Hotuba ya Rais na Mashine za Kutoza Kodi za TRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Rais na Mashine za Kutoza Kodi za TRA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Old ManIF, Apr 3, 2011.

 1. O

  Old ManIF Senior Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kati ya mambo aliyoyaongelea ni kuhusu suala hili la kutoza kodi kwa kutumia mashine hizi. Alisema anawaomba wafanyabiashara watoe ushirikiano kwa kutumia mashine. Sasa ninajaribu kujiuliza ushiriano huu utawezekana vipi ikiwa hao TRA wenyewe tangu mwanzo hawajatoa ushirikiano kwa wafanyabiashara? Wao wameleta mashine, wamewateua wasambazaji, wamepanga bei za hizo mashine wanawalazimisha wafanyabiashara wazinunue na hakuna ushahidi wowote kuwa katika michakato hii wafanyabiashara walishirikishwa sasa leo wanakuja from no where wanawaomba ushirkiano.

  Wanasema kuwa gharama za mashine zitarejeshwa kwenye marejesho ya VAT lakini wanachoshindwa kutuambia ni utafiti upi waliufanya wakaona kuwa kila mfanyabiashara anayelipa VAT anauwezo wa wakati mmoja kutoa fedha cash za kuinunua mashine na kuikopesha TRA na serikali ili baadaye wa mlipe kwa kukata kwenye marejesho ya VAT. Je serikali na TRA watamlipa Interest kiasi gani mfanyabiashara kwa huu mkopo wanao mkopa? Huu ununuzi wa hizi mashine ni ufisadi mwingine kama ilivyo Dawans, Richimond n.k. Mabilioni ya fedha za kodi zitakazokatwa kwenye marejesho ya VAT ni hela za walipa kodi wa TZ ambazo wanataka kuziiba kwa staili hii mpya kabisa. Hivyi haya makampuni ni yakina nani hasa? TRA waliyapata kwa kupitia utaratibu gani? Tutaendelea kuibiwa na kuonewa na viongozi kwa kutumia serikali yetu mpaka lini?

  Anasema huu ni utaratibu utakao waondolea wafanyabiashara usumbufu. Yeye na serikali ya ccm kumlazimisha mfanyabiashara kutoa sh 1,100,000 mapaka millioni 3,000, 000 kwa wakati mmoja tena cash sio tatizo wala usumbufu, kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Inasemekana mashine hizi zinaweza kupatikana sehemu nyingine chini ya bei hizi ambazo sasa hivi huyu mfanyabiashara analazimishwa kunununua, kwa nini katika kipindi hiki cha soko huria wafanyabiashara wasipewe specifications za mashine wakanunua wenyewe kokote wanako weza kuzipata kwa bei nafuu? Huu kweli si ufisadi na utapeli mwingine tunao ushuhudia hapa Tanzania.

  Mashine hizi baada ya kukatwa gharama zake kwenye marejesho ya VAT kimsingi zitakuwa mali ya Serikali kwa kupitia TRA, hii haingii akili kwanini serikali kwa kupitia TRA wasinunue machine hizi wao na kuja kuziweka kwa wafanyabishara ili wazitumie badala yake wanawalazimisha wafanyabiashara wa wakopeshe mabilioni haya ya fedha? Hapa kuna harufu ya ufisadi ambao hatujaustukia.

  Kama serikali na TRA wanaamini kwa dhati kabisa kuwa mashine hizi zitaongeza ukusanyaji wa kodi katika mazingira haya ya TZ ya ukatikanaji wa umeme na si mradi mwingine wa kifisadi kwa nini wasinge enda wao kukopa bank, kutafuta grands au hata kuwaomba wafadhili wa wasaidie katika kufanikisha mradi wa kuweka mashine hizi?

