Hotuba ya Disemba Mosi; UKIMWI na kupiga "fasihii matumizi ya simu za mkononi"

displayname

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,950
1,039
Ndugu WanaJamvi,

Hotuba hii nilipatatoa miaka kadhaa nyuma siku kama ya leo tulipokuwa na desturi ya kufanya maadhimisho haya kwenye majukwaa kabla ya kuadhimisha kivingine kwa kauli mbiu ya Hapa ni Kazi ya Ndugu John.


Hiki ni kisa cha kweli hebu soma utoe maoni yako.

Mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya mawasiliano alikaribishwa kutoa speech leo December mosi mwaka huu katika kuazimisha kilele cha siku ya UKIMWI Duniani, speech iliwalenga vijana kuhusu kujiepusha na vitendo vyenye kuweza kusababisha maradhi ya kisasa.



Speech ya Mkurugenzi huyu ilinukuliwa kama ifuatavyo; "Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa. Mtandao wa ugonjwa huu ni mkubwa, mimi nashauri muwe makini. Jitahidini sana kukaa bila KUPIGA.

Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na wala si KUPIGA PIGA kwani hii gharama yake ni kubwa. Kama shida ya KUPIGA itakuwa kubwa, basi hakikisha simu yako iko kwenye KIPOCHI, na hivi vinapatikana kwa wingi na gharama yake si kubwa. Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata madhara yanayoweza kupatikana kutokana na mionzi iliyoko katika SIMU hizi za kisasa. Ni mwiko kabisa kupiga "Voda kwa Voda" kwani hii ina hatari kubwa mno.

Mbaya zaidi ni kupiga TIGO, kwani hatari na madhara yake ni makubwa sana kwa wote WAPIGAJI na WAPIGIWAJI/WAPIGWAJI. Aidha natambua ya kwamba Watu wengi SIMU zenu zina fanya kazi vizuri tu na mna hamu angalau ya ku beep, lakini hii nayo ni hatari,kwani mwenzako akionyesha utashi wa kupokea ni rahisi sana kwako kuamua KUPIGA kabisa.

Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti SIMU zenu zitamaliza chaji, hii si kweli. Hakikisha tu kwamba simcard iko katika hali nzuri, hii ndio ina kumbukumbu zote na ndio inaongoza mawasiliano yote.

SIMU ni SIMU tu, na madhumuni yake yanafanana. Usidanganyike na SIMU kuwa eti kubwa kama mche wa sabuni au ndogo kama kiberiti au ina Kamera, four button sijui double skrini...na miaka ijayo zitagundulika SIMU zisizo na vitufe yaani touch screen, utakuwa ni ulimwengu wa smart, lakini hizo zote ni mbwembwe tu. Kuna SIMU nyingi sana feki siku hizi zinauzwa zimevishwa cover mpya, usidanganyike ndugu.

Ukiona maisha bila KUPIGA hayawezekani, tafuta sehemu inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia sana kwani SIMU ukitumia peke yako inadumu zaidi kuliko ile yenye subscribers wengi."

Mwisho kabisa niwatakieni mawasiliano mema, zitumie kwa umakini sana SIMU zenu KUPIGA. KUPIGA ni kuzuri sana ila sio KUPIGA PIGA tu hata kama huna cha maana cha kuzungumza kwani hugharimu afya, uchumi na nguvu ya kuzalisha mali wakati wa kuzungumza unapopiga SIMU, na ukimaliza KUPIGA wajikuta umechoka.

Ahsanteni kwa Kunisikiliza!

1.12.2011

DISPLAY NAME
Mgeni Mwalikwa
Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani,
 
ilikuwa poa sana ningeomba pia hipostiwe hata kwenye social media zingene kama fb,whatsapp group ili watu wajifunze kitu
 
Hii imekaa muruwa kabisa inafaa kwa rika zote, hata kama umekaa na mkwe unaweza kuisikiliza bila wasiwasi na hata mkajadiliana naye:spy:
 
Hii imekaa muruwa kabisa inafaa kwa rika zote, hata kama umekaa na mkwe unaweza kuisikiliza bila wasiwasi na hata mkajadiliana naye:spy:

Ndio matumizi sahihi ya fasihi hasa fasihi simulizi...japo mafumbo huwenda yakashindwa eleweka kiurahisi kwa baadhi ya watu/hazira.
 
lkn mbn ametaja mtandao wa tigo na voda tu, kwa iyo airtel ndo hauna madhara??? au yeye ni mkurugenzi wa airtel?

Haha nafikiri airtel enzi hizo haikuwepo kama sikosei ilikuwa celtel kama sio zain...sina hakika ka,a hauna madhara ila ni kutakana na maneno ya msimu mitaani wajua voda kwa voda wanaamanisha nini pia na tigo wanaashiria nini pia!!
 
Back
Top Bottom