Hongereni sana Madiwani wa Halmashauri yetu ya Shinyanga

Aug 15, 2013
55
23
HONGERENI SANA MADIWANI WA HALMASHAURI YETU YA SHINYANGA

Leo asubuhi kupitia Radio Free Afrika Matukio nimesikia Madiwani wa Halmashauri yetu ya Shinyanga mmeibua mjadala wa kupanda kwa Nafaka hususan Mahindi katika maeneo yetu ya Shinyanga.

Nimemsikia Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Mboje, amesema upembuzi yakinifu ufanyike kuhusu kupanda kwa bei na kuwepo kwa njaa katika halmashauri yetu kisha mahindi yaagizwe kutoka Ghala la Chakula la Taifa.

Ushauri wangu Naomba huo upembuzi yakinifu ufanyike haraka na kwa muda mfupi ili kuokoa hali tete inayowakumba wananchi wetu.

Bila ubishi mahindi yamepanda bei sana debe 22,000/= sio lelemama kwa mwananchi ambaye hana shughuli nyingine zaidi ya kilimo na ndio Shinyanga yetu ilivyo.

Yaletwe mahindi ya Bei nafuu kupunguza huu ukali wa maisha

Narudia kutoa Pongezi kwa Madiwani wetu kwa kupaza sauti zenu na wananchi tumezisikia mmetutetea ahsanteni sana.

Wenu katika Ujenzi wa Shinyanga Mpya

Comrade Leonard Waziri
Mwakitolyo, Shinyanga.
FB_IMG_1574149715749.jpeg
 
Back
Top Bottom