Hotuba kali ya mtoto Haramu

Hotuba kali ya mtoto Haramu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,094
Reaction score
79,492
HOTUBA YA MTOTO HARAMU.

Na, Robert Heriel.

Habari dunia, na wote mliomo juu yake. Siku ya leo ni siku ya furaha kwangu kuwaandikia andiko hili. Ni siku muhimu kuelekea SIKUKUU YA WATOTO HARAMU ambayo nimeinzisha mimi mwenyewe. Sikukuu hiyo itaazimishwa kila ifikapo tarehe 25 Machi kila mwaka ambapo ni siku niliyozaliwa. Lengo la maadhimisho haya yatakayofanyika kila mwaka, ni kuitangazia dunia kuwa sisi ni watu wenye mchango mkubwa duniani licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki kama vile, kunyanyaswa, kuteswa, kusimangwa, kubaguliwa, kutetwa, kupigwa, kuuawa, kutorithishwa mali, na kupewa majina yote ya hovyo na mabalaa.

Tunaishukuru jamii kwa kutupa nafasi duni miongoni mwa makundi ya watu. Tunashukuru jamii kwa kuruhusu tupewe majina yasiyo na staha. Majina ya matusi yenye dhihaka na kejeli ambazo zimekuwa zikiumiza hisia za miongoni mwetu.

Tunashukuru baadhi ya dini ambazo zinatuchukulia sisi kama watoto tusiostahili haki kama watoto wengine. Tunazifahamu dini hizo jinsi zilivyotutungia majina ya hovyo, hata hivyo tumeyakubali majina hayo. Zipo dini ambazo zimetupa majina ya kebehi na matusi, Ati sisi ni ‘watoto haramu’ , watoto wakambo, watoto wa zinaa, watoto wa nyoka, watoto wa makahaba, watoto wa malaya na majina mengine kama hayo.

Kwanza natoa rai na kuomba watoto haramu wote tusizitambue dini hizo. Kama sisi ni haramu basi nasi dini hizo tunazichukulia kama zinavyotuchukulia. Hizo sio dini, bali ni dini za hovyo ambazo Mungu wetu aliyetuleta duniani, huyo hawezi kutukuzwa katika dini hizo. Hatuwezi kuabudu kwenye dini zinazotutukana ilhali sisi tumezaliwa kwa njia tusiyoichagua. Na wala hatutathubutu kulaumu njia aliyotumia Mungu wetu kutuleta duniani, bila kujali njia hiyo itaonekana ni halali au haramu na mahasimu wetu.

Tunajua miongoni mwetu siye tulio haramu baadhi tulikataliwa na mababa zetu tangu tukiwa tumboni. Tunatambua kuwa Baba zetu walikuwa kwenye starehe zao, wala hawakuwa na kusudi la sisi tuje duniani. Ndio maana wengine walitukana na kusema mimba zetu wao sio wahusika. Tena Baba zetu hao wengine walikuwa katika ulevi, wengine katika tamaa ya ngono, wengine katika kutafuta mali za dunia hii hao ndio mama zetu. Sio kwamba hatuyajui mambo hayo, ukimya wetu haimaanishi hatuyajui bali ni kwa vile tuna hekima na tunajua aliyetuleta alikuwa na makusudi ingawaje ninyi hamkuta tuje.

Tunajua mimba zetu hazikupendwa hata kidogo, mtaani zilitukanwa, ndani ya familia zilionekana kama ni aibu na fedheha. Tunajua pia mimba zetu zilitungiwa majina na kuwafanya mama zetu kudhalilika na kujuta kwa nini walizibeba.

Wapo ndugu zetu watoto haramu ambao mimba zao zilichomolewa, ati hawakustahili kuzaliwa. Walitupwa chooni, wengine kufukiwa shimoni, wengine waliliwa na mbwa walipotupwa kwenye majalala. Yote ni kwa sababu hawakuonekana wanahaki ya kuishi kisa na mkasa ni watoto haramu.

Tunafahamu hamtupendi, tunajua siku mimba zetu zilivyotungwa vikao vya kifamilia vilikaa ati sisi tutolewe ili tusije kuzaliwa. Tunafahamu jinsi mlivyokuwa mkisema mpelekee mwenye huo mzigo kwa maana sisi tumizigo, yote hayo tunayajua. Tunajua upendo mnaotuonyesha sasa hivi ni matokeo ya unafiki wenu kwetu mkidhani hatujui na kama tunajua basi hatukumbuki.

Tunajua siku mimba zetu zilivyojulikana jinsi Mama zetu walivyotengwa huko makanisani na majumba ya ibada. Tunayajua yote hayo. Wala hatuwezi kujifanya tumesahau.
Tunajua jinsi mama zetu walivyochukia kubeba mimba zetu kwani waliona sio wakati wake. Tunajua malalamiko waliyokuwa wanayatoa siku tupo tumboni mpaka tunazaliwa. Maneno yao tunayajua.

Kuna wenzetu waliozuliwa kizaazaa siku walipozaliwa na kuonekana wanasura tofauti na Mababa zao. Tunakumbuka maneno yao. Kipeleke hicho kipanya chako kwa baba yake, huyo sio mwanangu, na maneno mengine kama hayo.
Tunajua Baadhi ya Mama zetu hawakuwa waaminifu waliingiwa na ujuha wa kipumbafu wakasingizia watu mimba zetu kwa wanaume wasiosahihi. Matokeo yake ilipobainika tulijeruhiwa na kunusurika kifo. Yote hayo sio kwamba hatuyajui.

Sisi watoto haramu tunajua tukiwa kwa Mama wa Kambo, au Baba Wa kambo jinsi vikao huko chumbani baina ya Mama mzazi/baba mzazi na mama wa kambo/ Baba wa kambo jinsi tunavyojadiliwa. Tunajua sisi ni watu wa kuzua migogoro na kuchochea vita vya kimapenzi na kimahusiano.

Sishangai jinsi watu wengi wasivyotutambua hata kwenye mambo ya kurithi. Sisi ni watoto haramu, hatuna haki ya kupewa urithi hata kama ni watoto wa kiume. Kama mlichukia sisi kuzaliwa haishangazi hata kidogo kutunytima urithi.
Sisi hatuna urithi, hatutambuliki. Sisi hatuna Baba wala hatuna Mama. Tunajua baadhi ya wamama hujifanya wanafiki baada ya sisi kuzaliwa lakini hawakutaka sisi tuzaliwe. Walituona tumekuja kabla ya muda. Walituona tunakiherehere cha kutaka kuvuruga ndoa zao baada ya wao kufanya zinaa nje ya ndoa licha ya kuolewa. Ati wao hawakuwa na kiherehere ila sisi ndio wenye vihere here.

Tunawatambua Mama zetu kwa unafiki ambao baadhi yenu mlituzaa baada ya kushindwa kutoa mimba zetu. Tunajua wengine kutwa mlikuwa mkilalamika na kuomba Mungu isiwe kweli kuwa mnamimba. Yaani mlitamani tuyeyukia matumboni mwenu. Lakini iliposhindikana ndio mkatuzaa kwa malalamiko huku kutwa mkitutukana tungali vichanga tusiojua hili wala lile. Mara kaa kimya, acha kulia, kamlilie Babaako Malaya Yule aliyekutelekeza.

Tunatambua Baba zetu wehu, ambao walituacha kwa matusi, wakiwapiga mpaka mama zetu ati kisa mimba zetu zimeingia. Dooh! Hivi mimba yangu kuingia ndio umpige mwenzako uliyepeana naye raha, Mbona hukumpiga siku ile mlipokuwa mkifanya starehe zenu. Starehe yake ndio inakufurahisha ila mimba zetu hakaa!

Tunajua hila za ndugu zetu ambao ati wao ndio watoto halali jinsi wanavyotunyanyasa. Jinsi wasivyopenda kuona tunafanikiwa. Ati sisi watoto haramu kufanikiwa kwao badala wafurahi ati wananuba. Kwa kawaida sisi watoto haramu hatujawahi kuwa na roho mbaya kwa maana hatukuja kwa makusudi ya binadamu tuliletwa kwa mapenzi ya Mungu. Hatujawahi kuombea ndugu zetu wasifanikiwe. Siku zote sisi tunapenda kuishi kwa umoja na upendo.

Hapana shaka kuwa sisi watoto haramu ndio tumeifanya hii dunia kuwa hivi ilivyo, kwa ujuzi na maarifa yetu. Hakuna asiyejua uwezo wetu hata hivyo tumekuwa watu wapole wenye subira na uvumilivu.
Tunaiambia Dunia, sisi hatukuja kwa mipango ya wanadamu. Hatukuja kwa vikao vya watu ati tuzae mtoto. Sisi tumekuja kwa nguvu ya mwenyezi Mungu licha ya kuwa Mama na Baba zetu hawakutaka iwe hivyo.

Sisi tunawapenda watu wote, Hatuna kinyongo na yeyote Yule. Ninyi ni ndugu zetu ingawaje hamtutambui.
Hatuna haja na maurithi yenu, hatutaki wala kuingilia mirathi na makorokocho ya namna hiyo. Sisi kama tulikuja kwa mapenzi ya Mungu bila nyie kutaka. Basi tutatafuta mali zetu wenyewe.

Hata hivyo tunashukuru kwa kuwa mnajua kuwa tunauwezo wa kutafuta mali zetu wenyewe ndio maana hamturithishi. Mnajua kiwango chetu cha uwezo wa akili, mapambano, ukakamavu na uvumilivu ndio maana hamuishi kutuandama.
Dunia tokea kuumbwa tumeonyesha uwezo wa kukabiliana na mazingira bila kutafuta upendeleo kwa wazazi wetu.

Upendeleo wetu upo kwa Mungu, ndio maana alituleta bila ya nyie kutaka. Lakini wengine walikuja duniani kwa kufungiwa na kuombewa miaka nenda rudi.
Hata hivyo wote ni watoto wa Mungu.
Watoto haramu ni hawa wafuatao:
1. Waliozaliwa kabla ya ndoa
2. Waliozaliwa ndani ya ndoa baada ya Mama kuzaa na mwanaume asiyemume wake.
3. Waliokataliwa na Baba zao
4. Waliotupwa na Mama zao
5. Mimba zilizotolewa na makundi yote yaliyozaliwa bila kufuata kanuni za ndoa kulingana na dini zao hizo za hovyo.

Tukutanae kwenye SIKUKUU YA WATOTO HARAMU Itakayofanyika siku ya tarehe 25 Machi. Kama wewe ni mtoto haramu ungana na watoto haramu wengine duniani kusherekea sikukuu yetu.

Siku hiyo mambo yafuatayo yanaweza kufanyika
1. Kutembelea wagonjwa
2. Kusaidia watu wenye uhitaji
3. Kutoa damu kwenye kituo chochote cha afya
4. Kujitolea kufanya usafi sehemu za umma kama hospitali,
5. Kutembelea wafungwa
6. Kutembelea watoto yatima na mambo mengine kama hayo

Hatuna haja ya kuomba kutambuliwa, ikiwa wewe ni mtoto haramu, mtoto wa nje, mtoto wa kambo huna haja ya kuomba kutambuliwa, huna haja ya kulia lia ati upewe upendeleo. Sema sitaki upendeleo. Aliyekuleta ndiye atakayekupa upendeleo. Kama hawakutaki achana nao, wala hawana la ziada kukuzidi zaidi sana wanahofu utawazidi.

Angalizo: Andiko hili halihalalishi zinaa hivyo amri za Mungu zitabaki pale pale bila kuathirika na andiko hili.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300/ 0711345431
 
Pole sana.umeandika kwa uchungu mno.
Yote na yotee.
DUNIA ni ya wotee
 
So touching,hata Daudi Mfalme inaaminika alikuwa mtoto wa aina hii, Jephthah pia soma Waamuzi 11 alikuwa Mwamuzi mzuri tu Mungu alimheshimisha. Mtoto huyu huwa amebeba baraka, karama au vipawa vya kipekee sana.
 
