Hospitali zetu ni salama kiasi gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali zetu ni salama kiasi gani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 23, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Maoni ya Katuni  Mwaka jana lilitokea tukio baya la kuuawa kwa wagonjwa wa akili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, baada ya mgonjwa mmojawapo kuwashambulia wenzake kwa chuma kwa kuwapiga kichwani. Hili lilikuwa ni tukio la kushtua na ambalo liliacha maswali mengi juu ya usalama wa hospitali zetu.
  Maswali hayo yaliulizwa kwa sababu hospitali ni mahali pa mwisho anakopelekwa mgongwa kuokoa maisha yake kutokana na ugonjwa unaomkabili na kwa kweli haiingii akilini kwamba ni sehemu ambayo tukio la mashambulizi kama yaliyotokea lingeweza kutokea.
  Wakati kumbukumbu za tukio hilo likiwa bado kwenye vichwa vya watu wengi, mwishoni mwa wiki limetokea tukio jingine la kuogofya la mama aliyejifungua kuvamia watoto njiti, akiwamo wake, na kuwaua katika hospitali ya Bombo mkoani Tanga. Ni tukio la kusikitisha sana.
  Taarifa za awali zinaonyesha kwamba mama huyu ambaye anashikiliwa na polisi, anadaiwa kufanya mauaji hayo kutokana na kupatwa na kifafa cha mimba, hali iliyomfanya apoteze ufahamu na hivyo kufanya mambo kama mtu aliyerukwa na akili.
  Tunasikitika kwamba tukio jingine baya limetokea katika hospitali zetu, tena zinazomilikiwa na serikali. Ni masikitiko kwa sababu watoto hao njiti ni viumbe hai ambao tayari walikuwa wamekwisha kuja duniani, na kwa kweli kwa sababu ya kuongezeka kwa utaalam wa kitabibu, wangepona tu na hivyo kuja kuwa raia wema baadaye.
  Tunaungana na ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na misiba hii miwili kwa kuwapa pole, huku tukiwaomba wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
  Hata hivyo, tunageukia wenye dhamana na hospitali za umma, hususan Mganga Mkuu wa hospitali ya Bombo, madaktari na wauguzi wa zamu na wote wenye wajibu wa kusimamia uendeshaji wa kila siku wa shughuli za hospitali hii kwamba walikuwa wapi hadi maafa haya yanatokea?
  Tunawahoji wao pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kama tukio la Muhimbili halikuwafungua kwa maana ya kutazama upya mfumo wa usalama katika hospitali za umma.
  Tunauliza haya kwa sababu tunaamini kama kweli matukio haya yangekuwa yanatokea katika hospitali binafsi, ama leseni zake zingesimamishwa huku wamiliki wakikabiliwa na maswali magumu ya kujibu kama si kushtakiwa mahakamani!
  Tunashindwa kujua ni kwa nini basi katika taasisi hizi za afya za umma suala la usalama si kitu cha kujisumbua nacho? Inakuwaje basi mama mwenye kifafa cha mimba aachwe huru kiasi hicho, atembee mwenyewe huko na huko, mpaka afikie watoto njiti, kisha aue mmoja baada ya mwingine kwa kumbwaga wake chini kabla ya kumngÂ’ata wa mwenzake kisha kumbwaga chini pia?
  Pia inakauwaje mama huyu aachiwe uhuru huo baada ya kuonyesha kila dalili ya kupoteza utimamu wa akili, arande huko na huko wodini, avunje vifaa vikiwamo vyombo vya wagonjwa wengine waliolazwa wodi ya wazazi, lakini asidhibitiwe na yeyote?
  Tunauliza maswali haya kwa sababu inawezekana kabisa katika wodi hiyo hakuwepo muuguzi wa zamu na kama alikuwako basi hakuwa eneo lake la kazi, na kama alikuwepo, basi alishindwa kuwajibika vilivyo kwa majukumu yanayomkabili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama wa wagonjwa walioko kwenye wodi yake.
  Baada ya tukio la Muhimbili na hasa baada ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza yaliyotokea kiasi cha kusababisha kuuawa kwa wagonjwa wengine wodini, tulitazamia kwamba udhaifu wa Muhimbili ungetumika kubuni mkakati mpya wa usalama wa wagonjwa wawapo wodini.
  Na mkakati huu ungewasilishwa kwa hospitali zote za umma, lakini pia kutoa hadhari kwa hospitali za binafsi jinsi ya kujipanga kuhakikisha kwamba usalama wa wagonjwa ama wakiwa wodini au hata wa Idara ya kwenda na kurejea makwao, unaimarishwa kwa kuweka mfumo wa kuwaangalia wagonjwa wakati wote.
  Ni jambo la bahati mbaya kwamba licha ya kupata janga la Muhimbili, bado uzoefu ule haujatushitua kama taifa na watendaji wa taasisi za afya za umma ili kubuni mbinu na mikakati ya kuhakikisha usalama kwenye taasisi hizi ni kitu cha kuzingatiwa kwa nguvu zote.
  Tunasema haya yaliyotokea Bombo hayakupaswa kutokea, ni matokeo ya ama kushindwa kujipanga au ni mwendelezo wa ile hulka ya watu wetu ya bora liende, kwamba mtu anafika kazini jina, lakini ukweli ni kwamba hakuna uwajibikaji wowote. Hali hii haivumiliki.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  MziziMkavu... Hiyo katuni hapo juu inahusiana na habari hiyo??

  Hizi Hospitali zetu za serikali kwa kweli ni kuomba Mungu tu...
   
 3. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Hivi unajua kuwa karibu Hospitali nyingi Tz sasa hivi hawana gloves wala dawa na kisingizio chao ni Audit inayoendelea MSSD kwa kipindi cha June yote na hakuna anayekubali kuwa pana tatizo hilo, lakini kwa kuwa watu wanakubaliana na kupewa fulana za kijani waacheni waambukizane mpaka watakapong'amua kuwa Kenya hawakufanya kosa
   
Loading...