Hotuba ya kutisha!!!!!!!!

hapo kwenye kusitisha matumizi ya misahafu ni muhimu zaidi
 

we unaleta ya kibwetele, tuache yatokee ya kibwetele, ndoto yako inakaukweli kiasi fulani.................................
 
ahahahaha nimeipenda kweli,
wewe ni g.thinker ndo mana ndoto zako zipo great.
 
Afadhali ulishituliwa na konda ole wako ungeendelea kuota halafu ukapata hasira na kuanza kuvunja vunja radio kumbe una mnyuka jirani yako makonde hapo ingekuwa balaaa
 
hahah, ni creativity ya hali ya juu sana. hongera mkuu
 
mkuu kwenye daladala unalala mpaka unaota bila shaka ni gmboto - tegeta
 
Afadhali ulishituliwa na konda ole wako ungeendelea kuota halafu ukapata hasira na kuanza kuvunja vunja radio kumbe una mnyuka jirani yako makonde hapo ingekuwa balaaa
Ahahahahaaaah!!!
 
Pole kwa uchovu mkuu...mpaka kupata usingizi mnono kiasi cha kuota!! uliupiga haswa hata Ngele..utakuwa ulimzidi kwa kuuchapa kwenye "kadamnasi" tena mbele ya umati wa watu

 
we! Siku hizi watu wakisinzia hadharani ni mwiko kukiri ulisinzia. Sema ulikuwa unasali au unakemea mapepo.
 
Unajua sijawahi kuchangia sehemu hii ya udaku na mara nyingi huwa sivijari humu kabisa. Niliingia hapa kutokana na curiosity ya hii headline sasa wakati naanza kusoma maneno haya...
Nikiwa ndani ya daladala asubuhi hii, karibu nusu ya abiria walikuwa wanajadiri kitendo cha Serikali kuingilia kati matibabu ya Babu Loliondo
... sikuwa makini sana (yaani sikuwa attentive na ninacho kisoma), nikaendelea kusoma mpaka nikafika hapa...

ghafla nikasikia redioni mtu anahutubia Taifa sauti kama JK hivi.

... hapo pia sikuwa na shaka (nikasema inawezeka ni kweli) kwasababu nipo mbali na nyumbani kwahiyo yanayozungumzwa redioni siyafahamu, mambo ya bongo nayapatia hapa JF.

Nilipofika hapo...

"Serikali yenu mliyo ichagua itahakikisha haiingilii imani za watu maana serikali yenu haina dini

... pia sikuona tatizo kwasababu nilishasoma hapa jamvini kuwa wamesitisha huduma ya babu, nikaendela mpaka hapa...

  1. Kusitisha kwa mda matibabu ya Babu Loliondo mpaka ijiridhishe na ubora wake.
kufika namba mbili...

2. Kusitisha kwa mda ubatizaji makanisani kwa kutumia maji

Nikasituka! (kumbuka sikujua nipo jukwaa gani), ghafla nikaanza kutia shaka na ninacho kisoma kwasababu mara nyingi wakati na soma kitu hupenda kusoma huku nikiangalia lengo la mwandishi. Kwahiyo nikaacha kusoma kabisa na kuangalia juu kwenye browser bar kutaka kujua kama ninacho kisoma ni kweli au ni mauzauza tu.

Ndipo niakaona https://www.jamiiforums.com/jokes-utani-udaku-gossips/116935-hotuba-ya-kutisha-2.html. Nilicheka sana huku nikamalizia kusoma.

Mkuu ubarikiwe kwa kutupatia kisheko hiki kweli kuna watu mmejaaliwa ku-hit home katika ujumbe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…