Uchaguzi 2020 Hongereni Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Trinity

JF-Expert Member
Jul 20, 2017
1,706
3,212
Habari ya Jumapili mabibi na mabwana, niende moja kwa moja kwenye kichwa cha habari!

Kwanza nashukuru Mungu kwa uhai kwangu kwako pia mpaka unasoma ujumbe huu naamini upo vzr, pia niwape pole kwa wenye changamoto za kiafya.

Mimi Ni raia wa kawaida kabisa, ukweli wagombea wote Wana sababu ya kuchaguliwa na kutokuchaguliwa lakini kutokana na sera zao maamuzi yako binafsi Ni muhimu zaidi.

Sijaona sababu ya tume kulaumiwa kabla na baada ya uchaguzi kwani hawa jamaa wemeweka mfumo ulio wazi na haki.

Kwanza kabisa mawakala wa vyama vyote wapo ambao wanawakilisha kuona namna ya upigaji kura unavyoenda, idadi ya kura zitakazobandikwa, zilizotumwa Kama zinaendana na hesabu aliyoipata mgombea kwa kila kituo halafu mwisho jumla ya kura zote kijimbo mpaka kitaifa.

Kwa sababu hiyo sioni watu KULINDA kura baada ya kupiga, KUGOMEA matokea.

Tusione tunaonewa kiasi hicho, Mara kwa mara nimesikia baadhi ya wagombea wakihamasisha kulinda kura na kugomea matokea.

No.! No! Tubadilike waungwa na tutoe elimu kwa wasiofahamu mtaani kwetu, hakuna sababu ya kupigana mabomu, risasi na uharibifu wa aina yoyote ile.

Big up tume ya uchaguzi Tz kwa kuwa huru na haki!

Mungu ibariki Tz!
 
Wewe hupaswi kumshukuru mungu kwa kukuweka hai kwani vigezo vyako vyote vya kuwatetea NECCCM Tumeccm na Polisiccm vyombo binafsi vya CCM ni haramu na vya kishetani, hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu anaiamini wala kuipenda NECCCM Tumeccm hata siku moja kwani wameonyesha udhaifu mkubwa kipindi cha kampeni kwa kuingilia kampeni za vyama utazani nao wanagombea ubunge na Urais.

Na kibaya kupita vyote ni NECCCM Tumeccm kuwapitisha wabunge wa CCM kienyeji kwa njia haramu za kishetani kuwa wamepita bila kupingwa wakati wamepigwa lakini rufaa za wapinzani zikatupwa na NECCCM Tumeccm kwa njia za hovyo kwa visingizio visivyo na Tija
 
Hongera NEC, moaka hivi sasa mmeifanya kazi yenu kwa weledi na uzalendo. Msiwasikilize chadema hawajawahi kuiongelea mazuri nchi wala taasisi zake.
 
Nchi ina miaka 59 hakuna maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, kama siyo CCM mda huu Tanzania ingekuwa ni Nchi tajiri kuliko mataifa yote mikubwa Duniani na pengine ingekuwa na kura ya veto, chini ya CCM Nchi imefirisika pesa nyingi zinatumika kwa mambo ya hovyo yasiyo na tija kwa Taifa ikiwemo kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani uonevu unyanyasaji uovu mateso ya kila aina,

Hawataki maendeleo na hata huto tumaendeleo kiduchu twa SGR bwawa la umeme flyover ununuzi wa Ndege ni 10% zao na kuna ufisadi mkubwa na tenda nyingi ni kampuni zao wenyewe na pindi wakilipwa pesa inazunguka inamrudia kaburu Mkoloni mweusi kwa njia moja au nyingine, CCM ni ile ile ukoo wa panya baba mama mtoto wote ni wezi
 
Kuna kikundi kidogo cha wajinga ambao wapo tayari kudangwa kwa siasa za maji taka mfano wakati mh.Rais Magufuli akisisitiza kuwa WE ARE IN THE RIGHT TRUCK wao wakasema hawajui JPM analipeleka wapi taifa.

