Hospitali ya Mkoa wa Arusha (Mt. Meru)

Hospitali ya Mkoa wa Arusha (Mt. Meru)

love more than100

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2014
Posts
2,061
Reaction score
715
Habari za J3 natumai nyote muwazima,

Kilichonileta leo kuandika mada hapa maana kwa asilimia kubwa huwa ni muangaliaji but leo nami nimepata cha kuja kuuliza humu kuhusu hospitali ya mkoa wangu ya Mt. Meru na nachouliza za kutaka ufafanuzi ni hii sera mpya iliyopo ya mwanamke kujifungua.Hii sijui niite sera ama Sheria ilishaptishwa mimi na baadhi ya wenzangu kwa 98% hatuijui au ni kitu kilichoanzishwa na Serikali,wafanyakazi,bodi au?

Ni kwamba naona matangazo kwenye TVs, Magazeti na kusikia katika Radios kuwa mwanamke mjamzito anayekwenda kujifungua hatakiwi kulipishwa au kudaiwa chochote au kwenda na vifaa vya kujifungulia kama glovs nk! Sasa sijui hivyo vifaa vipogo au havipo katika hospitali hii maana ukienda mwanamke kujifungua lazima uwe navyo tena vingi.

Na sasa wameongeza uwe na 10,000 na ndoo ndogo ya kutia nguo zako hii ya ndoo naweza sema llibidi ni usafi kuzingatiwa ni sawa ila sasa hivyo vifaa na hiyo 10,000 ya nini huku Serikali inatangaza kuwa utakiwi kulipishwa na vifaa utavikuta hukohuko?Ikiwa umetokea kwenda huna hivyo vitu unatukanwa matusi ya nguoni na unaachwa hapo mapokezi akugusi wala akupokei mtu.

Naomba tu kujuzwa je, hili limepitishwa kihalali na kama ndio kwanini wasitoe matangazo kwenye vyombo vya habari kuwa mwanamke yeyote anayetaka kuja kujifungulia Mt. Meru hosp anatakiwa kuja na hiki na hiki ili watu tujue na tusifatilize tangazo la Serikali?
 
Mkuu watakuja kukujibu japo hujauweka sehemu yake huzika kule habari na hoja mchanganyiko
 
Ndugu, sasa kama serikali yako inapanga bajeti na haifikishwi kwenye hospitali nesi afanye nini? Manake kati ya watu wanaokutana na dilemma kwenye mazingira ya kazi ni waalimu na watoa huduma za afya. Nawahurumia tu
 
love more than100

Ndugu yangu,hivyo vyote unavyovitaja vinaongelewa kwenye TV tu,lakini km wasipokwenda na hivyo vifaa wao wenyewe watapata shida baada ya kujifungua, Serikali imetangaza tu lakini haitekelezi inachotangaza,kwa maana nyingine ni kuwachonganisha watoa huduma za afya na wapewa huduma. Labda nikuulize ulishawahi kuchunguza zaidi kujua ni kwa nn inafanyika hivyo!?
 
Last edited by a moderator:
Weee achana na propaganda za tv

Mjamzito ahakikishe yupo kamili lasivyo atasanda...

Vifaa vyenyewe mahospitali hakuna
 
Serekali inatangaza tu lakini utekelezaji hakuna, na kingine watanzania wengi sana hawalipi kodi sasa mtu halii kodi alafu anategemea huduma ya bure?
 
Serekali inatangaza tu lakini utekelezaji hakuna, na kingine watanzania wengi sana hawalipi kodi sasa mtu halii kodi alafu anategemea huduma ya bure?

Hebu nitajie huyo mtanzania asielipa kodi yukoje?
 
Serekali inatangaza tu lakini utekelezaji hakuna, na kingine watanzania wengi sana hawalipi kodi sasa mtu halii kodi alafu anategemea huduma ya bure?

Yaani unataka kutueleza huduma ni mbovu kwa ajili ya kodi? Unajua Tanzania ni nchi ya ngapi kati ya nchi zinazotoza kodi kubwa? Unajua ni watumishi wa ngapi wa Serikali tu ambao wanakatwa kodi?
 
