Hotuba ya chadema ya kila mwezi

mkuu ukitaka kumkosoa mtu inabidi umQuote ili ubaki ushaidi. Mfano,apo jamaa kashakosoa ila sasa wewe ndo unaonekana umekosea. Kwa upande mwingine nashukuru wazo lake ila chama chenye magamba hawana hotuba ya kila mwezi,huwa wanakuwa nayo wanapojisikia,si unajua nchi yao hii. Kwa iyo cdm wakija na ujumbe wa kila mwezi watafanikiwa sana,tatizo ni media ipi itakubali itumike? Hapa mtihani utakuwa na majibu ambayo pia ni mtihani.

Tupo pamoja! binafsi huwa sioni zuri la kuiga kutoka kwenye chama cha magamba....wananchi wanataka action na majibu kwenye kero zao! Fikiria mzee wa Msoga kule Bagamoyo ameishatoa hotuba ngapi na kipi kimefanyika? CDM wasiinge kila kitu kwa wenye Magamba
 
Ndiyo wazo zuri. Kila mwisho wa mwezi kuwe na kipindi maalumu cha matukio ya shughuli za chama katika halmashauri mbalimbali ambazo zinaongozwa na CDM halafu baada ya kipindi hicho hotuba ya CDM itolewe kwa umma wa Watanzania kutoa uchambuzi wa hali ya nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii. Ni kweli nakubaliana na watu wengine CDM has not been very aggressive in application of electronic media, we need to do that now, idara ya uhamasishaji ndio kazi yao. aluta continua, use every opprtunity, and every opportunity is a resource to cdm, remember that it is the party's creativity that will add value to the change struggle. Mtu mmoja moja anaibua wazo, watu wengi wanatumia wazo hilo kuleta mabadiliko. Zao la juhudi zetu ni mabadiliko ya kutusogeza karibu na ustawi wa taifa letu. Nothing short of that will keep us united, tuongozeni kufika huko.
 
wazo zuri linaigwa hata kutoka kwa shetani, haijalishi unatoa wapi, hata wao wameiga Marekani, la muhimu hilo jambo uliloiga unalitumia likupe matunda gani.
 
Mnafikiri nani atarusha hotuba yao TBC? watakubali ili wachakachuliwe?

Wala msiumize vichwa wakuu ni hivi: Kwanza CDM wawasiliane na vyombo vya habari TBC, ITV, Radio one, STAR TV na Channel, & other radios watakazoona zinafaa ili wapate jibu (yes au no). Na ningeshauri wafanye haya mawasiliano kwa maandishi ili kuweka kumbukumbu (evidence). Kwa vyombo vitakavyosema NO basi wawajulishe wananchi (peoples power) for futher actions i.e kususia etc!

Hata hivyo sasa hivi tuko kwenye zama za Youtube, twitter na vingenevyo. Warekodi hotuba, download kwenye youtube ili walio na access na internet waone, pia waweke kwenye DVD na kusambaza kwenye matawi yao ili wananchi wanaoweza kufika kwenye matawi basi wasikie hotuba (wakati mwingine itabidi kufanya mambo kwa organic style!). Nina uhakika wananchi wakijua kuwa kila tarehe 30th ya mwezi kwenye ofisi fulani ya CDM kuna hotuba wataenda kusikiliza. hii itakuwa kama 'our own TEA-PARTY' na itavuta watu kibao. EVERYMONTH.

Mwisho, website ya CDM inabidi itumike ipasavyo. nadhani kwa sasa wamezongwa ila wajitahidi kuiweka sawa haraka iwezekanavyo. Kitila Mkumbo ni msomaji humu nadhani awashauri wapate webmaster atengeneze a user-friendly website, waweke low-resolution images ili watu waweze kufungua kwa urahisi. It is easy man if you know WARI AM SAYING:)
 
Mkuu, nimekuwa nafikiria hili kwa muda mrefu. Na ili kuwa na impact zaidi Chadema wanaweza kufanya hivi: Immidiately baada ya hotuba ya chama Tawala, wao wanatakiwa watoe yao ambayo kimsingi ni alternative views kuhusu mambo ambayo atakuwa ameongea mtoa hotuba wa CCM. Tukumbuke CHADEMA kazi yao ni kushawishi wananchi kuwa wao ni better kuliko ccm. Kwa hiyo kila hoja ya ccm wanatakiwa wajibu within 24hrs. Mfano kama hotuba ya ccm itakuwa Ijumaa basi Jumamosi isipite bila Chadema kutoa hotuba inayoonesha kwamba wao (chadema) watafanya vizuri zaidi ya ccm kwenye mambo yaliyoongelewa.

Nchi za wenzatu hasa Marekani wamekuwa wanafanya hivyo na impact yake ni kwamba inaupunguza kama si kuzima kabisa propaganda, na hata matukio ya Raisi kupewa takwimu zenye mgogoro zitapunguwa maana washauri wake watajua kuna kuumbuka kesho yake. Believe me hii itawapa kichaa CCM.

Goood idea! You've said it all!
 