Baada ya muda mfupi tu Tanzania ikatangazwa imeingia kwenye uchumi wa kati wao wakaona wanalitiaje doa jambo hili wakaja na kauli ya maendeleo ni ya watu na sio vitu.

Safi kabisa na mie nawaunga mkono lakini je, waliotoa takwimu hiyo ya kuwa sasa Tanzania ipo uchumi wa kati waliangalia barabara, ndege, fly overs au waliangalia kipato cha mwananchi mmoja mmoja kwa mwaka mzima anaingiza ngapi?

Na kama waliangalia kipato cha mwananchi mmoja mmoja je,tunamaendeleo ya vitu au pamoja na watu? Lisu anasikilizwa na wahuni tu wafuata upepo.

Na ndio maana kila siku nasema kama akifikisha kura 1.5m nipigwe ban miezi sita.

MAGUFULI4LIFE.
 
Hongera NEC, moaka hivi sasa mmeifanya kazi yenu kwa weledi na uzalendo. Msiwasikilize chadema hawajawahi kuiongelea mazuri nchi wala taasisi zake..
NECCCM Tumeccm ni chombo binafsi cha CCM kimefanya kazi gani nzuri?
 
Kuna kikundi kidogo cha wajinga ambao wapo tayari kudangwa kwa siasa za maji taka mfano wakati mh.Rais Magufuli akisisitiza kuwa WE ARE IN THE RIGHT TRUCK wao wakasema hawajui JPM analipeleka wapi taifa. Baada ya muda mfupi tu Tanzania ikatangazwa imeingia kwenye uchumi wa kati wao wakaona wanalitiaje doa jambo hili wakaja na kauli ya maendeleo ni ya watu na sio vitu. Safi kabisa na mie nawaunga mkono lakini je, waliotoa takwimu hiyo ya kuwa sasa Tanzania ipo uchumi wa kati waliangalia barabara, ndege, fly overs au waliangalia kipato cha mwananchi mmoja mmoja kwa mwaka mzima anaingiza ngapi? Na kama waliangalia kipato cha mwananchi mmoja mmoja je,tunamaendeleo ya vitu au pamoja na watu? Lisu anasikiliza n awahuni tu wafuata upepo.
Na ndio maana kila siku nasema kama akifikisha kura 1.5m nipigie ban miezi sita.

MAGUFULI4LIFE.
Wewe ni mnufaika wa blackmail kuwabambikia kodi TRA wafanyabiashara wakubwa na BOT kupora pesa za watu zinazotumwa tokea nje mpaka mmefanya wafanyabiashara kwenda kuweka pesa zao Uganda Zambia kenya kusiko na ujinga wenu , huwezi kujua tabu iliyopo kwa wananchi wa kawaida kwani wewe tayari umetajirika kupitia udikiteta wenu.
 
Tume ya Uchaguzi imefanya kazi kwa ueledi

Ila CHADEMA wanaogopa kushindwa ndio maana wanatoa shutuma za uwongo ili kuwadanganya wafadhili wao
NECCCM Tumeccm na Polisiccm ni vyombo binafsi vya CCM vinawezaje kufanya kazi nzuri?
 
Wewe ni mnufaika wa blackmail kuwabambikia kodi TRA wafanyabiashara wakubwa na BOT kupora pesa za watu zinazotumwa tokea nje mpaka mmefanya wafanyabiashara kwenda kuweka pesa zao Uganda Zambia kenya kusiko na ujinga wenu , huwezi kujua tabu iliyopo kwa wananchi wa kawaida kwani wewe tayari umetajirika kupitia udikiteta wenu
Nipe ushahidi hata wa mtu mmoja tu aliye bambikiwa kodi (tafadhali nakuomba sana usile kona).

MAGUFULI4LIFE.
 
No. Mjomba, haya yanatoka moyoni si kwa ushawishi wala kigezo Cha kujua kusoma na kuandika.

Fuatilia vzr mfumo wa uchaguzi hasa wa mwaka huu utajifunza kitu kizur Sana.!!

Nikikuuliza NEC imetumia vigezo na utaratibu upi kupanga majina ya vyama na wagombea kwenye karatasi ya kura unaweza kutolea ufafanuzi?
 
Back
Top Bottom