Hongera Rais Dr. Magufuli, huduma za afya zinaridhisha hakuna malalamiko kama awali

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,361
Ni muda mrefu sasa sijasikia malalamiko toka kwa wanainchi kuhusu Huduma za afya baada ya Utawala wa Awamu ya tano kuingia kazini na kufanya baadhi ya mageuzi ktk sekta ya umma.

Baada ya hospitali nyingi kuboresha Huduma zake ktk vitengo tofauti mfano maabara,madawa,uzazi na watoto,upasuaji,mionzi,mortuary,kinywa na meno,na pia Huduma kwa wagonjwa wa nje..OPD na waliolazwa..IPD naona kumekuwa na utulivu mkubwa sana toka kila ya nchi.

Viongozi na watumishi wamekuwa na kazi moja tu kuwatumikia wanainchi na wagonjwa wanatoa ushirikiano kwa watoa Huduma ili kujenga mahusiano mazuri ambayo hapo nyuma yaliyoyumba kidogo.

Changamoto kama zipo ni za kawaida tu kama sekta zingine lakini kwa afya kuna utulivu sasa nao uona.

Hongera Rais Magufuli na viongozi wengine kwa kuwapa nafasi na heshima wana taaluma hawa kufanya kazi zao kama viapo vyao vinavyosema.
 
Kwa sekta ya AFYA kwa kweli zilizobaki ni changamoto za sehemu mojamoja ambazo ukiangalia vyema zatokana na watendaji eneo husika na si serikali PAA SEE
Ni kweli kabisa.
 
Kwa sekta ya AFYA kwa kweli zilizobaki ni changamoto za sehemu mojamoja ambazo ukiangalia vyema zatokana na watendaji eneo husika na si serikali PAA SEE
ha ha ha hujui kinachoendelea huku mkuu laiti ungejua,

Ni kweli wakati mwingine watumishi wanakuwa na matatizo lakini ni kwa uchache sana,

Changamoto ya afya nchi hii bado sana bado sana aisee,

kama mnaongea kuwafurahisha wakuu wenu sawa lakini bora tukasema ukweli tu,

ocean road dawa hakuna, kuna hospitali vifaa vimeharibika muda sasa watu hawapati huduma,

Juzi kati nilikuwa maabara moja ya hospital kubwa tu hapa nchini oooh aisee kuna mashine imeharibika more than six months

endeleeni kumpigia vinanda mfalme mpate mkate wenu
 
Unaota au maana hakuna uduma mbovu kama kipindi hiki wananchi hawalalamiki kwa kuogopa mko wa chuma usiwaangukie hospital za selikali zinatoza pesa kama za binafsi kuna jamaa wamesusa maiti muhimbili wanadaiwa milioni kumi siku 28 alizo lazwa bahati nzuri ni mjumbe wa nyumba kumi ccm
 
Hii nchi tuna matatizo sana! Tangu zamani nchi ina uhaba mkubwa watumishi sekta ya afya including madaktari na manesi!

Tangu awamu ya tano imeingia; imefunga ajira... haijaajiri madaktari, manesi wala wang'oa meno lakini bado mnaamini mambo kwenye sekta ya afya ni mujarabu?!

Very sad!!!
 
Mkuu kama watu wako kimya na kazi zinaendelea malalamiko hatuyasikii sasa unataka tusemeje kama si kuwa hali ni shwari.

Bila Uzi huu ungeyasema hata hayo na hata kuitaja hiyo hospitali kwa jina umeshindwa kuhusu hicho kifaa unafikiri wa husika watapate taarifa kama hawajui kinachoendelea.

Tuwe wazi na Huduma za jamii kwa wanainchi jamani.
 
Hii nchi tuna matatizo sana! Tangu zamani nchi ina uhaba mkubwa watumishi sekta ya afya including madaktari na manesi!

Tangu awamu ya tano imeingia; imefunga ajira... haijaajiri madaktari, manesi wala wang'oa meno lakini bado mnaamini mambo kwenye sekta ya afya ni mujarabu?!

Very sad!!!
Hilo liko wazi mkuu kuhusu upungufu wa watumishi wa afya ktk kitengo vyote sio geni kabisa na hatujasema Huduma ziko super.

Ila watumishi waliopo kazini mpaka sasa wanafanya kazi kwa weledi wa hali ya juu sana na wanastahili sifa zao hata kwa upungufu walikuwa nao lakini Huduma ziko vizuri.

Ukiangalia Indicators kuna improvement kubwa sana.
 
Unaota au maana hakuna uduma mbovu kama kipindi hiki wananchi hawalalamiki kwa kuogopa mko wa chuma usiwaangukie hospital za selikali zinatoza pesa kama za binafsi kuna jamaa wamesusa maiti muhimbili wanadaiwa milioni kumi siku 28 alizo lazwa bahati nzuri ni mjumbe wa nyumba kumi ccm
Hakuna utawala wa mkono wa chuma Tanzania.

Kumbuka pia gharama ya maisha duniani iko juu tofautisha enzi za Mel Nyerere tulitibiwa bila malipo na sasa tunapochangia gharama za afya.

Ushauri pia kwa watumishi na vikundi mbalimbali ni vizuri kuwa na Bima ya Afya

Huduma ya watoto chini ya miaka 5 mama wajawazito na wazee ni bure.

