Hotuba Ya JK Dodoma: Tafsiri Yangu

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu Zangu,

JANA Jumamosi nimemsikiliza Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete. Mwenyekiti Kikwete alikuwa akihutubia kule Dodoma katika kuadhimisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa Chama chake Cha Mapinduzi.
Ukweli kwamba CCM ndio chama tawala ndio wenye kutufanya tufuatilie kwa karibu yanayotokea ndani ya chama hicho.

Nimeisikiliza na nimeisoma hotuba ya Kikwete. Tafsiri yangu;
Kikwete anasema; ” Chama cha Mapinduzi kiige tabia ya nyoka ya kila baada ya muda fulani hujivua gamba lake na kupata jipya. Hatuna budi kufanya hivyo na kufanya hivyo sasa” . Anasema Kikwete.

Naam. CCM ya Jakaya Kikwete ni nyoka anayejibua. Kwa nyoka kujibua kuna maana ya mabadiliko. Nyoka kutoa gamba lake ni mabadiliko makubwa katika mwili wake.
Kwa kumsikiliza na kumwangalia Kikwete sina hofu juu ya dhamira yake ya moyoni . Kikwete anaonyesha kukiona kile ambacho wengi ndani ya chama chake, ama wamekiona lakini hawataki kukiona au hawajakiona. Kikwete ameshauona upepo wa mabadiliko unavyovuma.


Kuna wimbi la mabadiliko linaendelea barani Afrika. Vijana ndio wenye kuongoza harakati hizo za mabadiliko. Watanzania hatuna sababu ya kupoteza muda kujadili na kujiuliza kama tunahitaji mabadiliko au la? Ukweli ni huu, wimbi la MABADILIKO linakuja. Tunachokiona sasa ni upepo unaovuma kabla wimbi lenyewe kutua.


Siamini kama ya Tunisia na Misri yanaweza kutokea Tanzania. Kuna tofauti kubwa. WaTunisia Na WaMisri wamechoshwa na Usultani. Mtu mmoja na familia yake kuongoza maisha. Wakati Hosni Mubarak ametawala kwa miaka 30, ndani ya miaka 30 hiyo Watanzania tumekuwa na marais watatu. Yetu ni matatizo mengine. Tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano. Tunachohitaji ni Marekebisho makubwa ya Katiba yetu ili tuwe na chaguzi huru na za haki.


Ni jambo jema kwa CCM na Watanzania, kuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi haitwi Benjamin Mkapa. Kikwete ni plagmatic , si dogmatic na teknokrati kama mwenzake aliyemtangulia. CCM inamhitaji kiongozi wa mfano wa Kikwete kulikabili wimbi la mabadiliko linalokuja.


Nilishapata kuandika miaka mine iliyopita, kuwa Jakaya Kikwete, kama Rais na
Mwenyekiti wa chama tawala, hana jinsi, bali ana lazima ya kufanya mabadiliko makubwa katika
safu za uongozi ndani ya chama chake na serikalini. Jambo hilo lilipatwa kufanywa na
Mwalimu Nyerere miaka kumi baada ya Azimio la Arusha.

Ikumbukwe, juma moja baada ya kuzaliwa kwa CCM tarehe 5 ya mwezi wa pili,
mwaka 1977, Mwalimu Nyerere alifanya mabadiliko makubwa ya uongozi wa Chama
na Serikali. Yale ya mwaka 1977 yanabaki kuwa ni mabadiliko makubwa ya kihistoria
kuwahi kufanywa na kiongozi wa Tanzania tangu tupate uhuru.

Yalikuwa ni mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri yaliyogusa karibu wizara zote. Ni
mabadiliko yale yaliyopelekea Bw. Pius Msekwa kufanywa kuwa Katibu Mkuu Mtendaji
wa Kwanza wa CCM.


Kikwete na CCM wana mtihani mkubwa kama wataka kubaki katika uongozi ifikapo mwaka 2015. Swali moja gumu wanalotakiwa kulijibu ni hili: Ni kwa namna gani watalifikia kundi kubwa la vijana ambao sio tu wanaonyesha kuchoshwa na chama hicho, bali hata baadhi ya viongozi ndani ya CCM hawaonekani kwenda na wakati.
Dunia Imebadilika. Nahitimisha.
Maggid
Iringa
Februari 6, 2011
mjengwa
 
Maggid,

..u missed the point.

..CCM muda wote imekuwa ikijivua gamba kama ilivyo kwa nyoka.

..hebu angalia mtiririko huu: Sukita,kutorosha dhahabu,Loliondo,Rio De Jeneiro,IPTL,ubinafsishaji holela,mikataba holela ya madini,wizi na uuzwaji wa nyumba za serikali,EPA,Richmond,Buzwagi,Dowans, kuchakachua uchaguzi, etc etc.

..CCM has been re-inventing itself. tatizo imekuwa inaji-reinvent katika masuala ya hujuma dhidi ya wananchi wa Tanzania.
 
Maggid,
You have missed the point!
JK has at last realised that those around him in the party are of no help in the long run.
Chama kimefedheheka sana katika uchaguzi uliopita, na si kwa sababu ya upinzani, bali kwa makundi iliyojitengenezea yenyewe.
Makundi haya ni ya kutoka 2005,na hayajasuluhishwa wala kukalishwa pamoja.Njia moja ya kuondoa makundi haya ni kuwaondoa vinara wake kwa kuwapa nafasi za ubalozi nje ya nchi, kama alivokuwa akifanya Mwalimu.
Pili,sababu nyingine ni chama kuanza kupoteza au kufifia mshikamano wake na wanachama wake.Chama sasa kimejaa wafadhili , wafanyabiashara wakubwa.Mwalimu hakuwa mjinga kuwaweka kina Songambele na Bibi Titi mstari wa mbele katika siasa, hawa walikuwa macho na masikio ya wanyonge.
Tatu msimao wa chama katika kashfa tofauti,EPA,Kagoda Benki Kuu Richmond na Dowans etc si wa kutia moyo.
Kuyaachia mambo haya yanayo mgusa mwananchi moja kwa moja, serikali kuyashughulikia bila msimamo mkali wa chama unatia mashaka kwa chama.Ni kweli chama hakiingilii uhuru wa mahakama, lakini karipio tu la nguvu limatosha kuifanya serikali na taasisi zake ishtuke kutoka usingizini.
Kwa siku za karibuni tofauti ya chama na dola imekuwa ndogo na watu wanashindwa kutofautisha.
JK ana kazi nzito ya kuwainua vijana wasomi kushika na kukiendeleza chama kwa ajili ya changamoto zijazo, kwa hili nampongeza kuwa ingalau ameliona.
 
Umetoa tafsiri nyepesi kwa swali gumu; nianze tu kwa kusema kwamba kwa maoni yangu, hotuba ya JK ya jana ilikuwa ni siasa tu, na wala haikuwa na maudhui yeyote. Chukua madhalani ili suala ulilozungumzia la kufufua uhai wa chama, kwa mtu yeyote ambaye amekuwa anafuatilia siasa za nchi hii, anafahamu fika ya kwamba, CCM imepoteza mvuto wake, siyo tu kutokana na utendaji mbovu, lakini hasa kwa kukumbatia matajiri na kuwatelekeza wananchi wa kawaida. Katika hali hiyo kubadilisha tu safu ya watendaji haiwezi kusaidia lolote.
 
Back
Top Bottom