MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Akiwa njiani kuelekea Singida kwenye sherehe ya CCM kutimiza miaka 39, Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi mbali mbali njiani wakitaka kumweleza matatizo mbali mbali yanayowakabili katika maisha yao.
Rais ameahidi kuzishughulikia changamoto za migogoro ya wakulima na wafugaji hasa mapambano yanayotokea mara kwa mara kati yao. kwa upande mwingine amesema sehemu ambayo wananchi wanapigana mara kwa mara mpaka kusababisha mauwaji kutokana na migogoro ya ardhi, viongozi wa maeneo hayo kuanzia Wakuu wa Mikoa mpaka watendaji wa vijiji watakuwa hawana sababu ya kuendelea kuwa viongozi wa maeneo hayo kwa sababu hiyo ni ishara kuwa wameshindwa kazi. Kama hawatajiondoa, yeye atawafukuza kazi.
Amewakumbusha adhima ya serikali yake kwa wawekezaji wa viwanda na mashamba ambao walichukua mashamba na viwanda lakini wameshindwa kuendeleza. Serikali ina mpando wa kuvichukua hivyo viwanda na mashamba ili kuwapa wananchi wengine.
Hii ni moja ya hotuba yake akiwa njiani kuelekea Dodoma.
VIDEO:
Msafara wa Rais Magufuli ukiwa njiani kuelekea Singida.
Rais Magufuli akiongea na wananchi katika maeneo mbali mbali akiwa njiani kuelekea Dodoma.
Rais Magufuli akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa . Sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS.