HOTELI YA KWANZA CHINI YA ARDHI

HOTELI YA KWANZA CHINI YA ARDHI

FM facts

Member
Joined
Mar 16, 2019
Posts
45
Reaction score
88
Kwa Mujibu wa Jarida Maarufu Duniani la Forbes, Hii ndio Hotel ya Kwanza Duniani Kujengwa Chini ya Ardhi.. ina Ghorofa 18, lakini Ghrofa 16 Zote ziko Chini ya Ardhi na Mbili Zilizobaki ziko Chini na Maji.

Hotel hii Ipo Chen Hua Barabara Namba 5888, Wilaya ya Songjiang Huko Shanghai Kilomita 50 Kutoka Katikati ya Mji wa Shanghai Mashariki mwa CHINA na Ilizinduliwa Rasmi November 15, 2018 na Kuanza Kuingiza Wateja December 1, 2018 Baada ya Miaka 10 Kupita Tangu Imeanza Kujengwa.

Kwa Mujibu wa Mtandao wa Hoteli Hiyo, Bei ya leo Jumanne March 26, Chumba Kimoja cha Kulala Katika Hotel hii Kinalipiwa TSHS 1,637,869 (1.6Million). Unaweza Kupiga Namba +86-21-67661888 Kama Utahitaji Kuweka Oda ya Vyumba Hapo.[emoji41]

Hoteli hii ina Julmla ya Vyumba 336 na Imejengwa Futi 289 (Mita 88) Ndani ya Ardhi ambapo Kuna Jumla ya Ghorofa 18, 16 Ardhini na 2 Majini na Imetumika Karibia TSHS. Billion 700 Mpaka Kukamilika Kwake. ([emoji118]Swipe)

Website ya Hotel: https://www.ihg.com/intercontinental/hotels/us/en/shanghai/shghe/hoteldetail
Mawasiliano ya Hotel: +86-21-67661888

Mmiliki wa Hotel Hii ni Kampuni ya Shimao Group ya China Iliyoanzishwa Mwaka 2001, na ni Kampuni inayomiliki Majengo Mengine Mengi sana Nchini China Zikiwemo Hotels Pamoja na Majengo ya Biashara, na Mmiliki wa Kampuni hii ni 'Hui Wing Mau' Pamoja na Mwanae Jason.

Billionea huyu 'Hui Wing Mau' Mwenye Asili ya Australia ana Umri wa Miaka 69 sasa, Ni Moja Kati ya Matajiri Wakubwa 15 Nchini China na Utajiri wake Unafika Dolla za Kimarekani Billion 9 Nyuma ya Matajiri Wengine Kama Jack Ma, Yung Wei, Li Ka Shing N.K.
20190326_031148.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom