Hospitali hoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali hoi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 9, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Madaktari wakwepa kutoa huduma
  [​IMG] Wagonjwa wakimbia, maafa yaja
  [​IMG] Kikwete kuzungumza na wazee leo  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete


  Wakati hali ya huduma katika hospitali kuu nchini ikizidi kudorora kufuatia mgomo usio na ukomo uliotangazwa na madaktari nchini kote juzi, huku wagonjwa wakizikimbia hospitali hizo, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam leo, ingawa ajenda kuu haijajulikana.

  Habari za ukakika kutoka ndani ya serikali, zinasema uamuzi wa Rais Kikwete kuzungumza na wazee unaelezwa kuchukuliwa ili kueleza umma juu ya undani wa madai ya madaktari, ikiwa ni juhudi za kutaka kuuzima mgomo wao ambao tayari umekwisha kuathiri utoaji wa huduma katika hospitali kubwa za umma nchini.

  Kadhalika, vyanzo vyetu vimesema kuwa jana Rais aliitisha Baraza la Usalama la Taifa na kuna habari kwamba suala la mgomo wa madaktari ni miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa kwa kirefu na mkutano wa leo na wazee ni njia ya kuwasilisha kwa umma msimamo wa serikali juu ya mgomo na madai ya madaktari.

  Hali ikitarajiwa kubadilika leo kutokana na mkutano wa Rais na wazee ambao ni staili ambayo imekuwa ikitumiwa na marais waliotangulia na hata Rais Kikwete mwenyewe, jawabu la ama kujiuzulu kwa Mawaziri, Dk. Haji Mponda wa Wizara ya Afya na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya, litapatikana.

  Madakatari wameshikilia msimamo wa kujiuzulu kwa viongozi hao wakuu wa wizara kwanza ndipo mazungumzo na serikali yaendelee kwa kile wanachodai wamekuwa chanzo cha kuzorota kwa huduma za afya nchini.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, juzi aliwajibu madaktari hao akisema kuwa madai ya kutaka mawaziri hao wajiuzulu hayawezekani, na kusisitiza kwamba hata kwa Rais pendekezo hilo haliwezi kupelekwa.

  Mkutano wa Rais na wazee ukisubiriwa leo kutegua kitendawili cha mgomo, utoaji wa huduma za afya, jana uliendelea kuzorota katika hospitali mbalimbali nchini, kufuatia madaktari kuanza kugoma, ikiwa ni awamu ya pili ya mgomo wao, ambao safari hii wanashinikiza kujiuzulu au kufukuzwa kazi kwa Waziri Mponda na Naibu wake, Dk. Nkya.

  VITANDA VYABAKI VITUPU

  Kutokana na hali hiyo, vitanda vya baadhi ya hospitali vilishuhudiwa vikiwa vitupu baada ya ndugu kulazimika kuwahamisha wagonjwa wao waliokuwa wamelazwa katika hospitali hizo na kuwapeleka katika hospitali binafsi au kuwarudisha nyumbani.

  NIPASHE jana ilishuhudia mgonjwa Edna Kameta akihamishwa na ndugu zake katika wodi ya Mwaisela ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kupelekwa katika Hospitali ya binafsi ya Regency.

  “Tumeamua kumhamisha mgonjwa wetu kwa kukosa huduma. Tumeamua kumhamishia katika Hospitali ya Regency,” alisema Maro Chacha ambaye ni ndugu ya Edna.

  MABENCHI YABAKI MATUPU

  Pia viti (mabenchi) vilivyotengwa kwa ajili ya kutumiwa na ndugu pamoja na wagonjwa kusubiri kupatiwa huduma katika hospitali hizo, vilishuhudiwa vikiwa vitupu kutokana na mgomo huo.

  Hali ilikuwa ni hivyo pia katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, ambako mgomo huo unaonekana kuwa mkali zaidi kulinganisha na hospitali nyingine za umma zilizoko jijini Dar es Salaam.

