Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Katika hotuba hii sioni nia ya serikali kutatua tatizo la mgomo wa Madaktari na hotuba hizi zinaongeza mafuta kwenye moto unaowaka,na kauli ya JK hapo penye rangi nyekundu ni ushahidi tosha katika swala la Dr.Ulimboka JK ana uhakika gani ya kua hao waliomshahuri hasihusishwe walidhia uamuzi wake?Kwa vile walipewa jukumu la kuendesha mazungumzo kutoka upande wa serikali waliona Ulimboka ni kikwazo katika kufikia makubaliaono ya fast fast na serikali hivyo wakaona njia pekee ni kumuondoa.Kwa kauli ya JK sina mashaka ya kua swala la Ulimboka mkono wa serikali upo.
 

Wanajamvi: Nimekitafakari sana kifungu hiki hapa chini cha hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi na ni dhahiri kwamba kwa muono wa serikali yake madaktari ambaorofession yao huchukuwa miaka mingi na gharama kubwa si chochotew au lolote, ni kama wafanyakazi wengine wa serikali kama wahudumu wa ofisi, makarani wa masijala etc.

Yaani madaktari wataongezwa mishahara kama kwa viwango (percentage kama hao wengine tu, pamoja na umuhimu wa taaluma zao!

Watu uhimu bila shaka ni kama vile Wabunge ambao huongezwa mishahara iwapo watakohoa tu.





........Ndugu Wananchi;

Jambo la pili ambalo muafaka haukufikiwa baina ya Serikali na madaktari ni kuhusu mshahara wa kuanzia kazi wa daktari. Madaktari wanataka uwe shilingi 3,500,000/= wakati Serikali inasema kiasi hicho hatukiwezi. Serikali imeeleza utayari wake wa kuongeza mshahara kwa kati ya asilimia 15 mpaka 20 kama ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha. Kwa kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya shilingi 1,100,000/= na 1,200,000/= kutegemea kiwango kipi hatimaye kitaamuliwa. Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania shilingi 3,500,000/=............
 
Hakuna mwanasiasa atakaye kwambia ukweli madaktari wanataka nini hasa.Kwa nini wanashikia bango hapo tu?
Kila mara nauliza report ya Mama Sitta inakitu gani kwa nini viongozi wetu wanaiogopa kuiweka hadharani?
Kwa nini waendelee kuudanganya umma?Watuambie ile Kamati iliongea nini na kada zote za afya.Watupe ukweli ili tuchanganue pumba na mchele.
Wabunge watuwekee kwanye mtandao tuione tuijadili tuwape majibu basi ilikila mtu awe na furaha basi.Au mnasemaje WanaJF?
 
Rais lazima awe na akili timamu. Hapa hakuna kiongozi. B...sht!
Na wasaidizi na washauri wake wote ni B...sht.
itasikitisha sana
Mwaka 2015 ni mbali sana.
 

Haya ndiyo madai ya madaktari na kusababisha mgomo, kuna tofauti gani na malalamiko ya wananchi dhidi ya madai ya wabunge kuongezewa posho kiwango ambacho kinatofautiana mno na watumishi wangine wa umma? Kuwa na kiwango cha juu zaidi kutokana na taaluma yao sishangai, lakini kwa madai haya ni juu mno ukilinganisha na uwezo wa serikali.
 
Sioni cha ajabu kwa rais wetu, kimsingi niseme sikutarajia jipya hata hivyo kajitahidi. Unakumbuka aliyoyasema enzi zile za kuasisi dhana ya kujivua gamba? Alisema wanaotuhumiwa wajipime na wachukue uamuzi. Rais anapokosa maamuzi ujue kuna mazito aliyoyapima na kuona hayawezi, JJ Mnyika alikuwa na hoja.
 

Mkuu hiyo Hotuba aliitolea wapi? Kwani "Michuzi Blog" ndo Kurugenzi yake ya Mawasiliano kwa wananchi siku hizi?



 
.............. Na mbio zetu tokea uhuru. KWELI HOSP ZETU ZA MKOA ZINAKOSA HATA X-RAY? WHY MKUU UJASEMA? NA WHY hotuba yako .. acha nisiseme!.
 
