Elections 2010 Hongereni wana Rombo kwa kummwaga Mramba

Notburga Alphonce Maskini: Ipo siku nitakuwa mbunge wa Rombo Send to a friend Saturday, 11 September 2010 15:22 0diggsdigg

masikini.jpg
Notburga Alphonce Maskin

•Alishika nafasi ya pili, nyuma ya Basil Mramba
Na Joyce Mmasi
NOTBRUGA Alphonce Maskini, ni jina geni katika ulimwengu wa siasa, lakini kwa wale wanaofuatilia mwenendo wa utumishi wa umma katika Serikali za Mitaa na harakati za wafanyakazi, sio geni kutokana na umahiri wake wa kutumikia, kusimamia, kutetea na kupigania haki za wananchi na wafanyakazi.Pamoja na kudumu katika utumishi wa umma kwa muda wote, Notburga Maskini aliamua kuchepuka na kujiingiza katika siasa ambapo alijitokeza kugombea ubunge katika jimbo la Rombo.
Mama huyu sio mwanasiasa, lakini anatoka katika familia ya kisiasa, kwani ni mtoto wa mbunge wa kwanza wa jimbo la Rombo, Mzee Alphonce Maskini, na pia muda mwingi wa utumishi amekuwa akifanya kazi na wanasiasa.
Jimbo la Rombo ni miongoni mwa majimbo magumu kisiasa, kutokana na kuwa chini ya mbunge mkongwe Basil Mramba ambaye inaelezwa kuwa anakubalika na kuheshimika na wananchi wa jimbo hilo.
Hata hivyo; kukubalika kwa Mramba hakikuwa kikwazo kilichoweza kumzuia Maskini kujitokeza kwa ujasiri na kueleza waziwazi na kwa umahiri mkubwa nia yake kwa wananchi wa Rombo.
Hivi karibuni nilipata fursa ya kufanya mazungumzo na Notburga Maskini ambapo swali langu la kwanza nilitaka kujua kwanini aliamua kujitosa katika siasa, na hasa kugombea ubunge katika jimbo hilo?
“Kwanza niliamua kujiingiza katika siasa kwa kuwa mimi ni kiongozi, nimesimamia maendeleo na huduma kwa umma katika maeneo mbalimbali kwa uadilifu na mapenzi makubwa hapa nchini na kujenga uwezo wa kuongoza.
Pia kutokana na mapenzi na ukaribu wangu na wananchi wa Rombo kwa maana ya kuwatembelea mara kwa mara ninapokuwa likizo, nayajua matatizo ya Rombo na naamini ninaweza kuwa kiongozi na mwakilishi mzuri zaidi wa wananchi wa Rombo na Watanzania endapo ningepata fursa ya kuingia Bungeni.
Kutokana na uzoefu niliojenga kwa muda mrefu nikisimamia maendeleo ya wananchi wakiwemo wanawake ambao ni idadi kubwa zaidi najisikia mwenye deni kubwa kwa kutotumia ujuzi na uzoefu wangu kubadilisha hali iliyopo sasa. Hata hivyo najisikia mwenye faraja kubwa kwa kuwa nilitimiza azma yangu kwa kujitokeza na kuonesha wazi nia hiyo endapo ningepata ridhaa ya kuwaongoza” anasema.

