Hongera Rais Kwa kuhutubia Kwa kiswahili

IamMrLiverpool

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
4,274
6,102
Ni katika mkutano na waandishi wa habari leo akiwa na Raisi wa Vietnam baada ya kupiga broken hatari kule Arusha
Nadhani washauri wamemshauri vyema kwamba kwa kuwa lugha haipandi bora atumie kiswahili tu wamtafsirie Tulisema humu nadhani katusikia
Aendelee kutumia kiswahili aachane na kingereza Labda wakiwa faraghani huko sio kwenye press.
 
Lugha ni ufahari wa nchi, ishara ya nguvu, heshima Wa mila na desturi...ukitaka kumtawala mtu utamaduni ni "soft power'' vs "hard power"
wafaransa na waingereza kila mmojawapo ukikuta anajua lugha ya mwingine kwenye international forums hutasikia akiizungumza...ataongea lugha yake I.e heritage. Ni ujinga kuwa na hoja kuwa na wazo kwamba kingereza ndio lugha ya kidiplomasia..hapana wafaransa ndio waasisi Wa Diplomasia. Ila etiquette nzuri ni kuilinda heshima yako na utamaduni wako.
Thanks Uncle magu.
 
Ni katika mkutano na waandishi wa habari leo akiwa na Raisi wa Vietnam baada ya kupiga broken hatari kule Arusha
Nadhani washauri wamemshauri vyema kwamba kwa kuwa lugha haipandi bora atumie kiswahili tu wamtafsirie Tulisema humu nadhani katusikia
Aendelee kutumia kiswahili aachane na kingereza Labda wakiwa faraghani huko sio kwenye press.

Binafsi kanikosha sana. Mtu aje kwako. Halafu uanze kujibanabana kwa lugha za watu, watu wenyewe wenye lugha hawahusiki na kusanyiko lenu. Kiswahili kiwe lugha rasmi kwa viongozi wa ngazi za juu hasahasa wawapo nchini, na hata nje ya nchi.
 
Haijalishi kutumia lugha yoyote ilimradi unaozungumza nao watakuelewa na wewe ni mahiri katika hiyo lugha. Lugha si kama nyumba, gari ama shamba bali ni kama mwanga, mvua au hewa ambovyo hutumiwa na wote. hakuna haja ya kuogopa kutumia au kutotimia lugha fulani kwa kigezo cha ufahari au unyonge!
 
hahahah mmetafuta sana la kuongea kwa hiyo mmeamua kuja na hii ana broken english! so hii ndio itakuwa sera yenu uchaguzi ujao! Magufuli ana broken English
kila siku wanatafuta chaka la kujifichia,linakosekana!ahahaha
 
Amefanya vizuri kukitumia kiswahili ingawa lugha yenyewe bado changa, kuna baadhi ya maneno yanahitaji ujuzi kuyatumia hasa hasa likija swala la mahusiano ya kimataifa. maneno kama. " nilikuwa nachomekea chomekea" ajiepushe nayo kwa sababu kutawachanganya wale wanaotafsiri hotoba yake kwa kutumia kamusi ya kiswahili

Awe makini na matumizi ya maneno ya kiswahili. hatujali lafudhi yake alimradi ni kiswahili fasaha
 
Back
Top Bottom