  WAGONJWA WAKATA TAMAA

  Wagonjwa wapya na wale wanaoendelea na matibabu katika hospitali hizo, baadhi walishuhudiwa wakiwa wodini na wengine nje ya hospitali wakiwa na nyuso zinazoonyesha kukata tamaa.

  Hali hiyo inatokana na baadhi ya wagonjwa kupata huduma hafifu kutoka kwa baadhi ya wahudumu wa hospitali pamoja na wauguzi waliojitolea kujaribu kuziba pengo la madaktari waliogoma na wengine kukosa kabisa huduma hizo.

  MSEMAJI MNH HAONEKANI

  Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Algaesha, hakupatikana jana ofisini kwake ili kuzungumzia hali hiyo.

  Waandishi wa habari walifika mara kadhaa ofisini kwake, lakini mara zote hizo walikuta ikiwa imefungwa, na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi, hadi tunakwenda mitamboni ilikuwa imezimwa.

  TEMEKE WAOMBA MSAADA KUOKOA JAHAZI

  Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Dk. Zaituni Mgaza, alithibitisha kuwapo mgomo wa madaktari katika hospitali yake.

  Alisema hospitali hiyo ina jumla ya madaktari 111 na kwamba wote wako kwenye mgomo, isipokuwa madaktari wawili tu walioko kwenye mafunzo ya vitendo na madaktari bingwa, ambao hakutaja idadi yao.

  “Ni kweli mgomo wa madaktari upo. Ila tunajaribu kutafuta njia za kuziba pengo lao. Kuna hatua tunachukua. Tumewaita madaktari kutoka Manispaa,” alisema Dk. Mgaza.

  Hata hivyo, alisema hadi jana mchana, madaktari hao kutoka manispaa walikuwa hawajafika hospitalini hapo na kwamba walikuwa wakiendelea kuwafuatilia katika vituo waliko.

  AMANA HUDUMA ZASUASUA

  Katika Hospitali ya Amana, huduma ziliendelea kutolewa, lakini kwa kusuasua.  Maeneo yaliyoshuhudiwa huduma hizo zikitolewa, ni pamoja na kwenye wodi ya wazazi, huku baadhi ya ndugu wakilalamikia kudorora kwa huduma katika wodi ya watoto.


  Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Meshack Shimwela, alikataa kuzungumzia hali halisi iliyoko katika hospitali yake, badala yake aliwataka waandishi wa habari kufika kujionea wenyewe kwa macho yao.

  HUDUMA MOI ZASITISHWA

  Wakati hayo yakitokea katika hospitali hizo, huduma katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) zimesitishwa kutokana na upungufu wa madaktari katika taasisi hiyo.  Baadhi ya wagonjwa waliokwenda kupata huduma ya kliniki katika taasisi hiyo walikuwa wakiishia kupangiwa tarehe nyingine ya kwenda kupata huduma hiyo.


  Kwa mujibu wa ofisa Uhusiano wa MOI, Almas Jumaa, huduma za Kliniki za nje (OPD) zimesimamishwa kwa muda kutokana na mgomo huo.
  Jumaa alisema madaktari katika taasisi hiyo, ni wachache ambao wanalazimika kuhudumia kitengo cha dharura.
  Alisema hadi jana kulikuwa na madaktari 10 badala ya 70 ambao wanatakiwa kuwapo kwa ajili ya huduma za kliniki.
  Baadhi ya wagonjwa walikuwa wakilalamika kukosa huduma ya kliniki.
  Mwanaheri Mwinyi ambaye ni mzazi aliyempeleka mwanaye, Issa Shehe, alifanyiwa upasuaji wa kichwa Oktoba, mwaka jana, alisema alipangiwa tarehe ya kurudi jana kwa mtoto wake kufanyiwa uchunguzi, lakini hakupata huduma, badala yake aliambiwa kuwa madaktari hawapo na arudi baada ya mgomo kumalizika.