Maskini ambaye amekuwa mtumishi katika sekta mbalimbali katika Serikali, Serikali za Mitaa na kiongozi wa wafanyakazi kwa muda mrefu, pia ndiye Makamu mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA).
Anasema amekuwa mtumishi wa umma na kiongozi wa wafanyakazi kwa muda mrefu na kutokana na kufanya vizuri kazi zake alipendekezwa na wafanyakazi mwaka 2005 kusogea hatua moja kwenye siasa katika kiti maalum cha wafanyakazi.
Kura hazikutosha na kama kawaida alishika nafasi ya pili kwa Mama Sita lakini kutokana na uzoefu aliopata katika zoezi hilo aliamua kugombea jimbo la Rombo mahali alipozaliwa, ambapo anasema anaamini alihitajika zaidi.
“Rombo ni nyumbani, na matatizo ya Rombo si tofauti sana na niliyoyaona huko nilikotumikia. Nilitamani kurudi nyumbani sasa, baada ya kutumikia watanzania maeneo mengine kwa miaka mingi, hivyo niliona ni vyema nigombee ubunge nyumbani ili niwasaidie na watu wa huko ambao nayajua matatizo yao” anasema.
Anasema sababu ingine iliyomsukuma kugombea ubunge Rombo ni kutokana na kutakiwa afanye hivyo na wazee ambao walikuwa wakishirikiana kwa ukaribu na wazazi wake ambao walikuwa na mapenzi makubwa na wananchi wa Rombo.
“Wazazi wangu walikuwa karibu sana na watu wa Rombo, na mimi nimekuwa karibu sana na wazazi wangu ambao wamekuwa wakinihimiza kupenda watu na kujitoa zaidi kuwatumikia kwa uadilifu na kwa hali na mali.
Anasema kwa kutambua msimamo wa wazazi wake, ameweza kuwatumikia Watanzania katika nafasi mbalimbali kama mtumishi wa umma katika Wizara, taasisi na wilaya kadhaa hapa nchini. Kwa kutambua kuwa matatizo ya wananchi wa Tanzania hayatofautiani sana, amekuwa akijitolea kuchangia katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika maeneo aliyokuwa anatumikia na Rombo japokuwa amekuwa akiishi nje ya jimbo hilo kwa muda mrefu.
Anasema kutokana na ukaribu wake na michango yake ya hali na mali aliyokuwa akiitoa kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo, baadhi ya wananchi wa huko walimtaka ajitokeze na yeye aliona mantiki hiyo na walimuunga mkono kwa kiwango kikubwa sana.
Anasema, licha ya kutopata ushindi kutokana na mazingira magumu ya Rombo kwa sasa, anaamini kura alizopata ni ishara ya ushindi na kuwa anakubalika kwa kiasi kikubwa nyumbani alikozaliwa licha ya kutokuwa mkaazi wa huko.
Mama Notburga Maskini, alijitosa kugombea ubunge katika jimbo la Rombo kupitia chama cha Mapinduzi na kushika nafasi ya pili, alipata kura 3,563 huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na mbunge aliyemaliza muda wake, Basil Mramba, ambaye alipata kura 8300.
Je nini malengo yake katika siasa, baada ya kukosa nafasi ya uwakilishi wa wananchi wa Rombo, anasema, “Ninayo matumaini makubwa, kama nilivyokwambia mimi ni kiongozi, nitaendelea na harakati zangu na kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu, naamini iko siku nitapata kile nilichokusudia” anasema
Anasema Rombo kuna matatizo mengi lakini kubwa ni umaskini, uharibifu wa mazingira, huduma duni za elimu, maji na afya ndio yaliyomsukuma kujitosa kutaka kulishughulikia hasa vifo vya wanawake wakati wa kujifungua na watoto ambao hufariki kabla ya kutimiza miaka mitano.
Anasema huduma za afya bado ni duni na hata hizo zilizopo haziwafikii wananchi wengi. Ningefarijika sana iwapo ningepata fursa ya kushiriki katika kupunguza tatizo la vifo vya kina mama na watoto ili kufikia 2015 tuweze kulifuta katika nchi yetu.
Akizungumzia harakati zake katika shirikisho la wafanyakazi Bi Maskini anasema, “Kwanza niweke wazi kuwa, licha ya kuwa kiongozi katika shirikisho, sikuingia katika shirikisho kama mwanaharakati, isipokuwa nilichaguliwa kuwa kiongozi wa wafanyakazi kutokana na msimamo wangu juu ya haki na huduma nzuri kwa watumishi kwa mujibu wa sheria zilizopo, kuhudumia umma kwa uadilifu na kujali utu” popote nilipotumikia. Nimejikuta kila ninapokutana na wateja wangu aidha watumishi au wananchi niliowatumikia wananikubali sana anasema.
Anasema kutokana na sifa yake ya kiongozi, alijikuta akiingia katika nafasi mbalimbali za uongozi katika maeneo mbalimbali na hatimaye kufikia hatua ya kuwa makamu mwenyekiti wa shirikisho hilo la wafanyakazi nchini.
“Kila niliofanya nao kazi mara nyingi walinipenda na ilipotokea nafasi yoyote ya uongozi walinichagua hata pale nilipokuwa sikugombea, naamini hii ilitokana na ukaribu wangu na wafanyakazi pamoja na tabia yangu ya kutetea wanyonge, kusimamia sheria kwa haki na kulinda haki za wafanyakazi niliofanya nao kazi” anasema
Anasema, licha ya kutokuwa mwanaharakati, alipoingia katika shirikisho hilo, amejikuta akifanya kazi zake lengo likiwa kusimamia haki za wafanyakazi wote tofauti na zamani alipokuwa akisimamia wafanyakazi wa eneo alilokuwa akifanyia kazi.
Notburga Maskini, ambaye anafuata nyayo za Baba yake mzazi, ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo la Rombo, Mzee Alphonce Maskini, alizaliwa katika Kijiji cha Kingachi, Useri, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, Mwaka 1958 na kupata elimu ya msingi wilayani Rombo na Dar es Salaam, na baadaye kujiunga na elimu ya Sekondari Jijini Dar es Salaam. Baada ya elimu ya Sekondari alijiunga na Chuo cha elimu ya Biashara Shycom mkoani Shinyanga.

