Hongereni Wana-Jangwani kwa Ubingwa Msimu 2021/22. Hakika Mlistahili.

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Tulikuwa na kazi kubwa sana ya kuwatafuta mbadala wa akina Juma Abdul, Kelvin Yondani na mwenzake Nadir Haroub. Tukapata Job, Kibwana na Mwamnyeto

Kazi nyingine ilikuwa kupata kiungo bora kabisa wa upishi kuzidi wakina Chuji na Domayo. Tukapata Feisal.


Kazi hiyo imekamilika.

Historia inasema:-
Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania wakiwa na wachezaji wazawa wasiopungua watano 5 kwenye first 11 yake, basi hudumu kwenye mataji mfululizo kwa kipindi cha misimu isiyopungua 5 pasi na kuyumba.

Sasa tuko Tayari kurudi kwenye reli ya kuendelea Kukwapua Makombe ya kwenye Ligi Mpaka waseme po.

Mabingwa wana kikosi chenye wachezaji walio na wastani wa umri wa miaka 23. Yaani ikimaanisha wana takribani miaka 7 ya kucheza soka pamoja.

Wale Makolo FC wana kikosi chenye wastani wa umri wa miaka 30. Yaani wamebakiza miezi 4 tu kuendelea kuwa katika ubora wao.

Msimu huu umedhihirisha wazi kuwa umri wa kikosi chao umekuwa tatizo la kuwakosesha Ubingwa wa msimu 2021/22.

Msimu ujao yaani 2022/23 watajaribu kureplace idadi kubwa ya wachezaji wao. Wakiwa katika hiyo process, wanajangwani watakuwa wakiendelea kutoa dozi kwakuwa wako na chemistry tangi msimu wa nyuma.

Kitakacho tokea Wanajangwani watatawazwa kuwa mabingwa tena wa msimu 2022/23.

Msimu keshokutwa ndio watakuwa katika nafasi bora ya kiushindani, lakini hawatakuwa kwenye ubora kuzidi Yanga SC kwasababu wachezaji wengi vIjana watakuwa katika peak yao.

Ninaona misimu mitatu 3 myepesi kwa wanajangwani.


Hongereni wanajagwani.
 
Back
Top Bottom