  MBEYA: WIZARA YAWABANA

  Menejimenti ya Hospitali ya Rufaa Mbeya imedai kuwa imeagizwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupeleka orodha na idadi ya madaktari wanaoendelea na kazi ili kuwabaini wale ambao wanashiriki mgomo ulioanza jana katika hospitali za serikali nchini kote.

  Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk. Omary Salehe, alisema jana kuwa wizara imetoa agizo hilo baada ya madaktari kuanza mgomo wao juzi kushinikiza, Dk. Mponda na Dk. Nkya kujiuzulu au kufukuzwa kazi.

  Alisema ametakiwa na wizara kupeleka majina ya madaktari wanaoendelea na kazi na wale waliogoma, kila siku katika kipindi chote ambacho madaktari wataendelea na mgomo wao.

  Hata hivyo, Dk. Salehe alisema baadhi ya madaktari ambao juzi walishiriki mgomo katika hospitali hiyo, jana waliripoti kazini na kuendelea kuwahudumia wagonjwa kama kawaida.

  Alisema kufuatia hali hiyo, analazimika kupita kila idara hospitalini hapo kuangalia hali ya utoaji wa huduma na kuhesabu idadi ya madaktari waliopo kwa nia ya kuwabaini wale ambao wanaendelea na mgomo ili kutekeleza agizo la wizara.

  “Hapa tunasubiri kikao cha menejimenti. Tutakachokifanya mchana huu na baadaye nitapitia kila idara kuangalia madaktari wanaoendelea na mgomo, kwa sababu baadhi ya wale waliokuwa kwenye mgomo jana (juzi) leo nimewaona kwa macho yangu wakiendelea na kazi,” alisema Dk. Salehe.

  Jumla ya madaktari 75 walio katika mafunzo ya vitendo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya jana waliripotiwa kugoma na kusababisha hali ya utoaji wa huduma katika hospitali hiyo kuwa tete.

  MADAKTARI BINGWA BUGANDO WAGOMA

  Madaktari bingwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza jana walianza mgomo. NIPASHE ilikuwapo Bugando kuanzia saa saba mchana hadi saa tisa alasiri na kushuhudia mgomo huo.
  Pia, ilishuhudia baadhi ya wagonjwa wakirejea majumbani kwa shingo upande, huku wengine wakiendelea kusubiri iwapo madaktari wangelegeza msimamo wao na kurejea kazini kama kawaida.
  Daktari mmoja aliyezungumza na NIPASHE kwa sharti la kutokutajwa jina, alisema: “Siyo suala la mishahara tu, hata vitendea kazi ni tatizo katika hospitali zetu. Kwa mfano, kipimo cha TC Scan katika hospitali ya Rufaa Bugando ni kibovu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Sasa utafanyaje kazi katika mazingira kama hayo wakati viongozi wetu wa ngazi za juu serikalini wakiendelea kula kuku kwa mrija?”
  Alisema kipimo cha X –Ray katika hospitali hiyo ni kibovu kwa zaidi ya wiki moja sasa. “Kwa nini hao watu wawili tusiowataka wasijiuzulu? Wao wana nini? Kwa nini asiwabadilishe wizara kama anawataka badala ya kuleta madhara na maafa kwa taifa?” alihoji.
  Mkurugenzi wa Hospitali, Dk. Charles Majinge, hakupatikana ili kuzungumzia suala hilo. Ilidaiwa kuwa alikuwa kwenye kikao ingawa hata hivyo, simu yake ya mkononi haikuwa hewani.