Alipata shahada ya kwanza ya uongozi wa Umma katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na baadaye kupata shahada ya uzamili ya uongozi wa biashara (utumishi wa umma) katika chuo kikuu cha Birmingham huko Uingereza. Aidha amepata vyeti vya usimamizi wa Rasilmali watu na kutoka Chuo Kikuu cha Connecticut nchini Marekani na Chuo Kikuu cha Bradaford nchini Uingereza.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments




0 #7 jongoo 2010-10-03 14:26 huyo MTUHUMIWA Mramba Kapania kwelikweli ama zake ama zetu nasikia mpinzani wake wa chadema kapata ajali kutokana na vitimbwi na vitisho yeye anawaambia wapiga kura wamwombee asirudi kulikoniiiii? Si majuzi tu aliulizwa kuwa kesi yake akishindwa akifungwa itakuwaje akajibu "kwani ukiwa na mgonjwa ICU unaomba apone au unaomba afe? Kwa nini awiwaeleze wananchi wamwombee apone haraka? hata kama ni Mgombea mwenza wake Joseph Selasini? Ama kweli siasa zetu TZ ni mcheazo mchafu usiojali hata uhai ili mradi mtu ashinde. Sijasikia hadi sasa kama kamtumia salaam za pole!! Warombo kuweni macho na unafiki huu uliojaa ubinafsi na chuki.
Quote









#6 Geza Ulole 2010-09-16 05:27 Quoting Hubert Fred:
Baada ya kusoma maelelezo ya huyu mama Masikini ni kweli ni mtumishi mzuri lakini swala kwamba eti watu walitoka Arusha na Moshi mjini kupiga kura hivi huyu Mr Olesiringoti hajui kwamba Warombo wengi wenye mapenzi mema na Rombo wanaishi Arusha, Moshi mjini na Dar.na ndio wachangiaji wakubwa kwa maendeleo ya Rombo. Kati ya watu hao ni wafanyabiashara na wasomi wa hali ya juu.Rombo tutafanya makosa sana kama hatutahakikisha kwamba Mramba anashinda kwa Kishindo. Mendeleleo Rombo tunayaona na ni kazi ya Mramba pamoja na wale Warombo waishio nje ya Rombo. Mzee Mramba kaza buti. Mama Masikini muda ukifika utafikiriwa hivyo basi naomba ushirikiane na Mramba akiwa mbunge wa Rombo mlete maendeleo 2010 - 2015.Nadhani sio kwamba ni lazima mbunge tu alete maendeleo na hata wale wenye mapenzi mema na wakazi wa Rombo kama akina Ngaleku wanaonekana wanavyosaidia na wengine wengi hivyo basi Mama Masikini naomba ufuate nyayo hizo hizo.​
wewe kweli una akili hata kama wkiwa wamegushi kadi za chama ni sawa kwako wewe kwa vile kwako wewe wana mapenzi mema na sio njama chafu!
Quote