So touching,hata Daudi Mfalme inaaminika alikuwa mtoto wa aina hii, Jephthah pia soma Waamuzi 11 alikuwa Mwamuzi mzuri tu Mungu alimheshimisha. Mtoto huyu huwa amebeba baraka, karama au vipawa vya kipekee sana.
Karibuni katika Dini yangu.
Mungu wangu kaagiza kuwa
Wale wote wasiojulikana baba zao au
kuzaliwa kwa namna isiyokuwa kawaida katika jamii na
wakawa ni watu wema.
Basi wana haki sawa na watu wengine mbele za Mungu wangu.
Na akawapa jina tukufu mno.
Akataka waitwe "Waja ma Mwenyezi Mungu" (Abdallah)
Mfano wewe jina lako ni Daudi ubini wako ni Mja wa Mwenyezimungu.
Na mfano wewe ni Fatma binti Mja wa Mwenyezimungu (Abdallah)
Karibuni wote .
Mungu anawapenda
hamna kosa lolote ila yale mutakayo yafanya wenyewe binafsi.
Ni wazazi wenu ndio watahukumiwa kwa makosa yao ,na kama wakitubu nao watasamehewa.
Mungu wangu ni mkarimu mno kwa watu.
 
Hii inasikitisha kwa kweli
Binadamu ni wakatili sana na wengi hawana huruma kabisa
Ila wapo wema pia waliowakubali na kuwalea


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Uislamu ni Dini ambayo ni mfumo kamili wa maisha ya mwanaadamu katika maisha haya ya duniani. Hapana chochote ambacho ni muhimu kwa mwanadamu isipokuwa Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) wametuelezea. Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) anasema:

“Hatukupuuza (Hatukuacha) Kitabuni kitu chochote” (6: 38).

Katika Uislamu kitendo hicho cha zinaa ambacho kimefanywa na mwanaume na mwanamke ndio makosa na waliofanya wanafaa waadhibiwe hapa duniani ili wasafishwe kwa kosa lao hilo hadharani. Na Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Ametuagizia Tusikaribie kabisa zinaa (17: 32). Lakini tufahamu ya kwamba yule mtoto anayezaliwa hana hatia yoyote. Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema:

“Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Naye Atakuambieni mliyo kuwa mkitofautiana” (6: 164).

Na Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) amesema: ((Kila kinachozaliwa kinazaliwa katika Uislamu .....)) l-Bukhaariy).

Na haifai kwa Muislamu kumuita mtoto aliyezaliwa kwa jina la mwana-haramu kwa sababu mtoto mwenyewe si wa haramu bali kitendo chenyewe ndicho haramu. Na ieleweke kuwa mtoto huyu hataitwa kwa jina la huyu mwanaume aliyezini na mamake kwa sababu kisheria si mtoto wake wala hawa wawili hawarithiani kabisa. Mtoto huyu hatamrithi huyo mwanaume na huyo baba hatamrithi mtoto huyo. Lakini mtoto anaweza kumrithi mama yake na mama kumrithi mtoto wake.



Tanbihi kwa kila mmoja wetu ajichunge sana ili asiingie katika madhambi haya ya zinaa. Na ndio sheria ikafanya ndoa kuwa rahisi na ikaweka adhabu kali kwa wenye kuzini.



Na Allaah Anajua zaidi.
 
Akhy umeelezea vzr sn allah akulipe kwa hili. ila baba kama ana uwezo naweza kufanya majukumu yote kwa mtoto huyu kama kumsaidia kimaisha kama vile kumsomesha, kumuhudumia matibabu na kuhakikisha kua anapata malezi bora, na pia anaweza mjengea nyumba au kumpa kiwanja kama zawadi na sio kumpa kama mtoto. Kitu pekee kwenye dini kilichokatazwa ni kuhalalisha mirathi na kuhalalisha undugu baina yako na mtoto huyu ila matumizi yote unaweza kutoa kwa kijana au bint huyu. Pia kuzaliwa nje ya ndoa sio sababu ya ww kua mcha mungu wapo mabint na mabrobaro wengi tu walizaliwa nje ya ndoa na ni wachamungu wazuri tu. So ewe ndugu yetu usihuzunike wala kujisikia vibaya, achana na maneno ya watu mitaani allah anajua uwepo wenu, na Allah anajua zaidi.
Uislamu ni Dini ambayo ni mfumo kamili wa maisha ya mwanaadamu katika maisha haya ya duniani. Hapana chochote ambacho ni muhimu kwa mwanadamu isipokuwa Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) wametuelezea. Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) anasema:

“Hatukupuuza (Hatukuacha) Kitabuni kitu chochote” (6: 38).

