Hongera sana mh. Rais, Sasa TRA wamepata viongozi waadilifu

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Napenda kmpongeza Mhe. JPM kwa kuwateua Ndugu Alphayo Kidata na Ndugu Eliakim Maswi kuwa viongozi wakuu wa TRA.

Mimi binafsi nawafahmu wote wawili ni watu waadilifu sana na kwa sasa nawahakikishia kuwa TRA ina uwezo wa kukusanya 2.6tr kwa mwezi.

Kwa staili ya JPM nchi itapiga sana sana hatua ya kimaendeleo kinyume na Serikali ya awamu ya nne.
 
Last edited by a moderator:
Napenda kmpongeza Mhe. JPM kwa kuwateua Ndugu Alphayo Kidata na Ndugu Eliakim Maswi kuwa viongozi wakuu wa TRA. Mimi binafsi nawafahmu wote wawili ni watu waadilifu sana na kwa sasa nawahakikishia kuwa TRA ina uwezo wa kukusanya 2.6tr kwa mwezi. Kwa staili ya JPM nchi itapiga sana sana hatua ya kimaendeleo kinyume na Serikali ya awamu ya nne.
JPM anajua sana na namkubali sana.
 
Rais wetu ni mtu makini na ana washauri wazalendo wanaopenda nchi yetu nina uhakika hatakuja kukosea katika kufanya maamuzi sahihi ya nchi yetu.
Ni mzalendo na mweledi
Tuzidi kumwombea Rais wetu
 
Hapana,Kidata ni kijana mwadilifu sana,kwa nafas alizoshika angekuwa mtu wa tamaa,angekuwa na mali nyingi mno.lakin jamaa si mtu wa kujisikia kabisa,ana maisha ya kawaida hata kijijin kwao hana cha kutisha kabisa.ila Maswi kias si muadilifu.ila poa tu kazi itapigwa.Uzuri hao wote wanatoka mkoa mmoja.
 
u

umakini wake ungeonekana hata katika hatua ya kuwateua watendaji waandamizi serikalini. kama wabunge wetu walitumia siku mbili wakilipwa kodi zetu, tumeshuhudia bunge likifanya kazi hadi usiku wa manane wakiwajadili wezi wa escrow, Tulishuhudia wabunge wetu wakiziweka pembeni tofauti zao za kihitikadi na kuuvaa uzalendo kuwawajibisha wezi. Leo haujapita hata mwaka, haohao waliowajibishwa wanarudishwa tena kwa kuwapromote. ni fedhea kwa chombo chetu kinachoaminika kama sauti ya umma yaani Bunge letu tukufu. Bado sijapata tafsiri ya hatua hii.
 
Napenda kmpongeza Mhe. JPM kwa kuwateua Ndugu Alphayo Kidata na Ndugu Eliakim Maswi kuwa viongozi wakuu wa TRA. Mimi binafsi nawafahmu wote wawili ni watu waadilifu sana na kwa sasa nawahakikishia kuwa TRA ina uwezo wa kukusanya 2.6tr kwa mwezi. Kwa staili ya JPM nchi itapiga sana sana hatua ya kimaendeleo kinyume na Serikali ya awamu ya nne.

Kama itakua hivyo, basi hakutakua na haja ya kutembeza bakuri kwaajili ya kujazia mapungufu katika budget yetu. Na hata wale waliokua wanapongeza safari za aliyemaliza muda wake kwamba zinaleta tija kwa pesa za misaada watapata aibu zaidi.
 
Ninacho kifahamu mimi kwa uhakika ni kuwa, E Maswi ni mtendaji kazi mzuri sana! Na kama alihusika na escrow pengine ilimbidi ahusishwe kwa lazima ili mamlaka za juu yake zijihakikishie usalama wao!

Najua hatuwezi kuwapata malaika wawe watendaji wetu,ila naunga mkono uteuzi wake hapo ailipowekwa!
 
Hapana,Kidata ni kijana mwadilifu sana,kwa nafas alizoshika angekuwa mtu wa tamaa,angekuwa na mali nyingi mno.lakin jamaa si mtu wa kujisikia kabisa,ana maisha ya kawaida hata kijijin kwao hana cha kutisha kabisa.ila Maswi kias si muadilifu.ila poa tu kazi itapigwa.Uzuri hao wote wanatoka mkoa mmoja.
tunawapaje nafasi watu ambao siyo waadilifu, tena waliokwisha wajibishwa kwa ubadhilifu, huku tuna watu kibao wenye weredi na kazi wasipewe fursa?
 
u

umakini wake ungeonekana hata katika hatua ya kuwateua watendaji waandamizi serikalini. kama wabunge wetu walitumia siku mbili wakilipwa kodi zetu, tumeshuhudia bunge likifanya kazi hadi usiku wa manane wakiwajadili wezi wa escrow, Tulishuhudia wabunge wetu wakiziweka pembeni tofauti zao za kihitikadi na kuuvaa uzalendo kuwawajibisha wezi. Leo haujapita hata mwaka, haohao waliowajibishwa wanarudishwa tena kwa kuwapromote. ni fedhea kwa chombo chetu kinachoaminika kama sauti ya umma yaani Bunge letu tukufu. Bado sijapata tafsiri ya hatua hii.
Kulikuwa na.nguvu ya fedha chafu nyuma ya kamati
 
Back
Top Bottom