  BOMBO WAGOMA
  Madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Rufaa mkoani Tanga, (Bombo) wamefanya mgomo baridi kwa kurandaranda wodini bila ya kujishughulisha na kutoa huduma kwa wagonjwa.
  “Mgomo huu umeanza leo (jana) kwa sababu jana (juzi) nilipata huduma hapa, lakini leo (jana) kila daktari yupo mbio na majukumu yake wala hatuangaliwi,” alisema mmoja wa wagonjwa aliyekutwa mapokezi.
  Wananchi waliokwenda kupata matibabu hospitalini hapo, walisema mgomo huo ni janga na kwamba licha ya kuleta usumbufu kwa wagonjwa, pia unatishia maisha ya wananchi wa hali ya chini.
  Pia wagonjwa waliokuwa wodini walilalamikia madaktari kutoonekana wodini.
  Kadhalika, ndugu wa wagonjwa waliolazwa wamelalamika kuwa licha ya wagonjwa wao kutopatiwa huduma, shughuli nyingine zimekuwa zikiendelea, ikiwamo michango ya vitanda na dawa.
  Jonathan Bahweje alisema kitendo cha serikali kushindwa kutatua mgomo wa madaktari kinatokana na vigogo kutotibiwa katika hospitali za nchini.
  Abdallah Kubo alilalamika kukosa matibabu baada ya kupata ajali juzi usiku na kufikishwa hospitalini hapo saa 5 usiku na kwamba hadi jana asubuhi hakuwa amepata matibabu wala kuonana na daktari.
  Rose Mwaimu alisema alifika asubuhi jana kuonana na daktari katika kitengo cha mazoezi ya viungo, lakini hakukupata msaada wowote baada ya kuelezwa kwamba madaktari hawafanyi kazi.
  Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Fred Mtatifikolo, hakupatikana baada ya mwandishi kufika ofisini kwake na kuelezwa kwamba yupo kwenye shughuli maalum na hawezi kupatikana.
  IRINGA MGOMO BARIDI
  Mgomo huo umeziathiri baadhi ya hospitali za Mkoa wa Iringa kutokana na madaktari wake kufanya mgomo baridi, hali iliyowafanya wagonjwa kulalamikia utoaji wa huduma za kusuasua, licha ya madaktari na wauguzi kuwapo kazini kama kawaida.
  Idadi kubwa ya wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Hospitali ya Wilaya ya Njombe (Kibena) na Kituo Kikuu cha Afya Makambako, jana walisimama katika foleni kwa muda mrefu, huku wakilalamika.
  “Ndugu yangu hali unayoiona ndiyo hii na hatujui huu ndio mgomo wao unavyokuwa au ni uhaba wa madaktari. Tumekaa hapa kwa muda mrefu, lakini huduma zinatolewa kwa kusuasua sana,” alisema Deo Mlimwila, mkazi wa Kata ya Ubena, Mamlaka ya Mji mdogo wa Makambako.
  Celina Anderson ambaye ni mkazi wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa, alisema hali iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ni tete kutokana na mgomo baridi unaoendelea na kusababisha huduma kuchelewa kutolewa.
  ”Mambo hapa sio mambo na tunavyoona ni kama vile huo mgomo upo, ila hatuna cha kufanya zaidi ya kuwa wavumilivu ili tupate huduma. Mara tunasikia kuna madaktari wamehamishwa kikazi, tunajiuliza kwani wakihama watu hawafanyi kazi?” alihoji.
  MADAKTARI 33 DODOMA WAGOMA
  Madaktari 33 walio katika mafunzo kwa vitendo wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wameendelea na mgomo baridi huku wengine wakiendelea kutoa huduma.
  Jana asubuhi NIPASHE ilishuhudia baadhi ya wagonjwa ambao walifika mapokezi kwa ajili ya huduma, lakini hawakuhudumiwa kwa wakati mwafaka.
  NIPASHE ilishuhudia eneo hilo la mapokezi likiwa limefurika wagonjwa huku kukiwa na madaktari wazoefu wawili ambao walikuwa wakitoa huduma huku wakuu wa idara mbalimbali wakiwa kwenye kikao cha dharura.
  Msemaji wa madaktari wa mafunzo kwa vitendo, Dk. Kassim Mkuwa, alisema walikutana jana asubuhi na madaktari wenzake kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu na kuwa wameafikiana kugoma hadi hapo madai yao ya msingi yatakaposikilizwa.
  “Tutagoma hadi hapo madai yetu ya msingi yatakaposikiliza…na wale wote wanaosema kuwa hapa hakuna mgomo si kweli mgomo upo na hautaisha hadi hapo madai yetu yatakaposikilizwa.
  “Napenda kuwaambia kuwa sisi tumegoma tangu juzi na wala hatukufanya kazi yoyote ile,” alisema.  KCMC MGOMO BARIDI
  Utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Mjini Moshi, unaendelea kwa mtindo wa mgomo baridi.
  Madaktari wapo kwenye vikao vya mara kwa mara ili kufanya maamuzi sahihi juu ya uamuzi wa kuanza mgomo huo.
  Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa madaktari ambaye si msemaji, kwa sasa viongozi wa madaktari hao wapo kwenye vikao, ili kutoka na uamuzi wa kuanza mgomo rasmi bila kuwaathiri wagonjwa wala wao wenyewe.
  “Kwa muda mrefu tangu jana tupo kwenye vikao. Tunajadiliana kwa kina juu ya nini cha kufanya. Utendaji kazi kwa sasa haupo kwa asilimia 100, kwani madaktari wengi hawapo wodini. Ila tunachotaka kufanya ni kuepuka mikwaruzo kama ilivyotokea kwenye mgomo wa awali,” alisema.
  Taarifa kutoka kwa mmoja wa wagonjwa aliyelazwa katika wodi za watoto, zilisema hali ya utoaji wa huduma si ya kuridhisha.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dk. Moshi Ntabaye, jana hakupatikana kwani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokewa.

