Hospitali za Umma na Hospitali za Private (Binafsi)

Dr James G

Senior Member
Oct 16, 2016
147
242
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu aliwahi kusema kua watu wengi wanapenda kuanzia matibabu hospitali za private kwa muda mrefu unakaa uko haponi au anazidiwa ndo ndugu wanamuhamisha mgonjwa hospitali za Umma akifika hospitali za umma anashindwa kulipia huduma kwa sababu alimaliza hela hospitali binafsi na bila kupona.

Lengo na uzi huu sio kuziponda hospitali za private kua wagonjwa hawaponi na garama ni kubwa hapana ila lengo ni kuzisemea sasa hospitali za umma kwani kwa sasa hopitali zetu za umma zinatoa huduma nzuri tangu mapokezi hadi kuonana na daktari japo sio zote lakini kuna mabadiliko makubwa sana tofauti na zamani.

Uwekezaji mwingi umewekwa kwenye sekta ya afya, vifaa tiba na wataalam bingwa wengi, watendaji wa wizara kuanzia waziri, naibu waziri na makatibu wote wako makini na wafatiliaji.

Taasisi zilizo chini ya wizara mfano JKCI imekua mfano mzuri kwa Africa, hospitali ya Muhimbili, Benjamini Mkapa nk

Watanzia wenzangu tuziamini hospitali za umma kwa sasa wanajitahidi huduma ni bora, wajawazito, watoto na watu wazima, huduma za kibingwa na huduma za dharura (emegency department).

IMG_0895.jpg




MATUMIZI YA AMBULANCE
Ningeishauri kua na utaratibu wa matumizi ya gari za wagonjwa yenye vifaa muhimu vya kumsaidia mgonywa wa dharura, kumchukua mgonjwa toka nyumban had hospitali hii ingepunguza vifo vingi vinavyotokea mara tu mgonjwa anapofika hospitali.

Yawezekana hizo gari zipo lakini zingefanyiwa utaratibu watu wajue watangaziwe namba ya dharura gari ikipigiwa ifike kwa mapema ikiwa na muhudumu, huduma hii sio lazima ifanywe na serikali tu lkn hata makampuni binafs wanaweza fanya na hosp binafsi, gari nying za wagonjwa hazina vifaa vya huduma ya kwanza bali ni nafasi tu ya kumuweka mgonjwa kias kwamba hata mgonjwa akizidiwa ni rahisi kufia njiani.

Mwisho lakini sio kwa umuhimu serikali kupitia wizara ya afya itoe elimu juu ya bima ya afya kwa wote, uwezo wake kumsaidia mgonjwa hata wa hali ya chini kuweza kupata huduma zote muhimu za kitabibu na vipimo vikubwa, bima ya afya kwa wote isiwe tu kila mtu awe na bima ila kila mtu kwa uwezo wake bima imsaidie kupata huduma zotee muhimu .

Nitakua mchoyo kumaliza uzi huu bila kumpongeza mwana mama Ummy Mwalimu na naibu wake Dr. Mollel pamoja makatibu wote wa wizara ya afya, watumishi wa taasisi na hospital zote za umma na private kwa kuendelea kuwahudumia watanzania wenzao kwa moyo na upendo.
 
Back
Top Bottom