Hotuba ya Rais Magufuli kwa Kiingereza kwenye ziara ya Waziri Mkuu wa India

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Baada ya rais Magufuli kusoma hotuba yake kwa lugha ya Kiswahili baadae ilitolewa kwa lugha ya kiingereza kwa manufaa ya wageni wasiojua Kiswahili.

Mimi najiuliza je Yeye angeenda India au China kisha hotuba ikatolewa kwa kihindi na waziri mkuu wa India au kichina na rais wa China halafu baadae anakuja mtu mwingine ambaye hajui hata kusoma hotuba vizuri na English yake sio nzuri akawahutubia kwa Kiingereza wangejisikiaje?

Nadhani watajirekebisha wakati ujao

 
Mbona huyo Dada anayesoma mwenyewe hajiamini.? Anakosea Mara kadhaa. Je,hakuna waliobobea katika lugha kuongea na kuandika? Hata Neno Tanzania linamtatiza Mara kadhaa kulitamka.

Kuna Siku Gerson Msigwa aliongezea vema Sana. Kwa nini asingepewa hiyo nafasi?

Hotuba haisomwi kama story. Lazima Mara kadhaa uinue USO wako na kuiangalia hadhara yako. Aaagh!
 
Ewe Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema muumba mbingu Na nchi nakuombe uturehemu watanzania.....jamani kwa nn hata wasingemchukua Pascal akasoma hyo hotuba ya kiingereza....mbona Jamaa ngeli yake imetulia sana...huyo mama....duuu
 
prior preparation prevents poor performance, huu msemo unasaidia eti kujificha kwenye kichaka cha kuendeleza kiswahili ambacho hata hueleweki basi kama akitaka kuendeleza aombe watu wa mwambao wawe wanatolea hotuba maana walau ndo wanaweza kiswahili na siyo sisi wa bara intereor.
 
Rais akihutubia kwa kingereza watanzania 20% ndio wataelewa kinachozungumzwa .

Kwa nini uwanyime 80% ya watanzania kuelewa kinachozungumzwa kwa kisingizio cha kuwafurahisha mabalozi wasiozidi 10??

Kiswahili kwanza English baadae.


Go my lovely presidaa
gud umeongea vema
 
Duh..... Hii ni ya mwaka.

Kwa hiyo Wageni wamekuwa pale kusikiliza hotuba in two versions; Kiswahili na Kingereza!!?
Bila kujali nitatukanwa kiasi gani na wakereketwa wa mtukufu, siogopi kusema hii ni aibu ya "miaka". Pia ni uthibitisho wa kukosekana kwa uratibu makini wa shughuli yote hiyo. Kwa maoni yangu palipaswa kuwa na mtafsiri mmoja anayesimama wakati huo huo na mahali hapo hapo kutafsiri sentesi kwa sentesi hotuba ya raisi. Alternatively, maandalizi mazuri yangehisisha mtafsiri asiyeonekana kwa wote na tafsiri yake ingeandaliwa mapema na kwa speed tarajali ya mhutubiaji halaf wachache wasiojua kiswahili wasikilize kwa lugha yao kwa kutumia vile vi-gadjets. Kwa namna hiyo nafikiri azma ya raisi kudumisha kiswahili ingefanikiwa.

Kusomewa hotuba na mtu mwingine wakati mwenye hotuba yupo ni kuonyesha udhaifu au upungufu mkubwa katika uratibu ambao ungeficha udhaifu wetu usionekane.

Hili kosa halipaswi kurudiwa!
 
Back
Top Bottom