  SERIKALI KIMYA
  Msemaji Ofisi ya Waziri Mkuu, David Kirway, alipoulizwa jana na NIPASHE kuhusu hatua zinazochukuliwa na ofisi hiyo kuhusiana na mgomo huo, alisema kufikia jana mchana, alikuwa hajapata taarifa zozote kutoka kwa bosi wake.
  Alisema taarifa zilizopo ni zile zile zilizotolewa na Waziri Mkuu Pinda, katika mahojiano na waandishi wa habari, Ikulu, jijini Dar es Salaam juzi kwamba, serikali inajipanga kukabiliana na mgomo huo.
  MADAKTARI: MGOMO PALEPALE, KUTOA TAMKO LEO
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, alisema madaktari wanaendelea na msimamo wao wa kugoma mpaka hapo serikali itakapotekeleza madai yao.

  Alisema jana walikuwa na vikao vyao vya ndani na kwamba wanawasubiri wawakilishi wao wa mikoani kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo kuhusiana na sakata hilo.

  Dk. Ulimboka alisema leo watatoa tamko baada ya kikao chao kumalizika na yatakuwa ni maazimio ya madaktari wote.

  Hata hivyo, alisema madaktari hawakuwa tayari kufikia hatua hiyo na kusisitiza hali hiyo imesababishwa na serikali kutokuwa sikivu.
  Imeandikwa na Muhibu Said, Sharifa Marira, Jimy Mfuru, Gwamaka Alipipi na Beatrice Shayo, Dar; Godfrey Mushi, Iringa; Dege Masoli, Tanga; Salome Kitomari, Moshi; Emmanuel Lengwa, Mbeya; Juma Ngh’oko, Mwanza; Jacqueline Massano na Ibrahim Joseph, Dodoma.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Ma Daktari nakuombeni rudini Ma hospitalini wagonjwa wanamalizika kwa kufa ehhh jamani kuweni na roho za huruma.......
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 19. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Du!! Kaaz kwelkwel
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Chama cha madaktari kimezindua kitengo cha propaganda?
   
Loading...