  Kimsingi nakubalina na serikali katika juhudi zake za kuongeza ukusanyaji wa kodi ambazo zitatumika vizuri kusaidia kuboresha kumhudumia mwananchi wala sio kama sasa ambapo zinatumika katika maisha ya kifahari ya viongozi wetu huku wakijua kuwa hii ni nchi maskini ( mfano tumejionea wenyewe kwenye Tsunami ya japani aina ya magari waliyo nayo ukilinganisha na haya yanayotumiwa na viongozi wetu tena mbaya zaidi wengine kutokea nyumbani Masaki kwenda ofisini mt wa Samora). Ila sikubaliani na watu wanaotumia mwanya huo kuwaibia wananchi ili wajinufaishe hii si haki na wananchi tupinge uonevu huu wa wazi kabisa.
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mashine zenyewe mbovuu, tunayo hata haifanyikazi. Bei kubwa. Mkuu wahidi wa BMTL wameamua kulitafuna taifa, wizi wizi tupu... Mashine mpya mbovu ikimaliza mwaka?
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii ni kawaida kwenye nchi zetu kutafuna nchi kwa kuwatumia maburushi!
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,489
  Likes Received: 5,579
  Trophy Points: 280
  Binafsi naona huu utaratibu wa mashine ni mzuri kwa kukusanya kodi na itapunguza nafasi za kukwepa kodi.nafikiri kwanza tupongeze kwa hiyo hatua lakini mchakato wa kupata makampuni ya kutoa hizo machine haukuwa wazi na pengine utaratibu umefuatwa ila kwa mazingira ya sasa ya nchi yetu ni bora kuwa wazi maana hatuaminiani tena na tuna loop holes nyingi kimifumo na sheria zetu.pia wasiwasi wangu zaidi ni jinsi TRA walivyojipanga na huu utaratibu mpya maana unaitaji very quick response linapotokea tatizo popote kama muongozo wao wa mashine hizi unavyosema.pia strategies hizi za kukusanya kodi ziende sambamba na maendeleo yanayoonekana na sio kulipia madudu kama dowans maana hapa anaezidi kubanwa ni mwananchi hivyo yakiwepo maendeleo ushirikiano utakuwepo otherwise ni bomu jingine hilo.
   
 5. R

  Reyes Senior Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bei ya mashine moja haifiki dola 200, kwa nini ziuzwe milioni 3? huu ni ufisadi mwingine
   
 6. O

  Old ManIF Senior Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiongozi wewe umesema, ndio maana sisi wengine tunapata taabu sana kwa kujiuliza hawa viongozi wetu wako kwa ajili ya kuwatumikia wananchi au kushirikana na mafisadi kuwaibia wananchi tena bila ya huruma. Ila tunasema haya yana mwisho wake tena kwa yeyote mwenye busara mwisho huu hauko mbali sana, tusubiri tutaona.
   
 7. O

  Old ManIF Senior Member

  #7
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mh Mtazamo naona wewe umepongeza huu utaratibu, labda tusaidie umesikia wapi tukiambiwa kuwa TRA wana wafanyabiashara wangapi wanaolipa kodi ya VAT na hawa wafanyabiashara watakapo kuwa wote wameikopesha serikali kwa kupitia TRA wanapo nunua mashine hizi serikali itakua imetumia kodi kiasi cha billioni au trilioni ngapi kwa makato ya marejesho ya VAT?


  Je serikali na TRA wange tafuta sorce ya fedha kwa kukopa kwenye taasisi za fedha au kuomba misaada wakatangaza tender ya wazi na kupata mashine hizi na wakawapelekea wafanyabiashara kuzitumia wangekuwa wametumia kiasi pungufu au zaidi ya hiki watakachotumia sasa kwa kumkopa mfanyabiashara? Maswali kama haya na mwengine ndiyo yanayotufanya wengine tuwe na mashaka je huu si mradi wa kifisadi? Kuna taabu gani ya serikali na TRA kuwa wazi kwenye mambo haya kama kweli nia yao ni njema?
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,489
  Likes Received: 5,579
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimeandika kwa hoja tatu za msingi,kwanza kusifia system hiyo mpya ya kukusanya mapato na nafikiri mtu yeyote mwenye nia njema ya serikali kuongeza mapato kupitia kodi ataona hilo.pili ni kuunga mkono hoja yako hasa mchakato wa kupata wazabuni na gharama za machine hizi kwa tax payer lakini pia kwa serikali huku wazabuni hao wakivuna superdupa profit na tatu nikatoa angalizo la kasi ya mbinu ya kukusanya kodi wananchi waone faida zake na sio kupewa takwimu za kiasi cha mapato kinachoongezeka kila mwezi.
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,489
  Likes Received: 5,579
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimepanua tu wigo wa hoja ili maana nzima ya huo udhaifu ionekane vizuri,ni maoni yangu tu kwa uzoefu wangu mdogo wa kodi.
   
