Hospitali ya mkoa Mbeya,hayazungumziki!

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Ikiwa ni baada ya miezi miwili kupita tangu mgomo wa madaktari uliopelekea kutekwa,kuteswa na kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande.Hali bado siyo shwari katika hospitali nyingi nchini..! Leo nimetembelea hospitali ya mkoa Mbeya kumwona mdogo wangu anaesoma Ivumwe Sekondari aliyeugua ghafla | |Kwa mujibu wa Matron aliyefanikisha kumfikisha mdogo wangu hospitalini hapo amelalamikia kusuasua kwa huduma kwani tangu walipofika saa 10:07 asubuhi hawajahudumiwa hadi saa saba.Ukifika hospitalini-reception utakutana na kundi la watu wanaosubiri huduma,kwa upande mwingine utakutana na watu wasiopungua 100 wakisubiri kuwaona madaktari. Kwa mujibu wa Nesi mmoja amedokeza kuwa hali ya utoaji tiba siyo nzuri,dawa zimebaki kidogo sana kiasi kwamba uongozi umeamua kuhalalisha kuwaandikia dawa wagonjwa ili wakajinunulie. Miundombinu siyo nzuri kwani hakuna hata nyenzo za kubebea wagonjwa from A to B...Kimsingi huduma ni mbovu kiasi cha kutozungumzika.
 
Kaka/Baba/dada ulidhani kweli huduma zitaboreshwa sekta ya afya kwa ujumla wake na kwa kiwango kikubwa huwa inaendeshwa kwa fedha za wafadhili,wafadhili wamemnyondea Jakaya hawampendi wanaona anahatarisha vitega uchumi vyao kwa kuendesha siasa mbovu za kiuchumi na kulea umaskini wa kufuru nchini
 
"mkuu tunaoumia ni sie masikini,serikali imetutupa wagonjwa haijali kabisa,wiki iliyopita kuna ndg yetu kapata ajali ya pikipiki uyole ya kati muda wa saa kumi jioni aliumia mguu na mkono kidogo ilipofika saa mbili uck alikatwa mguu bila sabbu ya msingi.wengi wanafanyiwa hivi but serikali haioni yote haya"
 
Pipitamu said:
"mkuu tunaoumia ni sie masikini,serikali imetutupa wagonjwa haijali kabisa,wiki iliyopita kuna ndg yetu kapata ajali ya pikipiki uyole ya kati muda wa saa kumi jioni aliumia mguu na mkono kidogo ilipofika saa mbili uck alikatwa mguu bila sabbu ya msingi.wengi wanafanyiwa hivi but serikali haioni yote haya".....ama kweli hawataacha kwenda kutibiwa ulaya,inasikitisha kusikia ufisadi kila corner huku hata pulling chair kwa ajili ya kuwapeleka wagonjwa wanaoshindwa kutembea hamna.Bado haitoshi,hakuna huduma nzuri ya chakula karibu na eneo la hospitali.Kinachonichukiza zaidi,mgomo wa madaktari uliibua mengi na ulimalizwa kimizengwe,kwa nini watendaji wa serikali hawajifunzi?
 
mkuu Gandagumu, nilidhani kuna jingine, kumbe hilo?.. Hilo/hayo kawaida sana tu mkuu..labda kipindi kile cha mgomo, ungetambua hali halisi iliyopo usingeshangaa madaktari walikuwa wanadai nini!!

Na wengi hawajui hali halisi ya hospitali zetu ndi maana tulipinga.

Anyway, POLE sana kwa kuuguza mkuu.
 
"mkuu tunaoumia ni sie masikini,serikali imetutupa wagonjwa haijali kabisa,wiki iliyopita kuna ndg yetu kapata ajali ya pikipiki uyole ya kati muda wa saa kumi jioni aliumia mguu na mkono kidogo ilipofika saa mbili uck alikatwa mguu bila sabbu ya msingi.wengi wanafanyiwa hivi but serikali haioni yote haya"

kama aliumia kwa kiasi cha ku tear popliteal artery beyond repair, there is no way you can salvage the lower limb. Hiyo bila sababu ina walakini kidogo, unless uwe ni medical personel ambaye uliona uwezekano wa kuunga upo. Otherwise, mambo hospitalini siyo mazuri kabisaaa. Serikali yenyewe inaendeshwa bora liende, unadhani watawajali nyie? Mlichagua boga mkidhani mnachagua dhahabu.
 
Heri hiyo, Mwananyamala ni nouma wanauza mpaka marehemu.
 
kama hatukijifunza kwa migomo dhahiri ya madaktari sasa tutajifunza kwa migomo baridi.subiri waziri akatwe mguu ndio tutaona huduma za afya zikiboreshwa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Back
Top Bottom