Hongereni wanasiasa kuongea kiingereza kibovu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
52,003
Kiingereza kina matawi na lafudhi nyingi na matamshi tofauti tofauti.Waingereza wenyewe wanasisitiza kuwa cha muhimu ni kueleweka ulitaka kusema nini

Mfano kwenye kiswahili Mswahili wa pwani akimsikiliza mchaga akiongea kiswahili anatamani kucheka maana kiswahili chake si fasaha anaongea utafikiri kameza chura aliye hai mdomoni anapoongea.Cha muhimu mtu wa Pwani anachofanya ni kumvumilia kumwelewa hasa anataka kusema nini.

Kiingereza kiko toifauti tofauti.Mhindi akikuongelesha kingereza una kazi ya kuelewa.KINGEREZA KIKO CHA uk,IRELAND,america na kuna kiingereza kile cha BLACK AMERICANS ni aibu tupu kiko hovyo hovyo lakini kinakubalika katika jamii ya waongea kiingereza kuwa ni kiingereza kama ambavyo kiswahili kibovu cha wahindi,wakenya na wakongo kinavyokubalika kwenye jamii ya waongea kiswahili

Kwa mwanasiasa yeyote hana haja ya kuogopa kuongea broken english.Cha muhimu aeleweke alitaka kusema nini

Wazungu wengi huwa wanawashangaa mno watanzania kuona kuwa wanajua kiingereza.Sababu kwa watanzania wengi kiingereza ni lugha ya tatu.Mfano mchaga akizaliwa anatakiwa kujua lugha ya kichaga hadi aimudu barabara,akitoka hapo anaingia kujifunza kiswahili hadi akimudu barabara,halafu baada ya hapo aingie lugha ya tatu ya kiingereza aijue.Wanashangaa.Hivyo mtu lugha ya Tatu akiongea broken kumzomea si sahihi inabidi apongezwe

Kumbuka waingereza na wamarekani wakizaliwa lugha ni kiingereza tu sasa utawalinganisha na mtu anayetakiwa kuijua kama Lugha ya tatu? Wazungu wengi wanasema mtu kumudu lugha tatu ni kitu cha ajabu

Wote mnaoongea broken English hongereni endeleeni kuongea hata umoja wa mataifa.

Mzungu akija nchini akiongea kiswahili kibovu watu wanapiga makofi mswahili akiongea kiingereza kibovu eti waswahili wanamzomea.Kuna waswahili nadhani wana mapepo hasa wanaozomea mswahili akiongea kiingereza kibovu.
 
hahaaaaaaaaa,lumumba bhana mnafurahisha.Usijali ,wakuelewa tuliposoma heading tu tulijua lengo la huu uzi ni kumkingia kifua mh mtumbua majipu.Sawa,tunajua kiingereza kinampiga chenga ila hatujalalama.Kinachotusikitisha ni kufichwa kwa matukio wakati mheshimiwa akitema yai,yaani TBC wakaficha kabisa.Wangetuonesha tu
 
Tuliosoma shule ya msingi miaka ya nyuma tunakumbuka kwamba masomo yote ya shule ya msingi yalikuwa yanafundishwa kwa kiswahili kasoro somo moja la kingereza. Ukienda sekondari unakuta masomo yote yanafundishwa kwa kingereza kasoro somo moja la kiswahili. Hapa unachanganya na ukweli kwamba huyo huyo mwanafunzi anayekua akilazimika kuzijua hizo lugha mbili, akienda kijijini kwao wajomba na mashangazi zake wanamcheka kwa sababu haifahamu lugha yake ya asili!!. Kichwa hicho hicho kimoja kizifahamu lugha tatu, tena kwa ufasaha.

Kilicho muhimu ni substance ya mtu, uwezo wa mtu kuzalisha na sio mbwembwe za kuongea lugha za kigeni. Kule Russia mrusi wala haoni aibu kutojua kingereza, profesa wa chuo anayekufundisha anajua hesabu utadhani kazitunga yeye, lakini akianza kuongea kingereza unaanza kusikia zis iz na zat waz nyingi sana. Na wasomi ambao wamefundishwa na maprofesa hao wa kirusi ndio hawa kina Profesa Makame Mbarawa na wasomi wengi tu ambao wamefanya mengi ndani ya serikali na katika taasisi nyingi za binafsi.

Tuache utumwa wa mawazo kwa kukiona kingereza kama vile ni lugha ya malaika wa mbinguni. Tukifahamu kingereza lakini kisitufanye tukajidharau, sisi na asili yetu.
 
Kama hujaenda shule basi muulize hata ndg yako kuwa mtu anapo defend Thesis Yake tena ktk level ya PhD huwa anatumia lugha gani??? Mind you Mhe. Rais ana PhD ya Mathematics.

Queen Esther

Nimeipenda hii!!
 
Siku Rais Obama alipokuja TZ Kulikuwa kuna muda Mhe. Rais wangu mstaafu JK alitoa speech.

