Hongera wizara ya elimu

Hongera wizara ya elimu

East African Eagle

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
3,759
Reaction score
2,209
Nawapongeza sana wizara ya elimu kusitisha kutoa mafunzo ya certificate ya ualimu kwenye vyuo vyake kuanzia mwakani.Hii ina maana kuwa watakuwa wakitoa mafunzo ya kuanzia Diploma ya ualimu.Hivyo kuondoa uwezekano wa wale waliofeli kidato cha nne kujiunga na ualimu kwa kuwa mtu ili ajiunge na diploma inabidi awe kafaulu vizuri kidato cha nne.Hivyo ina maana kuwa kiwango cha chini cha elimu cha mwalimu wa msingi itakuwa ni diploma na sio certificate.Itasaidia kupandisha kiwango cha ufundishaji.

Pia ni tahadhari kwa walimu wenye certificate kuwa wajisomee wawe na diploma maana muda si mrefu watajikuta tu-certificate twao twa ualimu hatuna mbele wala nyuma.
 
Mapema mno kuwapongeza, cancer imeenea mwili mzima kukata kucha kutasaidia nini? Waanze kwanda kuboresha maslahi ya Waalimu, then wafanye mapinduzi makubwa kwenye mitaala ya elimu kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu... kwa hali ilivyo sasa kunahitajika kuwepo na chombo cha kusimamia ubora wa elimu ngazi zote !!! Mtihani wa mwisho siyo kigezo hata kidogo cha kumpima mtahiniwa ... Bahati mbaya sana wakubwa wa Dunia hii kwa kuwatumia vibaraka wao wanahakikisha tunaendelea kuwa na wajinga wengi watakao angamia kwa kukosa maarifa ili hatimae waendelee kukomba rasilimali zetu...
Nawapongeza sana wizara ya elimu kusitisha kutoa mafunzo ya certificate ya ualimu kwenye vyuo vyake kuanzia mwakani.Hii ina maana kuwa watakuwa wakitoa mafunzo ya kuanzia Diploma ya ualimu.Hivyo kuondoa uwezekano wa wale waliofeli kidato cha nne kujiunga na ualimu kwa kuwa mtu ili ajiunge na diploma inabidi awe kafaulu vizuri kidato cha nne.Hivyo ina maana kuwa kiwango cha chini cha elimu cha mwalimu wa msingi itakuwa ni diploma na sio certificate.Itasaidia kupandisha kiwango cha ufundishaji.

Pia ni tahadhari kwa walimu wenye certificate kuwa wajisomee wawe na diploma maana muda si mrefu watajikuta tu-certificate twao twa ualimu hatuna mbele wala nyuma.
 
bado safari ni ndefu kuna watu wanashahada na stashahada lakini hakuna cha maana wanachofanya
 
Huwenda nikakubali kupongeza.....
walimu wazamani walikuwa na elimu duni, walifundisha kwa moyo, mpaka Leo wanasifika.
Lakini wakatoa mabomu, vilaza wengi , wachumia tumbo na warafi, watu wasio fikiri kwa kichwa kama Spika Sitta na kawambwa, wezi akina Hendrew, wahuni kina captain Comba na wasira, Na waozo wengi kina dhaifu.
Elimu bora ilnabaki kuwa ya mkoloni kwani iliwajengea watu kujamini na uzalendo kwa taifa lao.
Huenda hawa wa diploma wataleta mabadiliko
 
bado safari ni ndefu kuna watu wanashahada na stashahada lakini hakuna cha maana wanachofanya

Kuna wenye PhD, Professors wengi tu lakini sioni kama hali inaashiria mafanikio mbeleni, nitaafiki hoja iliyoletwa pale tu siku nikiona watoto wa vigogo wanafundishwa na hao walimu wanaoandaliwa kwa huo mfumo mpya, tena kwenye shule za umma, vinginevyo hii yote ni mbinu nyingine ya kuliuza taifa kwa janja ya kutuvisha miwani ya mbao
 
Akina mungai wamerudi tena. diploma ya ualimu ili umfundishe darasa la ngapi? yaani mtu anaamka huko kwake ameshauriana na mke wake halafu anakuja kutangaza. huu ni uamuzi wa kitoto,nani amesema hiyo certificate ya ualimu haina maana????? nina hasira
 
Nawapongeza sana wizara ya elimu kusitisha kutoa mafunzo ya certificate ya ualimu kwenye vyuo vyake kuanzia mwakani.Hii ina maana kuwa watakuwa wakitoa mafunzo ya kuanzia Diploma ya ualimu.Hivyo kuondoa uwezekano wa wale waliofeli kidato cha nne kujiunga na ualimu kwa kuwa mtu ili ajiunge na diploma inabidi awe kafaulu vizuri kidato cha nne.Hivyo ina maana kuwa kiwango cha chini cha elimu cha mwalimu wa msingi itakuwa ni diploma na sio certificate.Itasaidia kupandisha kiwango cha ufundishaji.

Pia ni tahadhari kwa walimu wenye certificate kuwa wajisomee wawe na diploma maana muda si mrefu watajikuta tu-certificate twao twa ualimu hatuna mbele wala nyuma.

umeniudhi mno! Unaposema walimu wenye tucertificate umewakwaza sana walimu wako kwani ndo waliokufundisha na kukupa msingi ulio nao sasa. Acheni dharau kwa waliowawezesha enyi wasomi msio na elimu!
 
Akina mungai wamerudi tena. diploma ya ualimu ili umfundishe darasa la ngapi? yaani mtu anaamka huko kwake ameshauriana na mke wake halafu anakuja kutangaza. huu ni uamuzi wa kitoto,nani amesema hiyo certificate ya ualimu haina maana????? nina hasira

Taratibu ndugu yangu, kuna walimu walikuwa na certificate wamejiendeleza mpaka degree na bado wamebaki kufundisha primary school, pili OUT wanatoa diploma ya primary school muda mrefu tuu, certificate imepitwa na wakati kama tunataka kuboresha elimu yetu.
 
Nani amesema certifite imepitwa na wakati?? Ninyi ndio mnaua vyuo vya mafundi mchundo mnaweka digrii mkidhani ndio sahihi kumbe ni fikra mbovu. Walimu waliotufundisha sisi ni wazuri sana kwa ubora kuliko hawa wa sasa. Diploma 4 what?? Tafakari
 
kwani.... anaeenda chuo cha ualim anatakiwa awe na vigezo gani
 
Kuna wenye PhD, Professors wengi tu lakini sioni kama hali inaashiria mafanikio mbeleni, nitaafiki hoja iliyoletwa pale tu siku nikiona watoto wa vigogo wanafundishwa na hao walimu wanaoandaliwa kwa huo mfumo mpya, tena kwenye shule za umma, vinginevyo hii yote ni mbinu nyingine ya kuliuza taifa kwa janja ya kutuvisha miwani ya mbao

uko sawa mkuu
 
nina ndugu yangu anasoma mwaka wa kwanza certificate of education katika chuo binafsi,je atapata ajira au anapoteza muda?
 
Back
Top Bottom