Hongereni jf kwa kuungana na watz kuomboleza msiba

AJALI YA LUCKY VICENT.
1)Ni msiba wa taifa,umeukumba
Arusha.
Tena bila taarifa,kifo hakina bahasha.
Kifo hafanyiwi dhifa,kifo hakina
bashasha.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.
2)Ni huzuni kubwa sana,chozi chini
ladondoka.
Tumuombe maulana,watoto
wameondoka.
Roho zipo kwenye janna,pepo yake
msifika.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.
3)Majonzi yametawala,nchi
imetikisika.
Tufanye dua na sala,kwa mola rabi
rabuka.
Utuepushe inshaala,tusijepata garika.
Poleni wana Arusha,msiba umetupa.
4)Yupo aloita mama,baba yangu
ninakufa.
Kwa huzuni kainama,roho ikitoa nyufa.
Kifo hatazami nyuma,huja bila taarifa.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.
5)Kifo hupangwa na Mungu,kukikwepa
ni vigumu.
Japo twapata uchungu,hakuna wa
kulaumu.
Moyo umepigwa rungu,furaha
imekuwa ngumu.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.
6)Nyota zimeshazimika,ni nani
wakuziwasha.
Limefika la kufika,gari alipodondosha.
Ziraili malaika,roho ameshasifisha.
Poleni wana Arusha,msiba umetufika.
Shairi=AJALI YA LUCKY VICENT.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
AJALI YA LUCKY VICENT.
1)Ni msiba wa taifa,umeukumba
Arusha.
Tena bila taarifa,kifo hakina bahasha.
Kifo hafanyiwi dhifa,kifo hakina
bashasha.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.
2)Ni huzuni kubwa sana,chozi chini
ladondoka.
Tumuombe maulana,watoto
wameondoka.
Roho zipo kwenye janna,pepo yake
msifika.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.
3)Majonzi yametawala,nchi
imetikisika.
Tufanye dua na sala,kwa mola rabi
rabuka.
Utuepushe inshaala,tusijepata garika.
Poleni wana Arusha,msiba umetupa.
4)Yupo aloita mama,baba yangu
ninakufa.
Kwa huzuni kainama,roho ikitoa nyufa.
Kifo hatazami nyuma,huja bila taarifa.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.
5)Kifo hupangwa na Mungu,kukikwepa
ni vigumu.
Japo twapata uchungu,hakuna wa
kulaumu.
Moyo umepigwa rungu,furaha
imekuwa ngumu.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.
6)Nyota zimeshazimika,ni nani
wakuziwasha.
Limefika la kufika,gari alipodondosha.
Ziraili malaika,roho ameshasifisha.
Poleni wana Arusha,msiba umetufika.
Shairi=AJALI YA LUCKY VICENT.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Hongereni JF. inaniuma sana. japo sina ninayemjua imeniuma sana nimelia sana. Hawa ni saizi ya wajukuu zangu. Our future generation.
 
Back
Top Bottom