Kwa kuwa CHADEMA ndiyo chama kikuu cha upinzani hapa TZ waTZ wana penda kusikia ujumbe maalumu toka kwa viongozi wao wakuu wa CDM,na kwa kuwa chama tawala cha magamba wana hotuba ya kila mwezi basi tunaomba CDM waanzishe hotuba ya kila mwezi.Wana JF mnasemaje?
Achaeni kuiga
 
Ni wazo zuri linatakiwa lifanyiwe kazi kwa kuanzia na kudai haki ya kutumia media za serikali kama TBC na radio kwa kipindi maaluma kwa wananchi maana CDM ni chama pinzani na kinatetea maslahi ya watanzania na maendeleo yao kama wanavyofanya CCM
 
Chadema si chama cha kuiga iga mambo,ukichukulia maanani hata hiyo hutuba ya Mkuu wa kaya anayoitoa kila mwezi haina tija yoyote zaidi ya Usanii uliobobea.
Chadema inayo mikakati yake ambayo inaleta na italeta tija kwa Watanzania wote na si kuiga chama cha Magamba.
 
Kumbe CCM wana hotuba ya kila mwezi mbona huwa siziskii...! Hotuba inatolewa na serikali kwakua inawajibu wa kuripoti utendaje wake kwa wananchi za Chadema utaziskia kwenye majukwaa ya siasa.
 
chama makini kilipojenga udom mlisema sera yetu nyie mnakamati kuu mabaraza wenyevt wa wilaya na mikoa wa cdm na sasa mwatakakuiga hotuba ya kila mwezi igeni tu coz ccm walimu wa siasa tz

hakuna wa kuwaiga nyie vimeo,lengo ni kukoso a unafik wenu.mfano mwadai uwongo ukisemwa sana huaminiwa bila ya kutaja uwongo huo inaelekea mnakuwa ndoton.
 
mie naunga mkono hoja hii ingawa CDM imekuja na style ya maandamano yasiyo na tija kwa watz isipokuwa ni njia ya kugawana ruzuku miongoni mwa viongozi waandamizi wa CDM:A S cry:
 
Mkuu, nimekuwa nafikiria hili kwa muda mrefu. Na ili kuwa na impact zaidi Chadema wanaweza kufanya hivi: Immidiately baada ya hotuba ya chama Tawala, wao wanatakiwa watoe yao ambayo kimsingi ni alternative views kuhusu mambo ambayo atakuwa ameongea mtoa hotuba wa CCM. Tukumbuke CHADEMA kazi yao ni kushawishi wananchi kuwa wao ni better kuliko ccm. Kwa hiyo kila hoja ya ccm wanatakiwa wajibu within 24hrs. Mfano kama hotuba ya ccm itakuwa Ijumaa basi Jumamosi isipite bila Chadema kutoa hotuba inayoonesha kwamba wao (chadema) watafanya vizuri zaidi ya ccm kwenye mambo yaliyoongelewa.
... Chadema wakijifanya ndiyo maconsultants wa CCM wanapoteza maana ya kuwa chama cha siasa. ...

UVCCM na jumuiya nyingine za CCM ndio zinatakiwa kutoa mawazo ya kuikosoa CCM kama chama ili kitawale vizuri. Wale ambao hatuikubali CCM jukumu letu ni kuidhoofisha ili ikataliwe zaidi na wananchi na hatimaye iondolewe madarakani. ...
?????????
 
?????????

Mkuu ninaposema kwamba 'CHADEMA kazi yao ni kushawishi wananchi kuwa wao ni better kuliko ccm' ninamaanisha waeleze ubovu na kuboronga kwa ccm huku wao (CHADEMA) wakeeleza watafanya tofauti kivipi. Kwa mfano sasa hivi Zitto anasema kuwa chadema watapunguza kodi kwenye mafuta ili bei ishuke. That is good maana inanesha udhaifu wa ccm katika kutatua tatiza la bei ya mafuta. You need to be clear unapomkosoa mtu/chama kwamba wewe una idea gani nzuri zaidi.
 
kwa kuwa chadema ndiyo chama kikuu cha upinzani hapa tz watz wana penda kusikia ujumbe maalumu toka kwa viongozi wao wakuu wa cdm,na kwa kuwa chama tawala cha magamba wana hotuba ya kila mwezi basi tunaomba cdm waanzishe hotuba ya kila mwezi.wana jf mnasemaje?

support-100%. Mnaoweza mfikishie dr slaa/mbowe/zito ujumbe huu
 
CDM wamekataa ku implement wazo la kuwa na TV yao, we have said this over and over again lakini sijawahi kuona kiongozi wa CDM akisema whether or not they are going to look into that idea.

Watanzania wengi wenye uelewa wamechoka kusikiliza propaganda za CCM toka kwenye almost all TV stations za hapa TZ. Tuna hamu ya kuwa na station inayotupa mawazo mapya, inayokutanisha vichwa vikaongea issues of the day (siasa, uchumi na jamii). Tunahitaji kusikia mawazo mbadala ya jinsi ya kuongoza nchi na kutuonesha failures za CCM kwa njia ya mijadala iliyoenda shule.

But CDM sijui kwanini hawajaiona hii avenue. Watu wamediliki kusema kuwa hata kama kuchangia uanzishwaji wa TV hiyo sie tupo tayari but its like they have decided they are not going to explore this wonderful opportunity.

Hiyo TV itakapokuwa on air kuna TV stations nyingi zitakufa including TBC1, CDM itaweza kupata mapato mengi sana out of this business.

Viongozi wa CDM please take this seriously, tuna kiu ya kusikia na kuona mawazo mbadala kwenye media na hasa TV, kwa sasa ni boredom of the highest order!!
 
cdm haina kiongozi wa kuweza kuchukua wazo zuri kama hili na kulifanyia kazi ruzuku wanayoipata imewachanganya
 
Back
Top Bottom