Hongereni akina Mama na Mabinti wa Kiislam

Hongereni akina Mama na Mabinti wa Kiislam

a hope

Senior Member
Joined
Oct 23, 2022
Posts
163
Reaction score
342
Wakuu kwema,

Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza wakina mama na wanawake wote wa kiislam kwa malezi Bora kabisa ya watoto wenu.

Kwanza kabisa mimi si wa dini hiyo, ila naomba tu niwe mkweli. Wahenga walisema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Katika suala zima la malezi ya watoto dini ya kiislam ipo vizuri mno.

Nimefanikiwa kujiari na ninajihusisha na masuala mazima ya childhood & early education na kwa siku moja ninawahudumia watoto zaidi ya mia moja.

Kwa kweli nina miaka 3 kazini. Sijawahi kupata experience mbaya na watoto wa kiislam na wengi wao wana tabia njema sana zinazofanana.

Kwanza watoto wao wako smart na nadhifu sana, asafi mno jambo linalopelekea wawe vizuri pia mentally.

Sijawahi kusikia wakitumia abusive language kwa wenzao kabisa

Upande wa christians pia na wao wako vizuri kwenye malezi lakini wakina mama wa kiislam wametuacha mbali sana kwenye upande huo. Hongera zao sana hawa wadada wa kiislam
 
Upo sahihi.

Hata kina sisi tunaofanya biashara za private hostels za wanachuo huwa hatupati changamoto za uvunjifu wa sheria kutoka kwa mabinti wa kiislam

Ngumu kukuta binti wa kiislam kagombana na mlinzi. Kutoka usiku kwenda club na kulazimisha afunguliwe geti usiku wa manane. Ila binti zetu wagalatia. Na tena akiwa mzuri ni shidaa tupu. Haoni noma hata kumleta bwana wake ampige miti ndani ya hostel
 
Ni kweli.. Kuhusu usafi hii Dini wanaongoza maana kuna miongozo ya kujiswafisha hasa akiwa ktk
Hedhi
Janaba
Haja zote ndogo na kubwa
Akijamba

Ikumbukwe hata kushikana mkono na jinsia nyingine inakuw tyr ushamtoa hali ya usafi inampasa kujiswafisha kwa kufata muongozo.
 
Ni kweli.. Kuhusu usafi hii Dini wanaongoza maana kuna miongozo ya kujiswafisha hasa akiwa ktk
Hedhi
Janaba
Haja zote ndogo na kubwa
Akijamba

Ikumbukwe hata kushikana mkono na jinsia nyingine inakuw tyr ushamtoa hali ya usafi inampasa kujiswafisha kwa kufata muongozo.
Ni kweli kabisa mkuu
 
Sio wote malezi sio dini ni utashi wa wazazi

Watoto wa masheikh wengi unakuta 'wamepinda'

Malezi ya watoto ni universal haina dini

Mtoto anafundishwa heshima, adabu, unyenyekevu, wema, upendo n.k hii inakuja automatic tu.

Kukumbushana tu kwamba ukali hausaidii katika malezi kwa kiwango kinachodhaniwa
 
Tunatakiwa wote tuwe na malezi bora kila sehemu,

Tumelelewa vizuri na sisi lazima tuwalee watoto wetu kwa maadili mema na kuwakataza mabaya na kuwafundisha mema tu

Nakumbuka tulipokuwa wadogo tulifundishwa mpaka namna ya kutembea na sio kwa kibri kwani ardhi hii hii ndio tutafukiwa nayo kwa baadhi yetu

Tumefundishwa mengi na muendelezo wa Enzi na Enzi tangu Mitume

Kwa waliofunga ongezeni fadhila mwezi huu na msaidie jamii inayowahitaji
 
Back
Top Bottom