Waswahili mkaizungusha hiyo speech mkionesha kasoro kwenye kila sentensi aliyoongea.

Badala ya kujadili content mkawa buzy kujadili lugha na jinsi alivyo ongea kingereza cha kuvunjika vunjika!!!

WaTZ acheni ujinga!!!

Queen Esther

Kiingereza kina matawi na lafudhi nyingi na matamshi tofauti tofauti.Waingereza wenyewe wanasisitiza kuwa cha muhimu ni kueleweka ulitaka kusema nini

Mfano kwenye kiswahili Mswahili wa pwani akimsikiliza mchaga akiongea kiswahili anatamani kucheka maana kiswahili chake si fasaha anaongea utafikiri kameza chura aliye hai mdomoni anapoongea.Cha muhimu mtu wa Pwani anachofanya ni kumvumilia kumwelewa hasa anataka kusema nini.

Kiingereza kiko toifauti tofauti.Mhindi akikuongelesha kingereza una kazi ya kuelewa.KINGEREZA KIKO CHA uk,IRELAND,america na kuna kiingereza kile cha BLACK AMERICANS ni aibu tupu kiko hovyo hovyo lakini kinakubalika katika jamii ya waongea kiingereza kuwa ni kiingereza kama ambavyo kiswahili kibovu cha wahindi,wakenya na wakongo kinavyokubalika kwenye jamii ya waongea kiswahili

Kwa mwanasiasa yeyote hana haja ya kuogopa kuongea broken english.Cha muhimu aeleweke alitaka kusema nini

Wazungu wengi huwa wanawashangaa mno watanzania kuona kuwa wanajua kiingereza.Sababu kwa watanzania wengi kiingereza ni lugha ya tatu.Mfano mchaga akizaliwa anatakiwa kujua lugha ya kichaga hadi aimudu barabara,akitoka hapo anaingia kujifunza kiswahili hadi akimudu barabara,halafu baada ya hapo aingie lugha ya tatu ya kiingereza aijue.Wanashangaa.Hivyo mtu lugha ya Tatu akiongea broken kumzomea si sahihi inabidi apongezwe

Kumbuka waingereza na wamarekani wakizaliwa lugha ni kiingereza tu sasa utawalinganisha na mtu anayetakiwa kuijua kama Lugha ya tatu? Wazungu wengi wanasema mtu kumudu lugha tatu ni kitu cha ajabu

Wote mnaoongea broken English hongereni endeleeni kuongea hata umoja wa mataifa.

Mzungu akija nchini akiongea kiswahili kibovu watu wanapiga makofi mswahili akiongea kiingereza kibovu eti waswahili wanamzomea.Kuna waswahili nadhani wana mapepo hasa wanaozomea mswahili akiongea kiingereza kibovu.
ais
 
Siku Rais Obama alipokuja TZ Kulikuwa kuna muda Mhe. Rais wangu mstaafu JK alitoa speech.

Waswahili mkaizungusha hiyo speech mkionesha kasoro kwenye kila sentensi aliyoongea.

Badala ya kujadili content mkawa buzy kujadili lugha na jinsi alivyo ongea kingereza cha kuvunjika vunjika!!!

WaTZ acheni ujinga!!!

Queen Esther

ais
Queen Esther wakoloni wameondoka miaka 55 iliyopita lakini mabaki yao bado yapo, ndio hawa wanaodhani ni sifa kujitambulisha kwa ukaribu na wale waliotutawala. Rais wa China huwezi kumsikia akiongea kingereza, lakini wamarekani kila wakisikia neno China, usingizi wote unawatoka vichwani mwao.
 
Tuliosoma shule ya msingi miaka ya nyuma tunakumbuka kwamba masomo yote ya shule ya msingi yalikuwa yanafundishwa kwa kiswahili kasoro somo moja la kingereza. Ukienda sekondari unakuta masomo yote yanafundishwa kwa kingereza kasoro somo moja la kiswahili. Hapa unachanganya na ukweli kwamba huyo huyo mwanafunzi anayekua akilazimika kuzijua hizo lugha mbili, akienda kijijini kwao wajomba na mashangazi zake wanamcheka kwa sababu haifahamu lugha yake ya asili!!. Kichwa hicho hicho kimoja kizifahamu lugha tatu, tena kwa ufasaha.

Kilicho muhimu ni substance ya mtu, uwezo wa mtu kuzalisha na sio mbwembwe za kuongea lugha za kigeni. Kule Russia mrusi wala haoni aibu kutojua kingereza, profesa wa chuo anayekufundisha anajua hesabu utadhani kazitunga yeye, lakini akianza kuongea kingereza unaanza kusikia zis iz na zat waz nyingi sana. Na wasomi ambao wamefundishwa na maprofesa hao wa kirusi ndio hawa kina Profesa Makame Mbarawa na wasomi wengi tu ambao wamefanya mengi ndani ya serikali na katika taasisi nyingi za binafsi.

