Hongera wanasheria Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera wanasheria Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ngambo Ngali, May 30, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tendwa apondwa kwa kutoisajili CCJ


  na David Frank, Arusha

  [​IMG] CHAMA cha Mawakili Tanzania (TLS) Mkoa wa Arusha, kimemkosoa msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa kwa kukataa kukisajili Chama Cha Jamii (CCJ) kwa madai ya kutokuwa na fedha za kuhakiki wanachama wake walioko mikoani. Mawakili hao wamemtaka Tendwa kukisajili chama hicho na vyama vingine bila ubabaishaji kwa kile walichoeleza kuwa hana sababu ya msingi ya kukataa kusajili vyama kwa madai ya kutokuwa na fedha kwani kufanya hivyo ni ukiukaji wa sheria.
  Wamesema kitendo cha msajili huyo cha kuweka visingizio kadhaa vya kukisajili chama hicho kinaweza kumtia matatizoni kwa kushtakiwa kwa kutofuata sheria kwa kuwa hakuna sheria inayomtetea kwa hilo.
  Tamko lao la Mei 28 mwaka huu lililosainiwa na Mwenyekiti wa TLS Mkoa wa Arusha, Duncan Oola, limebainisha Tendwa ana wajibu wa kusajili na kutoa hati ya usajili wa kudumu kwa chama hicho na vingine vilivyowasilisha maombi na kutimiza masharti yaliyowekwa kisheria.
  "Tunachukua fursa hii kumkumbusha msajili huyo kwamba kama cheo chake kinavyojieleza chenyewe, kazi yake ya msingi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa Sura Na. 258 (R.E. 2002) kama ilivyorekebishwa na Sheria Na 7 ya 2009 ni kusajili vyama vya siasa," inaeleza sehemu ya tamko hilo.
  Aliongeza kuwa kifungu cha 8 (5) cha sheria hiyo kinatamka wazi kwa lugha ya Kiingereza kuwa lugha iliyotumika katika kifungu hicho ni ‘shall' na siyo ‘may' kwa maana Msajili hana hiari kukubali au kukataa kusajili chama ambacho kimetimiza masharti ya kisheria ya kupewa usajili ama wa muda au wa kudumu.
  Tamko hilo liliongeza kuwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatakiwa kupokea na kushughulikia maombi ya usajili wa muda na wa kudumu wakati wote kwa kuwa sheria haijatenga kipindi maalumu cha kuwasilisha maombi ya kupewa usajili huo na kwamba sheria haijatamka muda ambao msajili anaruhusiwa kutopokea maombi ya usajili wa chama cha siasa.
  Tamko hilo lilisema kuwa msajili anawajibika kuahirisha shughuli zote ambazo si za msingi ili kushughulikia maombi ya usajili wa chama cha siasa ikiwa ni pamoja na maombi ya Chama Cha Jamii kwa kuwa ndiyo kazi yake ya msingi.
  Aidha, lilisema Tendwa anawajibika kuomba au kutafuta fedha za kumwezesha kutimiza majukumu yake ya msingi bila kutafuta visingizio kwani kutofanya hivyo ni kukwepa wajibu wake wa kisheria unaoweza kusababisha ashtakiwe kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha sheria iliyotajwa hapo juu.
  Hivi karibuni vyombo vya habari vilimnukuu msajili huyo akiwaambia viongozi wa muda wa CCJ kuwa hana fedha za kuzunguka kufanya uhakiki wa wanachama wake na kwamba kwa sasa ana majukumu mengine muhimu ya kufanya.


  Tanzania Daima.

  Nmependa sana kuona Wanasheria kwa umoja wao wakisimama kidete kukosoa pale mtumishi mmoja wa serikali anapoleta mbofumbofu kwenye kazi yake. Kituo cha sheria na haki za Binadamu, Tawla wanasheria wa mikoa mingine mnasemaje??????? Hamuwaungi mkono wenzenu????


  [​IMG]
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wasiishie hapo tu... akileta ubushi wamburuze mahamakani
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mbona kishaleta ubishi wampeleke tu
   
 4. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nyie wandugu, wanasheria sio watoa huduma kwa jamii, ni wafanya biashara ya profession ya sheria, na ni wachache sana wenye ethics za uanasheria....huyo huyo tendwa akiwa kwenye interest zao, wanaweza kuwageuka na kuwa rafiki yao sasahivi, na hata kama akiburuzwa mahakamani, atatetewa na wanasheria haohao. na watahakikisha anashinda kwasababu tu ya mshiko...
   
Loading...