Hospitali ya wilaya inakosa japo panadol!

emkey

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
728
136
Habari wadau.
Wiki 2 zilizopita nilimpeleka mke wangu hospitali wilaya ya kilwa kujifungua, cha ajabu ni kuwa nilipewa orodha ndefu ya dawa za kununua maduka ya dawa yaliyopo nje karibu na hospitali. Miongoni mwa dawa hizo imo panadol, pia niliambiwa kununua hadi kiwembe, gloves, cordclamp, pamba, drip, mabomba ya sindano, dawa za sindano na kadhalika. Nikajiuliza, hospitali hii ipo ktk bajeti au bajeti haipo ktk hospitali hii! Pia hapa hospitali ya kilwa kivinje hawana kipimo cha kuangalia wingi au uchache wa damu, ndugu wa mgonjwa anapewa damu ya mginjwa na anaambiwa aipeleke maabara yeye kwa vipimo. Naomba waziri mwenye dhamana ulishughulikie hili, nipo tayari kukupa ushirikiano.
 
Sasa mkuu cha ajabu ni nini?? Sio za wilaya tu hadi za mikoa, mimi juzi yamenikuta tmk, ila siku shangaa sana kwani, ukiwasikiliza wanasiasa wanavyowaaminisha wananchi, ukienda field sasa utachoka yaani ni vitu tofauti kabisa!!!
 
Inasikitisha sana..ngoja nieke vzr kichinjio changu mpk 2020 niwachinje vzr
 
Back
Top Bottom