Princemwalejr
JF-Expert Member
- Nov 9, 2017
- 496
- 492
Usafiri wa kwenda hospitali ni kitu muhimu sana na wakati mwingine ni dharura.
Wenzetu wana mabarabara yanayowezesha magari ya wagonjwa kusafiri kwa haraka. Na bado hospitali zao zina mahelikopta ya kuwahisha wagonjwa hospitali bila ya kukwama kwenye misongamano ya magari.
Mbali na hayo hospitali zao zina matawi. Utakuta hospitali moja ndani ya mkoa mmoja ina matawi kama manne hivi ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi.
Ngoma iko kwetu. Hatuna barabara nzuri wala leni za dharura barabarani. Hatuna helikopta na hospitali inayotegemewa inakuwa moja tu kwa mikoa iliyojaaliwa kuwa na hospitali kubwa. Hivi kweli ukilazimika kupelekwa Muhimbili kutokea Tandika ndani ya saa moja utafika?
Kuepuka tatizo hili wenzetu hospitali zao zina matawi yenye uwezo sawa wa kutoa huduma za afya.
Nazungumzia Muhimbili iwe na matawi Kinondoni na Temeka na kila tawi utakaloenda mapigo ni yale yale. Dokta dokta kweli, X Ray na MRI ni X Ray na MRI. Hivyo ndivyo wanavyokwenda wenzetu.
Ubishi usiokuwa na tija ruksa!