Hongera Wapinzani, kwa hili mmeonyesha utu

Hongera Wapinzani, kwa hili mmeonyesha utu

Sumulenga

Member
Joined
Jul 2, 2016
Posts
60
Reaction score
36
Habari wana jamvi,

Takribani mwaka mmoja sasa tangu uchaguzi mkuu upite ambo ulikuwa na vimbwanga na vituko na kutolewa kwa kauli za ajabu na ambazo hazikuwa na staha hata kidogo.

Wagombea wengi wa Chama cha Mapinduzi walitumia lugha nyingi za matusi dhidi ya mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA na UKAWA. Hoja yao ilikuwa juu ya afya ya Mh Lowassa. Maneno na kejeli kama sio vijembe vilitolewa kwa kadri mtu alivyoona inafaa aghalabu mzee huyu alijibu majibu kuwa "afya na uzima ni mipango ya Mungu labda wenzangu wamehakikishiwa kuwa wataishi milele"

Maneno hayo hayakufua dafu kwa wanamapinduzi hawa walizidi kumsakama na kumuandama mithili ya mwizi asakwapo na mwenye Mali.

Kauli ile ya mzee huyu ilianza kujidhihirisha pale waliokuwa wanamsakama kuanza kufa na kudhihilisha kuwa afya na uzima ni mipango ya Rabuka. Ndipo wapinzani walipoanza kuwaandama hawa marehemu na kauli zao na wengineo wenye kufuata kauli walizozitoa.

Kwenye kifo cha spika wetu mstaafu Samweli Sitta naona wapinzani wameheshimu mchango wa Mheshimiwa huyu. Ndipo suala la utu la kuheshimu marehem limefuata japo na yeye alitoa kauli tata juu ya Lowasa.

Asante wapinzani endeleeni kuonyesha utu huo maana AFYA NA UZIMA NI MIPANGO YA MUNGU.
 
Ngoja nisubiri walioelewa wachangie nami nawenza kuokota kitu maana mpaka hapa sijaelewa concept ya hii habari.
 
Unawapongeza kwa vile siyo kawaida yao kukaa bila matusi na wao nadhani, rejea kinachomsotesha Lema Rumande hivi sasa
 
Unawapongeza kwa vile siyo kawaida yao kukaa bila matusi na wao nadhani, rejea kinachomsotesha Lema Rumande hivi sasa
Lakin ninachowapongeza angalau kwa sitta wamehuzunika wote pamoja richa ya sitta kumtukana kuwa lowasa ni mngonjwa hawez pona
 
Hebu tunaomba orodha ya wote waliomdhihaki binadamu mwenzao na kumtabiria kifo.
 
"Ikulu sio ICU" ...... By Late Samuel Sitta (RIP)
 
Death is for me, i have prepared my self for it, am dying in a second to come, am not worring
 
Ikulu sii ICU...nadhan ilikuwa Urambo au Mwanza
 
Ikulu sii ICU...nadhan ilikuwa Urambo au Mwanza
0c48784586e82009aa78104bc29aa9df.jpg
 
Unawapongeza kwa vile siyo kawaida yao kukaa bila matusi na wao nadhani, rejea kinachomsotesha Lema Rumande hivi sasa
wangapi walikamatwa kwenye mkutano wa july pale sisim ina kikao chao eti kumpa yule kijiti.
mbona walitukana sana????

je,wamekamatwa pamoja na kauli tata za yule
 
Unawapongeza kwa vile siyo kawaida yao kukaa bila matusi na wao nadhani, rejea kinachomsotesha Lema Rumande hivi sasa

Kinachomsotesha Lema rumande ni kwa kuwa hana madaraka huku haonyeshi nidhamu ya woga kwa watawala. Ingekuwa matusi na kejeli zinampeleka mtu rumande hao waliokuwa wanamtusi na kumkejeli huyo mgombea mamluki wa cdm wangekuwa ndani.
 
Back
Top Bottom