Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 753
- 1,812
Mwanafunzi Criff Laiza [12] anayesoma darasa la Tano shule ya msingi Sekei katika halmashauri ya Arusha, amekufa maji wakati akiogelea kwenye bwawa la maji yenye kina kirefu katika hotel ya kitalii ya Mount Meru iliyoko jijini Arusha wakati wa sherehe ya X-mass .
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12 jioni wakati marehemu na watoto wengine wakiogelea katika hotel hiyo ikiwa ni sehemu ya kusheherekea sikukuu ya X-mass .
Kaimu meneja wa hotel ya Mount Meru , Eric Mgenya akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi na atalitolea ufafanuzi baada ya polisi kukamilisha upelelezi wa tukio hilo .