Hongereni Wakurya kwa hili

Hongereni Wakurya kwa hili

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,121
Reaction score
1,981
Kumekuwepo na dhana dhidi ya jamii ya wakurya kuwa ni wakatili lakini nawapongeza wakurya kwa hili

Wakurya ni kabila ambalo watu wake hawawezi kuulizana DNA ya watoto tofauti na makabila mengine

Mwanaume wa kikurya hana muda wa kuchunguza mtoto kazaliwa na nani au ana fanana na nani,yeye huamini kitanda hakizai haramu

Mwanaume wa kikurya anaweza kuoa mwanamke aliye na watoto zaidi ya wanne na akawatunza kama wanae na akawabadilisha majina wakaitwa majina ya ukoo wake,na ukoo ukawatambua hao watoto kama ndugu zao,na watoto waliokuja na mama watapewa urdhi,kuhudumiwa kama vile matibabu,elimu, na kuozwa au kuoa kwa gharama za mwanaume bila ubaguzi wowote

Ndio maana ni nadra sana kukuta watoto wa kikurya ni mahouse girl, au watoto wa mitaani, wakurya wanadhamini watu wao sana.


Wakurya huwa wanadhamini sana watoto,awe amemzaa,au hajamzaa,ila anahesabika ni mtoto wake

Ndio maana siku hizi wanawake wa makabila mengine wanatamani waolewe na wakurya,maana wamechoka watoto wao kuchunguzwa mara kwa mara wazaliwapo na wanaume waliozaa nao

Nimeshuhudia wanawake wawili wenye asili ya mkoa wa Tabora,wakitafuta waolewe na mwanaume wa kikurya kisa hawana complication kwenye ndoa zao

Kama wewe ni mwanamke una mtoto unasita kuolewa kisa mwanao ataenda kunyanyasika,tafuta mkurya,mwanao ataishi vizuri sana,na atahudumiwa kama watoto wengine
 
Wanaobagua watoto wengi wao wamechoka kimaisha,mimi kwetu aliletwa dada wa kulelewa(adopted). Majirani mpaka jamaa wote walikuwa wanampenda watu wengi walikuwa wanamwita kwa kabila letu. Watu wengi walijua alikuwa biological daughter ila kakulia kwengine. Na alikuwa anapendwa sawa na sisi au naweza sema yeye akipendwa zaidi
 
Ni Kweli wakurya hawana complication wanachotaka wanaume nikuheshimiwa tu, mwanamke asiwe juu ya mwanaume ,mwanamke akionekana anamzidi mwanaume kuongea au kutoa maamzi mwanaume huoa mwanamke wa pili
 
Ni Kweli wakurya hawana complication wanachotaka wanaume nikuheshimiwa tu, mwanamke asiwe juu ya mwanaume ,mwanamke akionekana anamzidi mwanaume kuongea au kutoa maamzi mwanaume huoa mwanamke wa pili
Fact
 
kwetu kuoa ni kuongeza mapato. Mwanamuke atalima mwenyewe, awe na chakula cha kumtosheleza na watoto wake. Akienda kuzaa, najua wake wenzie ndo watakwenda mpeleka na kumrudisha hospitali. Jinsi ninavyoongeza wanawake ndio naheshimika hadi kijijini. Ng'ombe za mahari napata kwa wake zangu. Sijui ka kuna kabila zuri ka mkurya wa ching'ombe.
 
Wakurya!! Wanangu, dadazangu au wanawake wote wanaonihusu wakiolewa na wakurya tu ni mwisho wa mahusiano yetu!!.
Haya madude sijui kwanni MUNGU aliyaumba! Yalitakiwa yazaliwe huko kwenye familia za simba yakazane kutulia nyumbu zetu
 
Back
Top Bottom