Hongera somebody! (JK et al): Now we are talking.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera somebody! (JK et al): Now we are talking..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 19, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Gazeti: Uhuru  NA SULEIMAN JONGO

  WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, jana alizindua mradi wa kuendeleza sayansi katika vyuo vikuu, na taasisi za elimu ya juu wenye thamani ya sh. bilioni 130.

  Akizindua mradi huo mjini Dar es Salaam, Profesa Maghembe, alisema hiyo ni hatua moja ya kuendeleza sekta ya sayansi na kuongeza wataalamu.

  Mradi huo, unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, utakuwa na awamu tatu ambapo mbili, kila moja itakuwa na gharama hiyo.

  Profesa Maghembe, alisema mradi huo utawezesha ununuzi vifaa vipya katika vyuo vikuu vya umma, kuvipanua, kuongeza idadi ya wanafunzi na kuwaendeleza wahadhari wasaidizi kitaaluma.

  Alisema katika mazingira ya maendeleo ya teknolojia duniani,nchi haiwezi kuendelea kisayansi kama haitakuwa na vifaa vya kisasa vitakavyoweza kutumika kwa mafunzo ya vitendo.

  "Kuna baadhi ya vyuo nilipovitembelea nilikutana na vifaa ambavyo mimi mwenyewe nilifanyia utafiti wakati nafanya shahada yangu ya udaktari wa falsafa katika miaka ya 1970, sasa unaweza kuona ni jinsi gani tulivyokuwa na matatizo," alisema.

  Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia nchini, Chiyo Kanda, alisema ufadhili huo umekuja kwa kuthamini juhudi za Tanzania katika kuendeleza sekta ya elimu.

  Chiyo alisema kuanzia miaka ya 2000, Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika sekta ya elimu, huku idadi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari ikiongezeka sambamba na wale wanaojiunga na vyuo vikuu na taasisi za elimu za juu.

  Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Profesa John Kondoro, alisema mradi huo utawezesha kuinua kiwango cha teknolojia nchini.

  Profesa Kondoro alisema, kutokana na uhaba wa kifedha baadhi ya kozi zilikuwa zilishindikana kuanzishwa, sasa itakuwa ni rahisi kufanya hivi.

  My Take:

  Now lets make the safeguards and benchmarks za kutuonesha kuwa hizo bilioni nyingi haziishii kununua vifaa vya ajabu ajabu. Watuambie tutapima vipi maendeleo yetu ya Sayansi na Teknolojia tukiwa na msaada wa aina hii. Hii ndiyo misaada ninayoizungumzia mimi. Misaada ya kuwezeshwa kuwa huru siyo kudekezwa kuwa dependent.
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Heri ziende kununulia vifaa hata vikiwa vibovu nitakuwa na amani kuliko zikipelekwa kwenye mchwa anayeitwa 'capacity building' yaani washa, semina kongamano, masurufu, vikosi kazi... you name it.
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Shs 130 billion mpaka tungojee world bank waje kutufanyia mambo hayo?. Za EPA ziliibiwa ngapi vile?. Richmond wanalipwa shs ngapi kwa siku, kwa mwezi na kwa mwaka?. Kuna haja ya kusubiri wahisani ama kuna haja ya kujirekebisha katika management yetu?
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kidatu,

  Even that is our money sio za WB kwa sababu... tutakuwatumekopa hivyo tutalipa na tena na riba juu... au wewe mtu akikukopesha unaona amekupa zawadi mkuu?

  Na hii hali ya kutotofautisha kati ya mkopo na hisani ina nikere sana hapa Tanzania... eventually tuna-mis-use mikopo na hivyo tuna-cost vizazi na vizazi kwa kuwa vinatakiwa kuja kulipa.

  Kasheshe
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inaonekana sasa umeanza kurudi kwenye akili yako aliyokupa mwenyezi Mungu. Nakuombea ubaki hapo hapo kule ulikokuwa (kutetea mafisadi) kulikuwa hakukufai kabisa.
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Masikini ni yule asiye thamini chake.

  Hili joho limeshonwa London, ujiko. Wakati kule Peramiho kuna masista kibao wa kingoni wenye uwezo wa kushona joho zuri kuliko hilo.

  Oh enzi zile chuo kikuu nyama ilikuwa ikitoka Argentina na kuku Israel, huo ni ujinga pia. Wako wafugaji kibao Tanzania nyama si lazima itoke huko nje.

  Shati langu limetengenezwa Hongkong siyo kama yenu ya kushonwa na fundi hapo msufini. Ujuha huo huko Hongkong wanashona sokwe?

  Wengi tusiothamini vyetu twaona ni bora kunukiwa na mavi ya maghaibhu kuliko kunukiwa na harufu nzuri ya Chipsi dume na dagaa bichi wa kukaangwa kwa mafuta ya nazi pale Mwembe Yanga.
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Du!!!! Hii kali kumbe nimewahi kutetea mafisadi, hivyo kwa maana nyingine pia nimewahi kupenda ufisadi.. du mbona mambo murua!!!
   
 8. 255Texter

  255Texter Senior Member

  #8
  Mar 20, 2009
  Joined: Aug 31, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli hii ni habari nzuri na kama watanzania tungekuwa na umakini unaostahili tungetaka habari kama hii iwe front page kwenye kila gazeti, but that's another story.

  I really hope kwamba mradi huu hautaishia kuwa kama miradi yetu mingi ambapo 50% ya fedha zinatumika kugharimia management ya mradi, 20% inatumika for technical consultancy and then 30% ndiyo inapelekwa kufanya kilichodhamiriwa. It is appauling to see all this money beig wasted to contruct and lavishly furnish "project head office" and buying a fleet of overpriced "mashangingi" for project coordinators. I hope that won't be the case with this project's funds.
   
 9. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ahahaha umenifurahisha na Sign yako! kwahiyo nao wanaona opportunity na wanasema: I came, I saw, I conquered.

  Wingi wake unaandikaje?
   
 10. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  According to WB database, “The Science and Technology Higher Education Project for Tanzania” ilikuwa approved 27-MAY-2008. Na ina muda wa neema wa miaka 10.

  Sasa karibu ni mwaka baada ya kupitishwa ndo mradi unazinduliwa. Sipendi kumlaumu mtu ila nataka kujifunza, hivi unapoomba fedha si unapanga na jinsi ya kuzitumia na kuweka rasilimali zako tayari tayari. Kwa nini mwaka mzima umepotea bila any deliverable isipokuwa mbwembwe za uzinduzi wa mradi?
   
Loading...