Wasiokuwa na uwezo kupitia Maofisa wa Ustawi wa Jamii wanapunguziwa gharama sana na wengine kupata Huduma bure
 
Hilo liko wazi mkuu kuhusu upungufu wa watumishi wa afya ktk kitengo vyote sio geni kabisa na hatujasema Huduma ziko super.

Ila watumishi waliopo kazini mpaka sasa wanafanya kazi kwa weledi wa hali ya juu sana na wanastahili sifa zao hata kwa upungufu walikuwa nao lakini Huduma ziko vizuri.

Ukiangalia Indicators kuna improvement kubwa sana.
Mkuu tatizo kubwa ni kwamba mmejitwika mzigo wa kusifa kila kukicha,

Naamin kabisa inawezekana ukawa na muda mrefu hujaenda kutibiwa hospitali za serikali hata ukikataa nafsi itakusuta,

watumishi wa afya hawana ule mzuka au morali ya kazi tena kwa sababu ya matendo ya kisiasa yanayoendelea,

Katika mahospitali ya serikali hasa mikoani kule kwa bibi yangu KOROMIJE huduma mbovu sana nikisema mbovu sana namaanisha nnachokisema.

Ukirudi hapa mjini kila kona kuna kituo cha Afya uliza huduma inayotolewa sasa utakaa chini ulie kama unaujua ukweli,

Taasisi zilizopewa jukumu la kufuatilia ubora wa huduma wamekalia kufukuzana na mashoga,

Nchi yetu haina mfumo rasmi wa kipi kitumike na kipi kisitumike katiaka mahospitali kuanzia vifaa,madawa na reagents kulingana na ubora matokeo yake kila mtu ana-import vitu anavyovijua yeye na kuviingiza sokoni.

kuna midawa kibao nchi za wenzetu imepigwa marufuku kwa kuwa na madhara makubwa kuliko matibabu ila sisi wapi ndo tunazid kuwalisha

mkuu usiongelee habari ya afya nchii bado sana sana

JS
 
Hebu weka hapa hizo indicators!!!

Kutosikia malalamiko katu hakuwezi kuwa indicator.

Msingi wa kwanza wa huduma za afya ni watoa huduma za afya! Hata kama hospitali itakuwa full equiped with all medical facilities; bado itakuwa ni kazi bure kama watoa huduma za afya hakuna au wapo kwa uchache!

Jambo lisilo na shaka ni kwamba tuna uhaba mkubwa wa watoa huduma za afya... na huko vijijini hali ni mbaya zaidi!! Na kwavile tunakaribia miaka miwili sasa hatujaajiri; ina maana gap kati ya watoa huduma za afya na wananchi linazidi kuongezeka!

Kwahiyo, hata kama watumishi waliopo wanafanya kazi kwa weledi lakini bado watakuwa short of resources including human resources. Na kwa maelezo yako, unaonekana unazisemea hospitali zile ambazo tayari zinao hao wahudumu na kwamba hivi sasa wanafanya kazi huku ukisahau kuna zingine hazina kabisa hata hao wahudumu... lakini bado hata huko; nadhani huna taarifa za malalamiko ya wananchi!!! Hiyo nayo inaonesha malalamiko ya wananchi hayawezi kuwa kigezo!
 
Mkuu tatizo kubwa ni kwamba mmejitwika mzigo wa kusifa kila kukicha,

Naamin kabisa inawezekana ukawa na muda mrefu hujaenda kutibiwa hospitali za serikali hata ukikataa nafsi itakusuta,

watumishi wa afya hawana ule mzuka au morali ya kazi tena kwa sababu ya matendo ya kisiasa yanayoendelea,

Katika mahospitali ya serikali hasa mikoani kule kwa bibi yangu KOROMIJE huduma mbovu sana nikisema mbovu sana namaanisha nnachokisema.

Ukirudi hapa mjini kila kona kuna kituo cha Afya uliza huduma inayotolewa sasa utakaa chini ulie kama unaujua ukweli,

Taasisi zilizopewa jukumu la kufuatilia ubora wa huduma wamekalia kufukuzana na mashoga,

Nchi yetu haina mfumo rasmi wa kipi kitumike na kipi kisitumike katiaka mahospitali kuanzia vifaa,madawa na reagents kulingana na ubora matokeo yake kila mtu ana-import vitu anavyovijua yeye na kuviingiza sokoni.

kuna midawa kibao nchi za wenzetu imepigwa marufuku kwa kuwa na madhara makubwa kuliko matibabu ila sisi wapi ndo tunazid kuwalisha

mkuu usiongelee habari ya afya nchii bado sana sana

JS
Pamoja na yote uliyoongea kuhusu Huduma za afya nadiriki kusema kuna nafuu sana ukilinganisha na tulikotoka.

Siko hapa kumsifia MTU ila nasema kwa dhati kabisa Dr Kikwete amefanya kazi kubwa sana kuhakikisha Tanzania tunapata baadhi ya Huduma ambazo zilikuwa ndoto kuzipata ktk nchi masikini MF; operation za moyo,mishipa ya fahamu n.k

Na kwa Dr Magufuli tunaona kuna kuanza kupandikiza figo ifikapo May mwaka huu.

Upungufu wa wafanyakazi na mifumo ya kuhakiki ubora wa huduma issue ya madawa hizo ni changamoto za kufanyiwa kazi siku hadi siku.
 
Back
Top Bottom