Hospitali ya mkoa wa Mara ni shida, RC Mara ipitie

jmi

JF-Expert Member
Sep 11, 2015
532
468
Mama yangu mzazi leo trh 28 12 2016 saa 01.00 asubuhi amefikishwa hospitalini hapo akiwa mahututi. Mimi nilisafiri toka nikikokuwa hadi hospitalini hapo na kumkuta mama. Niliwauliza nurses kama amefanyiwa vipimo ajabu nurses wananijibu kuwa Dr. hajaandika mama afanyiwe vipimo.

Niliomba file la mama nikakuta ameandikiwa kufanyiwa vipimo haja ndogo, kubwa na damu niliwaambia nurses ndiyo wakasema mda huo wa saa 9 jioni hospitalini hapo hawafanyi vipimo mpaka kesho asubuhi.

Ina maana nisingeenda hispitalini hapo mama asingefanyiwa vipimo. Ajabu hata nurses hawakusoma hata file la mgonjwa.

Kweli baba Rais Magufuli kazi bado unayo. Na hii ndiyo Tanzania. Pamoja na tumbua tumbua lakini watu hawabadiliki.
 
Kuna no za simu za viongozi zinakuwepo mapokezi kuanzia ya Mganga Mfawidhi mpaka ya Waziri kama sikosei.
Asante kwa maelekeo mkuu. Huku mm ni mgeni ngoja nicheki hizo number ikibidi nimpeleke kwa mgonjwa na baada ya hapo nimtoe mgonjwa wangu kwa tahadhali
 
jmi pole sana lakini umesahau huyu mganga mkuu aliwekwa ndani na mfalme wa eneo hilo?unategemea wauguzi watakujibu vipi kama ungekuwa wewe ndio mganga mkuu ungejisikiaje
 
Mimi baba yangu alipataga ajari ya gari akafikishwa hosptal huko mara wakaishia kumtazama tu hadi akaaga dunia kizembe zembe nawachukia wahudunu wa huko sana R. I. P baba yangu ulikufa kwa uzembe wa wahudunu
 
Back
Top Bottom