Hospitali ya Mwananyama mambo yaleyale | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali ya Mwananyama mambo yaleyale

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sumasuma, Feb 9, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwandishi Wetu,
  HALI ya wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala Manispaa ya Kionondoni ,Dar es Salaam jana iliendelea kuwa mbaya baada ya wagonjwa hao kulalamikia vitendo vya kutelekezwa.Licha ya Serikali kuwataka madaktari wote warejee kazini, lakini uchunguzi wa gazeti hili ulijionea wagonjwa wakiwa katika hali mbaya.

  Wagonjwa waliohojiwa walisema wagonjwa wapya wanaoingia katika hospitali hiyo walikuwa wakisikilizwa bila kupatiwa tiba kama invyotakiwa.

  Aidha wagonjwa wa wodini wengi wao walisema walikuwa wakipatiwa huduma ndogondogo na wauguzi ambao walionekana kuwa wenye huruma zaidi.

  “Kwakweli hapa wanaohudumiwa ni wajawanzito na watoto, kwa wagonjwa lakini wagonjwa wengine wanaosumbuliwa na matatizo mengine wanansikilizwa na kutelekezwa’’, alisisitiza mgonjwa.

  Mgonjwa huyo ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake alisema kumekuwa na vikundi vya madaktari kukaa muda wa kazi haieleweki ni jambo gani linalozungumziwa kwa muda wote.

  Lakini Ofisa Afya wa Manspaa ya Kinondoni, Dk Gunini Kamba alisema mgomo kwa hospitali hiyo umepungua baada ya kuwaondoa waliogoma na kubakiwa na madaktari walioajiriwa na Manispaa hiyo ya Kinondoni.

  “Tumewaondoa madaktari 42 waliokuwa wamegoma na kwasasa waliobaki ni waajiriwa na mansipaa, huduma inatolewa kama kawaida , tangu mgomo uanze ni wiki mbili ,tumekuwa tukiwapokea wagonjwa kutoka katika Hospitali ya Temeke kutokana na uchache wa madaktari tunatoa kipaumbele kwa wajawazito na watoto kisha huduma kwa wote. Lkaini hakuna mgonjwa anayeondoka bila kutibiwa” alisema Kamba.

   
Loading...