Hongera sana Mh.JPMagufuli kwa kupasua majipu.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Kama mwananchi wa kawaida sina budi kumpa hongera Mh.Mafuli raisi namba moja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar aka TANZANIA.

kwa namna alivyoanza tu na kuwamsha wafanyakazi wazembe na kuwa weka kiti moto wanaopoteza muda na kula mishahara minono ya serikali huku Serikali haipati faida ,nikiongezea ni bora pia akaweka taratibu ambazo siku hizi zimekuwa ni chachi ya maendeleo huko majuu kwa kila mfanyakazi awe anaweka data kwa siku amefanya kazi gani katika sehemu anayo husika na kila mwisho wa mwezi iwepo statistic report yao.

Hongera sana Mheshimiwa raisi kwa kuendeleza kasi iliyopata jina la kupasua majipu tunategemea kazi hii itagusa wizara zote sehemu zote za Muungano kwa wizara husika bila ya kutazamana usoni.

Sasa haya majipu yanapopasuliwa na kupasuka halafu yakakamuliwa ni bora isiishie hapo ,hapo kwenye jeraha patibiwe na pahakikishwe pamepoa kinyume chake kunaweza kuota au kufanya donda ndugu.

Hongera za dhati endelea na kasi hiohio na mimi napenda kukuunga mkono kwa hilo japo nipo upinzani na sio upinzani kichama hapana nipo upinzani kiuwananchi lazima niwepo huku ili kuona Serikali iliyopo madarakani inanifanyia yale iliyotuahidi.

Mpaka iwe sina pa kuilaumu dnio nilisema Ccm ikishindwa nitajiunga nayo ili nwe upande wa upinzani.

Hongera Johni Pombe ,kwa kazi uloianza.
Wewe umepata kombe,shindano halijaanza.
Chomoza yako mapembe,uchome walojibanza.
Magufuli ndo wa kwanza,Tanzania aipambe.
Mwiba
 
Jiup gani?hivo vidogo vidogo master plan wa mafisadi tanzania nzima sahv ni mwenyekiti wa bunge
 
Back
Top Bottom