Hotuba ya kwanza ya Yesu

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
Kabla ya kutoa hiyo Khutba juu ya ufalme,Yesu alisoma maneno haya katika Maandiko,

''Mtakuwa kwangu falme ya mapadri,watu watakatifu. Yahweh ni mwamuzi wetu,Yahweh ndiye anayetupa sheria. Yahweh ni mfalme wetu;atatuokoa. Yahweh mfalme wangu na Mungu wangu. Ni mfalme mkubwa juu ya dunia yote. Upendo upo juu ya Israel katika huu ufalme. Ubarikiwe utukufu wa Bwana kwa vile yeye ni mfalme wetu.''
Alipomaliza kusoma hivyo,Yesu akasema,
'' Nimekuja kutangaza kuanzisha kwa ufalme wa Baba.Na ufalme huu utajumuisha roho zote zinazoabudu,za Myahudi na yule ambaye siyo Myahudi,tajiri na maskini,aliye huru na mtumwa,kwa vile Baba yangu habagui watu;upendo wake na huruma yake ni juu ya watu wote
''Baba yangu mbinguni anaipeleka roho yake kukaa ndani ya akili za watu,na nitakapomaliza kufanya kazi yangu duniani,hivyo hivyo,Roho wa Kweli atamwagwa kwa miili yote. Na roho ya Baba yangu na Roho ya Kweli vitakuweka wewe katika ufalme unaokuja katika ufahamu wa kiroho na haki ya kitakatifu. Ufalme wangu siyo wa dunia hii. Mwana wa Mtu hataongoza majeshi ili kujiweka kwenye kiti cha enzi au kutafuta ufalme wenye utukufu wa kidunia. Ufalme wangu utakapofika,mtamwelewa Mwana wa Mtu kama Mwanamfalme wa Amani. Watoto wa dunia wanapigana ili kuanzisha na kupanua falme za dunia hii,lakini wafuasi wangu wataingia ufalme wa mbinguni kwa maamuzi yao ya kimaadili,na kwa ushindi wao wa kiroho,na wakishaingia ndani,watapata furaha,haki na uzima wa milele.
''Wale ambao kwanza wanataka kuingia katika ufalme,yaani ,wanaotaka kuanza kuwania kuwa na nafsi iliyotukuka kama ya Baba yangu,hatimaye,watapata mengine yote wanayohitaji. Lakini nawaambia kwa moyo mkunjufu;Utafute kuingia kwa imani,imani tegemezi kama mtoto mdogo,ama sivyo hautaruhusiwa kuingia.
''Usidanganywe na hao wanaosema ufalme uko hapa au uko pale,kwa vile ufalme wa Baba yangu hautegemei vitu vinavyoweza kuonekana au vinavyoweza kuguswa. Na huu ufalme upo miongoni mwenu hata sasa,kwa sababu pale ambapo roho ya Mungu inamfundisha na kuiongoza roho ya mtu,hapo kweli ndio ufalme wa Mungu.Na huu ufalme wa Mungu ni haki,amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
''Yohana kweli aliwabatiza ili mtubu dhambi zenu,lakini utakapoingia katika ufalme wa Mungu,utabatizwa na Roho Mtakatifu.
''Katika ufalme wa Baba yangu hakuna Myahudi au yule ambaye siyo Myahudi,isipokuwa tu wale ambao wanatafuta ukamilifu kwa kutumikia,kwa sababu nasema yule anayetaka kuwa mkubwa katika ufalme wa Baba yangu lazima kwanza awe mtumishi wa wote. Kama uko tayari kuwatumikia wenzako,utakaa pamoja nami katika ufalme,kama vile ambavyo mimi nitakapotumikia kwa mfano wa kiumbe,baadaye nitakaa na Baba yangu katika ufalme wake.
''Huu ufalme wangu ni kama mbegu inayoota katika udongo mzuri katika kiwanja. Haizai matunda kamili upesi. Kuna muda unapita,tokea kuanzisha ufalme katika roho ya mtu na saa ile ambayo ufalme unakuwa matunda ya haki ya milele na wokovu wa milele.
''Na huu ufalme ninaowaeleza siyo utawala wa uweza na fanaka. Ufalme wa Mungu siyo swala la kula nyama na kunywa,ila ni swala la kuendelea katika haki na kuongezeka kwa furaha katika kukamilisha utumishi unaofanya kwa Baba yangu mbinguni,kwa vile si Baba amesema kuhusu watoto wake wa dunia hii,'nataka hatimaye wawe wakamilifu kama ambavyi mimi ni mkamilifu.'
''Nimekuja kufundisha habari nzuri za ufalme,sikuja kuongeza katika mzigo mzito wa wale ambao wanataka kuingia katika ufalme huu. Natangaza njia mpya na nzuri zaidi,na wale watakaoweza kuingia katika ufalme watapata kupumzika. Na chochote itakachokugharimu katika vitu vya dunia,gharama yoyote ile utakayolipa ili uingie katika ufalme wa mbinguni,utalipwa maradufu furaha na maendeleo ya kiroho,na wakati ujao,uzima wa milele.
'' Kuingia katika ufalme ;hakusubiri majeshi kusonga mbele,au kupinduliwa kwa falme za dunia hii,au kukatwa kwa minyororo ya mateka,ufalme wa mbinguni upo hapa sasa hivi,na wote watakaoingia watapata uhuru mkubwa na furaha ya wokovu.
'' Ufalme ni utawala wa milele. Wale watakaoingia katika ufalme watakwenda juu kwa Baba yangu;bila shaka watafika katika mkono wa kuume wa utukufu wake Paradiso. Na wote watakaoingia ufalme wa mbinguni watakuwa watoto wa Mungu,na katika wakati ujao watakwenda juu kwa Baba yangu. Na sikuja kuwaita watu ambao wana hamu ya kuokoka,ila watenda dhambi,na wote ambao wana njaa na kiu ya kukamilika kiroho.
''Yohana alikuja kuwafundisha toba kuwatayarisha kwa ufalme,sasa nakuja kutangaza imani,zawadi ya Mungu,kama ndio gharama ya kulipwa ili kuingia katika ufalme wa Mungu. Kama tu ukiweza kuamini kwa upendo usiokuwa na kifani,basi upo ndani ya ufalme wa Mungu.
''Baada ya kuzungumza hivyo,Yesu akaketi.Wote waliomsikia walishangazwa na maneno yake.Wafuasi wake wakashangaa.Lakini watu wote hawakuwa tayari kupokea habari njema kutoka katika midomo ya huyu Mungu-mtu. Takriban theluthi moja ya waliomsikia waliamini,ingawa hawakuelewa vizuri,theluthi moja wakajitayarisha kupinga ufalme wa Mungu unaozungumzia roho tu,na theluthi moja iliyobaki haikuyaelewa mafundisho yake,ikaamini kwamba huyu ni mwehu.''


[Natoa uhuru kwa wote kuandika haya mambo in whole au in part ,with or without aknowledging that it came from me.]
 
Back
Top Bottom