Hospitali anayotibiwa Lissu yasema haijapokea pesa kutoka bungeni

mnyawusi

Senior Member
Apr 1, 2012
169
254
Hospital ya Nairobi hawajapokea fedha za Bunge 43Millions hadi muda huu, hivyo taarifa ya Bunge ni feki iliyotengenezwa kisiasa ili kuzima upepo wa aibu kwa CCM na Serikali yake.

Hospitali ya Nairobi alikolazwa Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha wanasheria nchini Tundu Lissu imesema haijapokea fedha zozote kutoka bunge la Tanzania hadi kufikia jana saa 10 jioni.

Mkuu wa mahusiano ya umma wa KHA inayomiliki hospitali hiyo Bi.Catherine Njoroge ameiambia televisheni ya K24 kwamba hadi kufikia jana malipo hayo yalikuwa hayajafika kwenye akaunti yao.

Catherine alieleza hayo baada ya kuhojiwa na mtangazaji wa K24 aliyetaka kujua kama wamepokea malipo hayo ya TZS 43Milioni sawa na Shilingi 2.1Milioni za Kenya, baada ya bunge la Tanzania kueleza kuwa limefanya malipo hayo tangu jumatano ya tarehe 20 mwezi huu.

"Akaunti iliyotajwa kwenye taarifa ya bunge la Tanzania ni sahihi, lakini bado fedha hizo hazijafika. Kama walituma kwa TT (Telegraphic Transfer) muamala huchukua hadi saa 48 kukamilika. Hivyo kama kweli walituma tunategemea kufikia jumatatu fedha hizo zitakua zimeonekana kwenye akaunti". Ameeleza Catherine akiwa Nairobi Hospital.

Chanzo:K24 TV ya Kenya.
 
Maana watenda mabaya wataharibiwa, Bali wamngojao Bwana ndio watakaoirithi nchi.

For evildoers shall be cut off: but those that wait upon the LORD, they shall inherit the earth.

Zaburi 37:9
 
watakuwa wamefanya malipo jana haraka haraka mara baada ya press ya Mbowe ili waweze kujibu mashambulizi ndio maana hawakuweka copy ya deposit slip kwani ingeonyesha tarehe ya malipo au risiti ya wire transfer wakiogopa tarehe kwani malipo yanachukua 24 to 48 hrs kuonekana kwy account ndio maana acount ya hospt haijapokea malipo.

integrity ni kitu kizuri sana ukikosa basi utadanyanga hata kwy vitu visivyo na msingi badala ya kukubali makosa. viongozi wetu wengi hawana integrity bahati mbaya
 
Back
Top Bottom