wengiwengi
Member
- Jun 13, 2014
- 30
- 23
Nina mgonjwa wangu nilimpeleka pale hospitali ya kairuki juzi saa 6 mchana, alikua anaumwa sana sanaa lakini cha kushangaza wao walivyompokea walimwekea drip tu na wakasema wamechukua vipimo na hakuna kingine kilichofanyika juu ya mgonjwa wangu zaid ya kumpa kitanda alale asubirie kesho yake madaktari waje ndio watoe majib ya vipimo. Nikajiuliza kuanzia sa 6 mchana nilimpofikisha hawajaweza hata kumwambia unaumwa maleria anza na dozi hii au kunywa dawa hizi wao ni wanasema hadi kesho sasa kama akizidiwa usiku itakuaje??? Na huu utaratibu wa kusubiri had kesho kwa wagonjwa walio serious si hatari kwa uhai wa wagonjwa???? Hii hospitali nayo ichunguzwe, yawezekana ikawa inasabibisha vifo visvyo vya lazima kwa kuchelewesha kuhudumia wagonjwa.