#5 wenceslauce 2010-09-14 14:22 Kitakachoimaliz a CCM ni uchakachuaji wa kura,inakuwaje hata mnaibiana wenyewe kwa wenyewe?Ninavyojua mimi hata paka shume au mbwa koko haibi nyumbani,na ikitokea akaiba huuawa ili asiendelee kuitia kaya hasara.Kwa mambo yote yanayofanyika ndani ya chama TWAWALA nina uhakika kuna siku mawe yatapiga kelele na historia itawahukumu.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
Quote









-3 #4 Hubert Fred 2010-09-14 09:19 Baada ya kusoma maelelezo ya huyu mama Masikini ni kweli ni mtumishi mzuri lakini swala kwamba eti watu walitoka Arusha na Moshi mjini kupiga kura hivi huyu Mr Olesiringoti hajui kwamba Warombo wengi wenye mapenzi mema na Rombo wanaishi Arusha, Moshi mjini na Dar.na ndio wachangiaji wakubwa kwa maendeleo ya Rombo. Kati ya watu hao ni wafanyabiashara na wasomi wa hali ya juu.Rombo tutafanya makosa sana kama hatutahakikisha kwamba Mramba anashinda kwa Kishindo. Mendeleleo Rombo tunayaona na ni kazi ya Mramba pamoja na wale Warombo waishio nje ya Rombo. Mzee Mramba kaza buti. Mama Masikini muda ukifika utafikiriwa hivyo basi naomba ushirikiane na Mramba akiwa mbunge wa Rombo mlete maendeleo 2010 - 2015.Nadhani sio kwamba ni lazima mbunge tu alete maendeleo na hata wale wenye mapenzi mema na wakazi wa Rombo kama akina Ngaleku wanaonekana wanavyosaidia na wengine wengi hivyo basi Mama Masikini naomba ufuate nyayo hizo hizo.
Quote









+3 #3 Geza Ulole 2010-09-12 19:40 tatizo ni wafanyabiashara mafisadi wa Rombo ambao wamefaidika na wizi wa Mramba kuanzia Michael Shirima, Ernest Massawe na wengineo! CHADEMA itawaonyesha mwaka huu!
Quote









+3 #2 hamisi 2010-09-12 16:03 CCM kweli ni chama cha makapi yaani Luka mchomba baada ya kufilisika kwenye kiwanda cha mbao ameamia ccm kutafuta maslai. huyu mama baba yake aliyafanya kazi nzuri sana kwa maana bibi yangu kabla ya kufariki kila siku alikuwa akiniambia Alphonse maskini ndiye alikuwa mbunge mzuri wa Rombo.
Quote









+3 #1 Olesiringoti 2010-09-12 12:05 Huyu mama alishinda ila viongozi wa CCM Rombo na Kilimanjaro wamemdhulumu maana kuna kura 5000 ziliingizwa kinyemela na Luka Mchomba na wenzie, watu walitoka Moshi Mjini na Arusha kuja kupiga kura na kadi bandia yaani za wanachama wasiotambulika! Na kuwahakikishia tu CHADEMA watashinda hili jimbo maana wananchi wa Rombo wamesusia wizi wa CCM
Quote







Refresh comments list

MY TAKE:
Ushindi wa CHADEMA ulitabiriwa siku nyingii na wachambuzi wa mambo maana ni dhahiri maamuzi ya kikandamizi ya kura za maoni ndo yamei-cost CCM Rombo huyu mama aliibiwa ushindi kura za maoni CCM! alishinda kwa kura 4200+ dhidi ya Mramba 3300+ ila wakina Mchomba na Ngaleku wakaingiza kura 5000 na Mramba akapewa ushindi na hata baada ya malalamiko hakuna kitu kilifanywa! na hayo ndo mazao ya Ufisadi wa viongozi wa CCM Kilimanjaro... Big Up CHADEMA
 
Hongereni sana waru wa Rombo kwa kulitokomeza hilo jizi ambalo kwa mshangaoi wa Watz wengi JK alitaka lirudi mjengoni. Alilinadi jukwaani na kuwaambia wanaCCM eti ni lijitu safi linafaa! Kama vyombo vyetu vya dola vinavyomilikiwa na CCM vinashindwa kumhukumu, basi angalau wananchi wenye kuipenda nchi yao wamemhukumu.