 10. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Kaka sio WAHINDI ni WABONGO wenzetu tu hapo watakuwa wamekula COLABO na WAHINDI wao wanapata cha juu, unaweza kukuta MHINDI alitenda 200,000/= WABONGO waka weka 1,000,000/=
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hapo ndio tatizo lilipo, wabongo kila kazi wanachakachua kisha ndio hao hao utawasikia wa kwanza kulaumu na kulalamika!
  Hata aje kiongozi gani, kama watu wet ndio hawa na hulka ya udokozi (... na kutaka kuvuna usichopanda) hatutafika kokote.
   
 12. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Nimenunua hiki kimachine kwa 1.7million toka Pergamon Agency. Ni zaidi ya siku 10 toka walivyokiacha kwa madai wanaenda kumalizia kuunganisha na TRA.
  Kwenye hivyo vimachine connection kati yangu na TRA ni Vodacom, kwa nini isiwe TTCL ambayo ni cheap na ni shirika la umma?
   
 13. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kuna training na technical support ya namna ya kuitumia hiyo machine effectively
   
 14. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Umesahau kuwa WAKUU wametoka juzi tu IKULU, TTCL washaiua siku nyingi lakini ukweli ni kwamba makampuni yote ya simu bila TTCL hayawezi kufanya kazi, Wote bado wanaitegemea TTCL.
   
 15. O

  Old ManIF Senior Member

  #15
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu wewe wanena na mwenye akili ajiulize hiyo Vodacom wamiliki wake kina nani? Halafu ujiridhishe huu si ufisadi mwingine unaofanywa na Mafisadi walewale wanaolindwa na viongozi wetu na wakati huohuo wakishirikina na viongozi kupanga deals za kuibia nchi hii.


  Nani anaweza kutuambia Pilot project ya huu utaratibu ilifanywa lini na ikaonekana inatija ili tuaminishwe kuwa jumuiya yote ya wafanyabiasha wanaolipa VAT ikiingizwa itasaidia kuongeza makusanyo ya kodi?


  Wakati umefika wananchi wanaoitakia mema nchi hii na hasa vizazi vijavyo wakatae uhuni huu wa viongozi wetu wanaoambukizwa na mafisadi.
   
 16. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nchi yoyote lazima wanainchi wake walipe kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi! Hili ni muhimu sana. TRA ilitakiwa itenegeneze mazingira mazuri ya Watanzania kupata machine hizi kwa ghrama nafuu. Bei ya computer set pamoja na kile kidrawer cha kuhifadhia fedha haizidi dola 450. Sasa unapokuja na kumwambia eti mteja ajilipie halafu mtarejesha hii sio sawa. Tanesco wameanzisha LUKU lakini wanahakikisha kuwa wateja wanapotaka kuunganishiwa umeme wanawapatia luku. Sasa hawa wenzetu wanataka tujinunulie sisi wenyewe huo ni wizi. TRA wanunue hizi mashine wazifunge kwa wateja na wao.
   
 17. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  duuuh mil 3!!! kwa hiyo hizo mashine ni kwa ajili ya wafanyabiashara wa aina gani?:confused3:
   
 18. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ama wao watupe uhuru wa kununua halafu tuwapelekee receipts watakachokifanya wao ni kutuma watu wao wa IT waje kufanya configurations tu. Tuone kama hatujazipata hizi machnes kwa laki nne
   
 19. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nakwambia hakuna kitu hapo tunakamuliwa tu. Taasisi ya kiserekali inapoamua kufanya biashara na mtu binafsi elewa wazi kuwa kuna kinachooendelea nyuma ya pazia. TTCL ina mtandao nchi nzima na tena kwa sasa ndo wenye internet yenye uhakika zaidikuliko mtandao mwingine wowote. Iweje tenda ya mawasialiano ya taasisi ya kiserekali ipitishiwe kwenye kampuni ya mteja aliyesajiliwa na shirika lililo chini ya serikali kuu? Kama JK angekuwa na nia ya dhati na nchi hii angeiwezesha TTCL kushirikiana na TRA wangeuza machine hizi kwa bei nafuu then wananchi wangekuwa motivated kufunga mchine na hata wafanyabiashara wadogo wangemudu (maana ndio wengi) kufunga na tungeongeza kipato kwa serekali.
   
 20. LD

  LD JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dah, wamekuja juzi kwenye kaduka kangu, kunilazimisha ninunue hichi kimashine. Eti na faini juu kwa kuchelewa kununua.
   
Loading...