Mkuu, nimekuwa nafikiria hili kwa muda mrefu. Na ili kuwa na impact zaidi Chadema wanaweza kufanya hivi: Immidiately baada ya hotuba ya chama Tawala, wao wanatakiwa watoe yao ambayo kimsingi ni alternative views kuhusu mambo ambayo atakuwa ameongea mtoa hotuba wa CCM. Tukumbuke CHADEMA kazi yao ni kushawishi wananchi kuwa wao ni better kuliko ccm. Kwa hiyo kila hoja ya ccm wanatakiwa wajibu within 24hrs. Mfano kama hotuba ya ccm itakuwa Ijumaa basi Jumamosi isipite bila Chadema kutoa hotuba inayoonesha kwamba wao (chadema) watafanya vizuri zaidi ya ccm kwenye mambo yaliyoongelewa.
Nchi za wenzatu hasa Marekani wamekuwa wanafanya hivyo na impact yake ni kwamba inaupunguza kama si kuzima kabisa propaganda, na hata matukio ya Raisi kupewa takwimu zenye mgogoro zitapunguwa maana washauri wake watajua kuna kuumbuka kesho yake. Believe me hii itawapa kichaa CCM.