Hongera TBC

Hongera TBC

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,497
Reaction score
38,347
Napenda kutoa pongezi kwa kituo chetu pendwa cha TBC1 kwa kujaribu na kujitahidi kwa viwango vya chini kabisa kama si sana kutoa habari za wapinzani zenye muelekeo chanya.

Jana nilikuwa napata kinywaji katika viunga vya mji mdogo wa Arumeru [USA RIVER] na bahati nzuri nikawa natazama taarifa ya habari ya saa 2 TBC waliitoa habari ya Mheshimiwa Mbowe kuhusiana na ombi lake la kusafisha magereza kwa Mheshimiwa Jaji Mkuu,IGP na Commissioner General wa Magereza.

Kwa kawaida Mimi si miongoni mwa watazamaji wa TBC,niliacha siku nyingi kuitazama TBC kwakuwa walikuwa wamejikita katika kusifia tu.Habari zao nyingi si balanced hata kidogo,viwango vyake vya habari huwezi kuvifananisha au kuvilinganisha na enzi za Tido akiwa Mkurugenzi Mkuu.TBC ili cover uchaguzi wa Kenya baina ya Raila na Mwaikibaki katika viwango ya BBC.

Leo TBC imekuwa kichekesho,kituko kwajinsi inavyowapatia habari waTanzania,unaweza kufikiri Dr Rioba kalogwa au pengine si yeye.Ni bahati mbaya jana nilikuwa bar nyumbani kwangu ni marufuku kuitazama TBC.
 
Mbona kama wewe ndio mkurugenzi mwenyewe wa TBC ?

Au ndo unaifanyia tangazo kiana
Mimi kuliko kuangaria TBC ni bora huo muda nikasikilize UONGO mpya kwenye vijiwe vya kahawa aise

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Mbona kama wewe ndio mkurugenzi mwenyewe wa TBC ?

Au ndo unaifanyia tangazo kiana
Mimi kuliko kuangaria TBC ni bora huo muda nikasikilize UONGO mpya kwenye vijiwe vya kahawa aise

Sent using my iPhone using jamiiforum app

Mkuu soma tena na tena labda utanielewa.
 
Kuliko niangalie taarifa ya habari TBC ni bora niangalie TBC ya wanyama,
Kuliko kuangalia ahadi za uongo za viongozi wetu kila siku ni bora niangalie simba akimla swala(nafarijika sana)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TBC ya wanyama ndo imekuja kuizamisha kabisa TBC taifa

Sent using Jamii Forums mobile app

Duh Mimi nilikuwa sijui kama kuna TBC ya wanyama kwaujumla mini siangalii zote niko DSTV.Jana nilikuwa bar ikatokea bahati nikatazama taarifa ya habari.Nadhani huu ni mwaka wa 5 sijawahi kuitazama.
 
Back
Top Bottom