Tuache utumwa wa mawazo kwa kukiona kingereza kama vile ni lugha ya malaika wa mbinguni. Tukifahamu kingereza lakini kisitufanye tukajidharau, sisi na asili yetu.
Ndygu uko sahihi kabisa, kuna prof kutoka Russia hapa chuoni kwetu kiingereza kwake ni shida lakini anapga madude ya kemia c mchezo. Hata wahindi pia tunao wengi sana na wako vizur sana.sema watanzania ulimbukeni mwingi mno na kukosa hoja za msingi za kuzijadili.huwa sielewi inakuaje mtu anaanzisha mada mbovu kiasi hiki kati kuna utitiri wa mada ambazo ni productive katika jamii,

Waafrika kweli inahitajika kutawaliwa tena hadi hivi vichwa vyetu vizinduke.
 
Ni kweli ndg yangu. Halafu hao waongeaji na wakosoaji ukisoma English yao humu JF unaweza kulia, sasa sijui ya kuongea maana Kama hujui kuandika English iliyonyooka ina maana kuongea ni balaa. Watu ni WANAFIKI sana.

Queen Esther

Queen Esther wakoloni wameondoka miaka 55 iliyopita lakini mabaki yao bado yapo, ndio hawa wanaodhani ni sifa kujitambulisha kwa ukaribu na wale waliotutawala. Rais wa China huwezi kumsikia akiongea kingereza, lakini wamarekani kila wakisikia neno China, usingizi wote unawatoka vichwani mwao.
 
Kama hujaenda shule basi muulize hata ndg yako kuwa mtu anapo defend Thesis Yake tena ktk level ya PhD huwa anatumia lugha gani??? Mind you Mhe. Rais ana PhD ya Mathematics.

Queen Esther

we elewa kiingereza cha Rais wetu kibovu,hakuna haja ya kukwepesha maneno.Pia anajua kinyamwezi ila ni kibovu pia.
Mtu unaweza ukawa huijui vizuri lugha ya kiingereza ila ukapresent kitu kwa technical language ya field husika na ukafanikiwa.mf Engineer anapofanya presentation ya field yake,most part ni tecnical language inayotumika.Lakini the same person ukamwambia azungumzie social issue kwa dakika 3 unaweza kuta anaongea kiingereza kibovu zaidi.Nimeshuhudia hayo mara nyingi tu.Ndio sawa na mh kama unavyosema,kudefend thesis ya field yako sio kazi,wataalamu wanaangalia content basi.Hata mmarekani unampiga gap as long as una content hata kama kiingereza cha kuungaunga.
tunachosema ni kuwa,Rais ana kiingereza kibovu,huo ndio ukweli mbaya zaidi hili linafichwa ndio maana watu wanaliongelea.TBC hawakufanya vizuri kuficha
 
Kwakuwa Ni Mh. Wako Unayemuabudu Kama Mungu Wako!!! NDIYE Anayechemka Kutema "NGERI " Hadi Kufikia Kuwakimbia Wageni Wake!!! LEO Umekuwa Mdogo Kama Choroko Vile!!! MWAMBIENI Kuna RAS SIMBA, Anapiga Msasa Vichwa Vitupu!!!!! SASA UDAKTARI Upi, Ambao Hauendani Na "UNG'ENG'E"!!!?? AU Labda DKT Wa KISWAHILI!!!!!??? MLETA UZI Huu Mwenyewe, Hata KISWAHILI HAKIJUI!!!! MF. Ni Pale Anapotumia "HALAFU " Badala Ya "ALAFU " SASA Kama Ni Hivyo BORA Mh. ATUMIE Hiyo LUGHA Yake Ya Kwanza Tu!!!
 
Hapa hata mkwepeshe vipi, ni jambo la ajabu MTU (huu ni mfano tuu) asome O &A level miaka 6 kwa kiingereza, kisha asome Diploma ya ualimu miaka 2 kwa lugha hiyohiyo, atumie miaka michache kufundisha sekondari kwa lugha hiyohiyo kisha degree ya kwanza miaka 3 lugha hiyo hiyo, Masters miaka 2 tena lugha hiyo hiyo kisha PhD bado lugha hiyo hiyo na miaka kama ishirini katika kazi ambayo inamkutanisha na watu wengi sana wa ndani na nje wanaiongea
lugha hiyohiyo ya Kiingereza. Kisha tuambiwe eti lugha hiyo inampa shida. Nina hakika basi kuna tatizo hapo.
Nina hakika hata mpwa wangu Elli ukimfundisha masomo miaka yote hiyo kwa Kisandawe atakuwa ana tiririka lugha ya kisandawe mfano hakuna.
Hapa nadhani kuna MTU anasingiziwa tuu. Hata hivyo sio lazima kuijua lugha hiyo ila cha ajabu kama miaka yote hiyo unaisoma huielewi jee hayo ukiyosoma ulikuwa unaelewa kweli au ulikuwa una kariri?
 
Back
Top Bottom