Kama mwananchi, ninachanganyikiwa. Sijui nani yuko sahihi, nani napotosha. Nasubiri tu kuona hii commedy kati ya serikali na madaktari itafikia wapi. Kitu kimoja nilicho na hakika nacho, wakati wao wanaendelea kulumbana, wananchi wasio na hatia wanaendelea kuteseka.
 
Ni taifa la aina gani mtalijenga kama wote tukikimbilia siasa? Chukulia wewe ndo msemaji wa serikali. Je kwa kauli hiyo tutafika?
 
Wewe nawe!!! nyie ndo tunasema wabinafsi sana tena sana, yaani unataka waongezewe mshahara madaktari tu, watumishi wauma wengine wasiongezewe??? fikiri kwanza ndugu.

kila taaluma inaumuhimu wake ndugu hata manesi pale muhimbili wanaumuhimu wao pia, hata makondakta wa daladala wanaumuhimu wao pia ambao wakigoma leo tutaadhirika tu, kinachotofautisha ni kiwango cha adhari.

tatizo la wabongo ni ubinafsi umetujaa tuuu, hatuna uzalendo na upendo, mtu amekaa nyumbani anataka aongezewe mshahara ile hali mwenzie anakufa?? what is this? ndo miiko ya udaktari au ...??

ndo mana wengine waliposoma PCB na nakupata divi 1 form 6 walitafakari kuona mazingira magumu hivyo wakaenda ualimu, uasibu au uanasheria, wakawapa nafasi wengine waliopata div 2 au 3 ili kuondoa usumbufu kama huo. sasa leo iweje ulieenda ulete bughudha kwa wengine?. Serikali lazima iwe na msimamo asiyeweza fanya kazi selikarini atoke halazimishwi??
 
Kweli huyu ni mheshimiwa dhaifu, Hotuba ya mwezi mzima suala ni moja tu, wakati yako mengi katika nchi yanahitaji kauli ya kiongozi wa nchi, kalikoroga la madaktari hana jinsi, Waziri wa afya, Waziri Mkuu na mwisho Rais mwenyewe hakuna alie na busara kutatua tatizo la madaktari.
 
Kikwete ahsante sana.

Sasa ondokeni mkafanye kazi zenu za private au mrudi kazini, uamuzi ni wenu, na huko mahospitali tutaanza kuwawekea tathmini ya kujuwa ni nani anaefanya kazi na anastahili kulipwa na nani asiyefanya. Mnalo?
Wewe ufanye tathmin, Akili za Makalio bwana
 
Mbona kuna watu wanalalamika kuwa walimsubiri dhaifu ili waweze kuisikiliza hotuba lakini hawaikuwa hivyo...

Hata mimi nimekaa sebuleni hadi saa tano usiku sikuona hotuba ya huyo anayejulikana kwa jina maarufu DHAIFU .Lakini hata hivyo hotuba yake kama michuzi alivyoiposti haina afya kabisa ina mapungufu mengi hajajibu hoja za madaktari na hoja ya wananchi kupitia hoja ya madaktari juu ya uboreshaji wa huduma za afya .

Asikimbile kukokotoa kutoa jumla ya fedha wananazoweza kulipwa madaktari kwa mwezi ili wananchi wawachukie madaktari, kikwete hoja hiyo ni dhaifu kama sifa yako ya udhaifu ,hapa unatafuta huruma ya wananchi waone wewe unawajali wakati sio kweli , wakati wananchi hao anawaua wewe na serikali yako ambayo haiko tayari kuboresha huduma za afya na akununua vitendea kazi ,unasema serikali haina fedha mbona kwenye mikutano ya ccm wanasomba watu kwa malori ilikushiriki mikutano yao isio na mvuto,mbona wanahonga watu kwenye chaguzi ili washinde ,kama kweli serikali haina fedha mbona amelundikiwa safari nyingi za nje ambazo hazina tija kwa watanzania ,mbona fedha za katiba billion arobaini amepeleka huko kunanini cha ajabu ambacho kinahitaji kamati ya tume hiyo inalipwa fedha nyingi sana kiasi hicho , wao ninani kuliko hata ushindwe kupembua kujua umuhimu wa madkatari na afya za wananchi,unashindwa nini kuwapa stahiki zao madaktari ,kikwete utahukumiwa baba wewe unawatesa watanzania ulikimbilia ikulu kufanya nini,fedha hizo za kuwalipa madaktari zipo ila hataki kuwalipa unawalinda wezi wa fedha za umma mafisadi .kama mnadhimu wa jeshi shimbo ameficha fedha trillion tatu nchini afrika kusini umeshindwa nini kuamuru fedha hizo zirejeshwe hapa nchini ili ziboresha hospitali zetu kwa kununua machine za kisasa pamoja na madai mbali mbali ya madkatari zingetosha .je hizo ni chache za shimbo mnadhimu mkuu wa jeshi.