Asanteni sana, wakati mnapiga kura mimi nilikuwa ndani ya myoyo yenu. Nina Sh 100,000/- nataka niwaleteeni kama zawadi kwa kazi hiyo lakini sijui nifanye vipi ziwafikie nyote mlioshiriki kulikomboa taifa kwa kulibwaga fisadi hilo.
 
Hongereni sana waru wa Rombo kwa kulitokomeza hilo jizi ambalo kwa mshangaoi wa Watz wengi JK alitaka lirudi mjengoni. Alilinadi jukwaani na kuwaambia wanaCCM eti ni lijitu safi linafaa! Kama vyombo vyetu vya dola vinavyomilikiwa na CCM vinashindwa kumhukumu, basi angalau wananchi wenye kuipenda nchi yao wamemhukumu.

Asanteni sana, wakati mnapiga kura mimi nilikuwa ndani ya myoyo yenu. Nina Sh 100,000/- nataka niwaleteeni kama zawadi kwa kazi hiyo lakini sijui nifanye vipi ziwafikie nyote mlioshiriki kulikomboa taifa kwa kulibwaga fisadi hilo.
changia yatima Rombo ingia Ngaleku.com kuna maelezo ya jinsi ya ku-deposit hela hizo
 
Hongereni sana waru wa Rombo kwa kulitokomeza hilo jizi ambalo kwa mshangaoi wa Watz wengi JK alitaka lirudi mjengoni. Alilinadi jukwaani na kuwaambia wanaCCM eti ni lijitu safi linafaa! Kama vyombo vyetu vya dola vinavyomilikiwa na CCM vinashindwa kumhukumu, basi angalau wananchi wenye kuipenda nchi yao wamemhukumu.

Asanteni sana, wakati mnapiga kura mimi nilikuwa ndani ya myoyo yenu. Nina Sh 100,000/- nataka niwaleteeni kama zawadi kwa kazi hiyo lakini sijui nifanye vipi ziwafikie nyote mlioshiriki kulikomboa taifa kwa kulibwaga fisadi hilo.


Sh 100,000/- gawanya kwa wapiga kura 29,566 kila mmoja atapata sh. 3.38.
 
Ni jambo jema watz hatuwezi kuendelea kuongozwa na wezi wa mali ya umma, wao wananeemeka na familia zao then sisi tuanataabika kutopata huduma bora za kijamii.

Najua wengine watashinda kama lowassa, aziz, jk lakini ipo siku yao watajibu mbele ya wananchi, maana kila wafanyacho/waamuacho rekodi zitakuwepo, haijalishi itachukua muda gani au miongo mingapi lakini lazima watawajibishwa siku ikifika.
 
Hivi Yona aligombea au yuko Segerea? Kama yuko Segerea amuandalie Mramba kitanda
 
"Huyu ndiye Mramba......mmemuonaaa?.....ni msafi,.....mchapakaziiii..."

Guess ni maneno ya nani hayo??
 
"Huyu ndiye Mramba......mmemuonaaa?.....ni msafi,.....mchapakaziiii..."

Guess ni maneno ya nani hayo??

i know! I know! ni DR Jk makofi tafadhali.

Na huyo mramba ajifunze hata nani akusafishe na kukusifia kama unanuka unanuka tu. POWER TO THE PEOPLE
 
Mtukanaji na fisadi wa watanzania hatumtaki jengoni, yaani wewe unatuambia hata tukila manyasi ndege ya raisi itanunuliwa, halafu unaidhinisha ununuzi wa ndege mbovu, Are you ok upstairs? Kwisha habari yako bora wanarombo wameamka na kuamua kukupindua kwa kupitia ballot box, weraaaaaaaaaaaaa weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
JK bwana, mweupe (hamnazo) mpaka unaskia mwili unawasha.... eti anasema walimruhusu mramba kwa sababu yeye anashutumiwa tu, na haijaamuliwa kuwa alifanya ufisadi ule. Kwani mwakalebela walikua wamethibitisha? Ndo mnategemea ajue kwanin tz ni maskini? We unamshtaki mtu af unarudi kumtetea hana hatia mpaka majirani wakuthibitishie ndo mwivi?
 
huyu si ndio yule fisadi alietuambia kwa kejeli kuwa sisi watanzania tule nyasi ili wanunue ndege ya rais? malipo ya uovu ni hapahapa!
 
Back
Top Bottom