mr gentleman
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,223
- 4,679
Kwanza kabisa natoa pongezi za dhati kwa serikali yako rais Magufuli kwa juhudi kubwa ya kurudisha nidhamu serikalini na mitaani ama kwa hakika namba inasomeka haswa na wapiga dili kuanzia juu mpaka chini kabisa.
Pili natoa pongezi kwa kutuletea Tanzania ya viwanda mpaka sasa tunaona uchumi unaanza kuimarika, pesa inaongezeka thamani na watu wanaanza kujituma na kuanzisha viwanda vidogo vidogo. Jamani lazima tutambue viwanda sio lazima majengo makubwa makubwa kama ya Dangote ata sisi mitaani tunaweza kuanzisha viwanda.
Ukiwa na cherehani yako hicho ni kiwanda, ukiwa na sindano yako ya kushonea vitu kama mikeka hicho ni kiwanda, ukiwa na nyundo na msumeno hicho ni kiwanda, ukiwa na blender hicho ni kiwanda..... Watanzania lazima tuamke tuache kulalamika na kulialia tukisubiri wazungu ndo watuletee viwanda au serikali itujazie mapesa mfukoni tuchangamkie hii fursa ya uwekezaji wa viwanda vidogo. Tuache kupenda kushabikia siasa, wewe unashabikia sijui Lema kama Mandela mwenzio siasa ndio kiwanda chake.
Tumuunge mkono rais, maana rais Magufuli sio mtu wa mchezo mchezo kabla hujakata funua yeye kashakufunika.