Kikwete wewe ni dhaifu hata ikulu umejenga uswahiba sana ,subiri maswaiba wako watataka uwapikie chai sasa.

kwenye bajeti mwaka uliopita zilitengwa fedha billion saba kwa ajili ya watu watakaopelekwa nje kutibiwa na tunajua watu waliotengewa fedha hizo ni vigogo sio walalahoi na ndiyo maana hamjali kuboresha hospitali hapa nchini kwa sababu nini matibiwa huko kwenye hospitali zenye vifaa vya kisasa.

Katika afya tunatambu kuwa ili mtu aweze kutibiwa na kupano nilazima vipimo sahahi vipatikane ,sasa kama wewe unalundika tu vitanda na madaktari bila vitendea kazi unataraijia huduma atakayopewa mawananchi itamsaidia kupona kama vitendea kazi vitakosekana.kikwete acha hizo .usidhani kwamba sisis watanania niwajinga kiasi hicho .tekeleza madai ya madakari na kuboresha hospitali na vituo vya afya.

Hizo billion saba je zimetumika kamazilivyokusudiwa ama mmehamishia kwenye akaunti zenu mkafaidi na watoto wenu.lakini ipo siku kikwete na jamaa zako mtaotoa hesabu ya udhalimu mnao wafanyia watanzania na ulimboka .

Tunajua uliagiza wamfanyie hivyo ulimboka na kikosi cha watu wako kile cha kijito nyama kikosi cha maangamizi tunataarifa zote na ndiko alikopelekwa kabla hajafikishwe kwenye msitu wa pande .kikosi hicho tunajua hatakodi namba zake leo hii ambayo ni 101. ikulu ikanushe kama sio kweli.tutweka hadharani kila kitu .
 
Nawaonea huruma watanzania waliomchagua mtu huyu ambaye sasa anawatesa kiasi chakusababisha baadhi ya wapiga kura wake kufa. Ila nasisi wengine tutafanya nini kama hali itaendelea hivi? Hospital hamna huduma? Naona tuige kilichofanyika uarabuni.
 

Kikwete ni mwanadiplomasia, wanaoelewa lugha iliyotumika ambayo ni diplomatic language anaelewa kwamba rais katoa tamko rasmi la kuwafukuza madaktari waliogoma na kufukuzwa kwenye nyumba za serikali wanazoishi ndani ya saa 24. Kazi hiyo imezanza kwenye hospitali zinazomilikiwa na mashirika ya dini Bugando Mwanza na KCMC Moshi.

Kwa mtazamo wangu serikali haiwezi kuacha mambo yaendelee kama yalivyo, ni lazima uamuzi ufanyike ili kieleweke tuna madaktari au la. Tuwajue madaktari waliopo kazini wanajituma na nani hawako pale kikazi ila kimasilahi.

Uwezo wa serikali umeishia hapo, asiyeweza na afungue virago aende huko anaokoona atapata mafao anayetegemea. Kulipwa milioni 7 kwa mwezi kwa hali ya serikali sasa hapana.
 
Nawaonea huruma watanzania waliomchagua mtu huyu ambaye sasa anawatesa kiasi chakusababisha baadhi ya wapiga kura wake kufa. Ila nasisi wengine tutafanya nini kama hali itaendelea hivi? Hospital hamna huduma? Naona tuige kilichofanyika uarabuni.

Nampongeza kikwete amefanya uamuzi mgumu tuliotazamia, tunataka watu wenye kujali uhai wa binadamu kuliko wanaotanguliza masilahi yao kwa kuwekea rahani uhai wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…