Hotuba ya Lowassa yavuja

paperwork

Member
Joined
Sep 25, 2015
Posts
22
Reaction score
26
Wandugu, nimepata kipande kikubwa cha hotuba ya Lowassa ya kufungia Kampeni, kuna mambo mapya meengi saana atayaongea, ambayo nina uhakika yatamuongezeau kura nyiiingi saaana zilizokua zimebaki CCM.

Kwa ufupi kati ya hayo mambo ni yafuatayo;

1. Kulipa madeni yote ya ndani, kuanzia kwa watu binafsi, makampuni ya ndani na watumishi wa umma, wanoidai serikali, wakiwemo na wafanyakazi wa iliyokua jumuiya ya Africa Mashariki, (wale wazee), pia kuna watu wanaidai serikali kutokana na kuishinda serikali kwenye kesi mahakamani lakini hawajalipwa na serikali haina mpango wa kuwalipa.

Hatua hiyo, licha ya kwamba itamuongezea kura, itasaidia saana kunyanyua uchumi wa watanzania wengi.

2. Lowassa, anaahidi kuwalipa fidia (kuwarudishia fedha zao) wale wote walioathirika na upatu wa DECI, walipanda lakini hawakuvuna. Ikumbukwe kwamba fedha zao zilikamatwa na serikali ikazichukua, viongozi wao wakafungwa lakini serikali haijawarudishia fedha waathirika na wala haijasema imeweka wapi zile fedha ambazo zinakadiriwa kuwa zaidi ya Billioni 29.

3. Pia anawapa moyo na kuwaahidi watumishi wa umma, kwamba ajira zao katika utumishi wa Umma zitaendelea kuwa vile vile, mathalani kwa mfano wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu, wakurugenzi wa halimashauri, wakurugenzi wa idara mbali mbali. Vyeo vyao vitaendelea kuwa kama kawaida, kama kubadirishwa itakua ni sababu yabutendaji na sio uhusiano wao na vyama.

Na mengine mengi subirini wenyewe kuisikiliza hotuba.

Nahisi hotuba ya hitimisho itamuongezea kura nyiingi saana Lowassa.


=====================================

 
sasa we aliyekutuma kuivujisha zaidi ninnani? si ukaekimya tu usubiri itoke nzimanzima? kiherehere chanini? We ndio wale wanona mtu kachuchumaa wanaanza tanganza kuwa kanya!
 
Hakika kaifanya hayo atakuwa amefanya jambo jema. Biashara za watu zimekufa kisa serikali haijalipa pesa, wengine ilikuwa mikopo ambayo imewagharimu nyumba na mali kuuzwa.

Mungu akupe kibali Laigwanani Lowassa uwe rais wa nchi..
 
kumbe DECI ni ilikuwa ya Lowasa? hii hatari sana.
 



Kuna mengi hapo Magufuli hajawai hata kuyawaza kuyaongea.

Zaidi ya kuongelea barabara na kilugha hakuna analolijua zaidi. Labda kupiga mikwara.

Na aimani Magufuli ataiba mawazo ya Lowasa.
 

Sidhani kama ataweza kuisoma kwa urefu huu labda atuwekee kwenye website ya chama tuipitie kabisa
 
Ng'ombe hanenepi siku ya mnada mkuu ikiwa ni sikio la kufa siku zote huwa halisikii dawa na mamvi ni sikio la kufa tu.
 
Kwanin mkuu dozi itaishia njiani nin
 
Utakaa sana kuwaona hivyo jichungulie wewe kwanza ndpo iwaone wao
 

Hakuna hata moja litakalomuongezea kura....cheap cheap politics...watanzania wanaweza ku-digest ahadi....
 
hotuba imevuja au imevujishwa? na babu seya vp atamtoa lini... hapo pia kuna pointi au vipi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…