Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,626
- 51,587
Yaani unahofia taifa kuwapa dhamana makampuni binafsi kufanya usajili wa fingure print kwaajili ya usalama, tena mratibu mkuu wa hili zoezi ni taasisi mbili za serikali yaani NIDA na TCRA?
Unasahau ni kampuni binafsi hizo hizo zinazotoa huduma ya mawasiliano, je huoni hofu ya kiusalama kwamba labda wakiamua vujisha taarifa nyeti za watumiaji wa huduma za mawasiliano???
Labda kabla ya huu uchambuzi wako wa hofu hofu, ni vyema ungejua ni jinsi gani huu mfumo wa usajili kwa njia ya fingure print unavyofanya kazi ili uweze kufanya hiyo risk assessment vizuri tujue udhaifu na ubora wa kimfumo.
Vingenevyo hiyo ni 'fear of unknown'.
Hizo Fingerprints zinakuwa stored kwenye servers za NIDA/TCRA au Makampuni ya simu?
Kwa sasa hivi ambapo hakuna system integration, sijaona ni kwa namna gani Makampuni ya simu yatunze taarifa zote za wateja wao kwenye servers zao isipokuwa tu eti Fingerprints zikatunzwe kwingine(NIDA na TCRA) , Kutokana na hilo ni dhahiri kuwa risk ya proliferation ya hizi fingerprints ipo na hilo ni jambo ambalo halitakiwi kuchukuliwa kimchezomchezo.