Katika Uislamu kitendo hicho cha zinaa ambacho kimefanywa na mwanaume na mwanamke ndio makosa na waliofanya wanafaa waadhibiwe hapa duniani ili wasafishwe kwa kosa lao hilo hadharani. Na Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Ametuagizia Tusikaribie kabisa zinaa (17: 32). Lakini tufahamu ya kwamba yule mtoto anayezaliwa hana hatia yoyote. Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema:

“Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Naye Atakuambieni mliyo kuwa mkitofautiana” (6: 164).

Na Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) amesema: ((Kila kinachozaliwa kinazaliwa katika Uislamu .....)) l-Bukhaariy).

Na haifai kwa Muislamu kumuita mtoto aliyezaliwa kwa jina la mwana-haramu kwa sababu mtoto mwenyewe si wa haramu bali kitendo chenyewe ndicho haramu. Na ieleweke kuwa mtoto huyu hataitwa kwa jina la huyu mwanaume aliyezini na mamake kwa sababu kisheria si mtoto wake wala hawa wawili hawarithiani kabisa. Mtoto huyu hatamrithi huyo mwanaume na huyo baba hatamrithi mtoto huyo. Lakini mtoto anaweza kumrithi mama yake na mama kumrithi mtoto wake.



Tanbihi kwa kila mmoja wetu ajichunge sana ili asiingie katika madhambi haya ya zinaa. Na ndio sheria ikafanya ndoa kuwa rahisi na ikaweka adhabu kali kwa wenye kuzini.



Na Allaah Anajua zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto hawa wanabaguliwa na kufichwa tokea utoto.

Ni watoto ambao mara nyingi hawalelewi na mama wala baba wanalelewa na bibi.
Yes bibi iwe mzaa mama au baba.

Akienda kwa baba yake mama yake wa kufikia kisirani sana na wengine hawawezi ficha hisia zao na kuwafanyia matendo ya kikatili.

Wakienda kwa mama mzazi wanakuta kaolewa na familia yake na mama mzazi pengine kutokana na presha kwa mumewe au ndugu wa mume anashindwa kutimiza umama wake kwa mtoto huyo na anaonekana intruder.
Ni mtoto ambae analelewa na bibi au wa kupigwa danadana kwenye nyumba za ndugu leo atalelewa huku kesho atapelekwa kwingine.

Ni mtoto ambae baba anaishi masaki na familia yake watoto wanasema St academia mama anaishi mbezi Beach na mumewe na wanae wengine, mtoto haramu anaishi mwanalumango na bibi au shangazi kwa kulala sebuleni kutandikiwa kipande cha godoro au manguo.


Ni mtoto ambae hata ikitokea kuna msiba au tatizo la kifamilia ataambiwa na ndugu wa mbali wa sana si mama au baba.
Na wengi wao huwa hawawajui baba zao wanafichwa baba zao.



Furahini katika bwana watoto wa haramu.
Nina mengi ya kuwaandikia ngoja niishie hapa.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
So touching,hata Daudi Mfalme inaaminika alikuwa mtoto wa aina hii, Jephthah pia soma Waamuzi 11 alikuwa Mwamuzi mzuri tu Mungu alimheshimisha. Mtoto huyu huwa amebeba baraka, karama au vipawa vya kipekee sana.
Ni solomoni ama Suleiman mtoto wa mfalme Daudi
 
Ni solomoni ama Suleiman mtoto wa mfalme Daudi
Hapa nilimaanisha Daudi, kulingana na Zaburi 51:3-5
Tazama! Nilizaliwa kwa maumivu nikiwa na kosa,
Na mama yangu alinichukua mimba katika dhambi.

commentaries nyingi kuhusu huu mstari zinasema kuwa mamake Daudi alitenda dhambi ndio akamzaa, jaribu kukumbuka pia kisa cha baba yake ambavyo hakumwita pamoja na kaka zake siku Nabii Samuel alipofika nyumbani kwao kumpaka mafuta kumtawaza kuwa mfalme, inasemekana hiyo ni moja ya sababu kwa nini Daudi ni kama alibaguliwa mpaka mwishoni kabisa Nabii aliposisitiza

Did David's Mother Commit Adultery?

King David’s big, dark secret

DID DAVID'S MOTHER COMMIT ADULTERY |
 
Back
Top Bottom