Hebu nitajie huyo mtanzania asielipa kodi yukoje?

Wa tz wengi wanaolipa kodi ni wafanyakazi coz it's simple kumkata mshahara wake, kuna siku niliuza gari yangu ya zamani na nilipata pesa na kodi sikulipa ,alie lipa ni yule niliemuuzia alienda kubadili jina
 
Yaani unataka kutueleza huduma ni mbovu kwa ajili ya kodi? Unajua Tanzania ni nchi ya ngapi kati ya nchi zinazotoza kodi kubwa? Unajua ni watumishi wa ngapi wa Serikali tu ambao wanakatwa kodi?

Nakuelewa na ndo maana kodi kubwa inaenda kwa wafanyakazi ili kufidia watu wengi ambao hawalipi kodi, na wanaingiza pesa,
 
Kilichonifurahisha sana ni usafi tofauti na zamani juzi nilikwenda kumjulia hali mke wa jirani yangu nilishangaa sana jinsi usafi ulivyotamalaki.Zile harufu mbaya,uchafu,maji maji hakuna kabisa mtu unaweza kupewa msosi ukala bila bugza.

Hongera sana uongozi wa Mt Meru Hospital.
 
Nakuelewa na ndo maana kodi kubwa inaenda kwa wafanyakazi ili kufidia watu wengi ambao hawalipi kodi, na wanaingiza pesa,

Exactly, ndiyo maana nikauliza hayo maswali hayo hapo juu ambayo sijapata majibu yake, huwezi kuweka rehani afya za watu kwa kigezo cha Tax, hii hakuna duniani kote, esp. kwente nchi yenye resources kama hii.

Pili, mimi na wewe tunajua uhakisia mjamzito, wazee watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanalipa hadi leo hii, haya ni makundi yaliyokuwa na msamaha(exemption), swali ni kwamba kwanini Serikali iendelee kusisitiza kuwa huduma kwa makundi haya ni bure?

Mwishowe tunawaona madaktari, wauguzi wakituagiza kununua hiki au kuleta hiki eti "wananatafuta chochote".
 
Serikali hii ni chonganishi...inatangaza hivyo wakati ht huko msd kwenyewe gloves...na vifaa vingine hakuna au umesahau kuwa msd inaiadai serikali mabilioni...vifaa havipo....jua tu ni uzushi...km unajipenda mkeo mfungashie kila kitu aende nacho...uhai kitu kingine
 
Chamsingi kwa afya yako na mtoto hakikisha unavifaa vyote na hela kidogo ya rushwa. hii ni sera ya serikali yako sikizu ambayo kwa bahati mbaya sana wewe unaisikiliza na kuiamini. Ungekua gamba shemeji angepelekwa Apolo India ndio iliko siptali ya CCM. Hii Mt Meru ni yetu sisi CHADEMA
 
serkali inakwambia mjamzito atibiwe bure lakini vifaa kama glovez.pamba dawa na vitu vingine haivisupply kwenye hizo hosp unategemea nesi amzalishe mkeo mikono mitupu bila gloves ndo mana anamucha manesi na wafanyakazi wote wa afya wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana ni mungu pekee ndie atakae walipa
 
best toa tafadhali ili uhudumiwe maana ww ndo mwenye uchungu na mwenye shida
hilo si mount meru peke ake ni TZ nzima gvt hosp.ziko hvyoo
ukijitia jeuri itakula kwako tena mie sisy wangu alikodishiwa ambulance elf 40 tulitoa wenyewe alikua anapelekwa hosp.ya mkoa DSM
yaani na vifa wajawazito wananyanyasika mno hasa ukiwa karibu kujifungua unaona bora liende tu
na km utaenda bila vifaa wanakuhudumia ila hutoki mpk uwalipe pesa yao
 
Hii ni shida ya muda mrefu sasa, due to isufficient and unequal distribution of resources katika hospitali na vituo vya afya,

always mgonjwa au mteja wa huduma ya afya anakuwa victimised.

Hii ndiyo serikali ya CCM tuliyoipa mamlaka ya kututawala tangu tupate Uhuru.
 
Back
Top Bottom