HOPE IN CIVICS (URAIA NA IMANI)

HOPE IN CIVICS (URAIA NA IMANI)

Amba Samedi

Senior Member
Joined
Apr 5, 2024
Posts
193
Reaction score
326
Katika masomo ya uraia (civics), tunafundishwa kuhusu haki, wajibu, na nafasi ya kila mmoja wetu katika jamii. Lakini leo nataka tuuangalie upande wa pili, upande wa ndani yaani uraia wa nafsi yako.

Kama ambavyo raia ana haki ya kusikilizwa, na wewe una haki ya kusikiliza sauti ya moyo wako. Kuna wimbo ndani yako haujaimbwa. Kuna nuru ndani yako bado inang’aa, hata kama kwa sasa inaonekana kama cheche ndogo.

Umechoka, lakini hujamalizika.
Umejeruhiwa, lakini bado unatembea.
Umelia, lakini bado una sauti ya kusema ‘naamini’.

Yesu alisema “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Mathayo 11:28

Simama tena. Songesha hatua zako hata kama ni ndogo. Dunia inakuhitaji. Ndiyo, hata wewe unaetembea huku umebeba mzigo wa huzuni bado una nafasi ya kubadilisha historia.

Wimbo Ulio Bora Media
 
Back
Top Bottom