Hoteli/Lodge nzuri iliyopo Bagamoyo

Hoteli/Lodge nzuri iliyopo Bagamoyo

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
6,551
Reaction score
20,260
Wasalaam,

Weekend hii baada ya shamrashamra za Valentines day nategemea kujivuta Bagamoyo kwa mapumziko mafupi.

Nimejaribu ku google nione sehemu nzuri ya kufikia ila napata sehemu za ghali sana nje ya bajeti yangu. Pia naona nyingi kwenye mtandao ni za zamani zamani. Mimi nataka hoteli / lodge ya 50 - 80 iliyotulia, safi mpya mpya.

Naomba mwenye uzoefu na maeneo hayo anisaidie.
 
50 - 80 utazipata Tabata siyo Bagamoyo...

Kama huna hela kwa nini ujipe taabu???
 
50 - 80 utazipata Tabata siyo Bagamoyo...

Kama huna hela kwa nini ujipe taabu???
Mkuu ina maana 80,000 sio hela? Sitaki kuamini kwamba Bagamoyo nzima siwezi pata lodge kwa bei hiyo!
 
Tatizo la bagamoyo vitu vya kawaida kabisa lakini ghali hatari. Utadhani wageni wote kule ni watalii.

Kuna lodge moja(Firefly kama sijakosea jina), ila kama ni mwenyeji ipo kale kanjia ka kuelekea soko la samaki upande wa kushoto. Ile sehemu ni cheap halafu nzuri sana. Au kama unatokea hospitali wa wilaya kuelekea soko la samaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom