umeme, ni wazi hawawezi kuwa na uwezo wala motisha ya kupendakusoma masomo ya sayansi. Hali hiyo pia imetamalaki kwenye shule za sekondari. Mheshimiwa Spika,kama hali hii ya wanafunzi kutoandaliwa mazingira ya kupenda masomo ya sayansiitaendelea kukua na kukomaa, utafika wakati taasisi zetu za sayansi nateknolojia zitakosa wanafunzi wa kitanzania wa kuwadahili, na hivyo taasisizetu ama zitakufa, au zitaishia kudahili wanafunzi kutoka nchi za nje.Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Wizara ishirikiane na Wizara ya Elimu kuwekamazingira yenye afya kwa ustawi wa masomo ya sayansi hili kuhamasisha wanafunzikupenda masomo ya sayansi. Aidha Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikuweka vivutio kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi kama vile kuwalipia karowanafunzi wa sayansi ngazi za sekondari na kuwapa mikopo asilimia mia moja kwa wale watakaoendelea na masomo yajuu katika taasisi za sayansi na vyuo vikuu.MGAWANYO WA FEDHA ZA MAENDELEOYA 2013/2014Mheshimiwa Spika, Wizarahii imetengewa kiasi cha millioni miambili 200,000,000 kwa uanzishaji wa vituo vya jamii vya mawasiliano Vijijini,lakini kwa mujibu wa idadi, ukubwa na umuhimu wa kazi zilizipongwa katika fungu hili ni wazi kuwa kiasi hicho cha fedhani kidogo sana na hakiwezi kukidhi malengo yanakusudiwa. Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka Serikali iongeze pesa kwenye fungu hili ili kuchagizamaendeleo ya mawasiliano ya Internetvijijini kwa mustakhabali wa mendeleo ya vijiji vyetu.Mheshimiwa Spika,baada ya kusema hayo kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani naomba kuwasilisha.
_______________________________________

Susan Jerome Lyimo (Mb)

MSEMAJIMKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

NA

WAZIRIKIVULI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Imesomwaleo, tarehe 3 Juni, 2013
 
Back
Top Bottom