Hongera Mwakyembe: Nchi tano kuunganishwa na meli mpya Kyela

Lupyeee

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
2,683
2,818
Kwa miaka mingi tuliteseka sana kila tunapotaka kusafiri ziwa nyasa.

Lakini kutokana na kuisha kwa ujenzi wa meli 3 chini ya usimamizi mahiri wa mbunge wetu Dr Mwakyembe tatizo hili limeisha sasa.

Hongereni sana wana kyela.

=======
New+Document.jpg

Kaimu Mkuu wa Bandari ya Itungi - Kyela katika Ziwa Nyasa mkoani Mbeya, Ajuaye Msese amesema biashara kati ya Tanzania, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Afrika Kusini na Malawi imepata huduma mpya baada ya meli mbili mpya kuanza majaribio.

Msese amesema iwapo majaribio hayo yatakamilika na meli hizo kuwa salama kwa ajili ya utoaji wa huduma, wananchi wa pande hizo wataweza kuendesha shughuli zao kwa ufasaha.

Meli mbili za mizigo zilizotengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine zimeshushwa katika ziwa hilo kwa ajili ya majaribio baada ya kukamilika kwa asilimia 95.

Meli hizo ni kati ya tatu, ikiwamo ya abiria zinazojengwa kwa gharama ya Sh20 bilioni.

Msese amesema: “Kila (meli) moja itakuwa na uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo tofauti na zilizopo zinabeba tani 720, hivyo kukamilika kwa meli hizi tutakuwa tumeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji wa majini badala ya kuendelea kusafirisha mizigo kwa barabara”.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Saleh Songoro amesema kitakachofuata ni matengenezo madogo na ukaguzi wa ubora kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

Chanzo: Mwananchi
 
Kyela wananchi wanakunywa maji ya vyura miaka hii ya 2017.
...nenda Ngonga,Bujonde,Kilwa,Katumbasonge etc...kuna mtandao wa maji uliotandazwa na Danida enzi za Kasyupa...ila alivyo kuja huyo jamaa wananchi wanakinywa maji ya vyura.

.....huo jamaa hakuna alichofanya chochote cha maana Kyela...ni mpiga kelele tu zaidi ya miaka kumi bila matokeo chanya yoyote.
 
!
!
nimebaki namshangaa tu huyu mleta mada....atakuwa ni somebody Mwakyembe tu wa huko ikolo
 
Kaimu Mkuu wa Bandari ya Itungi - Kyela katika Ziwa Nyasa mkoani Mbeya, Ajuaye Msese amesema biashara kati ya Tanzania, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Afrika Kusini na Malawi imepata huduma mpya baada ya meli mbili mpya kuanza majaribio.

Chanzo: Mwananchi
169550-004-B2292C66.jpg

Wakuu I am at loss, huyu Ag Port Manager wa Itungi owes us a detailed explanation.
I see 3 countries!!
 
Hizo nchi tano zinatoka wapi?
Hata elimu ya Geografia sifuri kabisa.

Ni nchi tatu tu ambazo ni Tanzania, Malawi na Msumbiji.
 
Kwa miaka mingi tuliteseka sana kila tunapotaka kusafiri ziwa nyasa.

Lakini kutokana na kuisha kwa ujenzi wa meli 3 chini ya usimamizi mahiri wa mbunge wetu Dr Mwakyembe tatizo hili limeisha sasa.

Hongereni sana wana kyela.

=======
Kaimu Mkuu wa Bandari ya Itungi - Kyela katika Ziwa Nyasa mkoani Mbeya, Ajuaye Msese amesema biashara kati ya Tanzania, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Afrika Kusini na Malawi imepata huduma mpya baada ya meli mbili mpya kuanza majaribio.

Msese amesema iwapo majaribio hayo yatakamilika na meli hizo kuwa salama kwa ajili ya utoaji wa huduma, wananchi wa pande hizo wataweza kuendesha shughuli zao kwa ufasaha.

Meli mbili za mizigo zilizotengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine zimeshushwa katika ziwa hilo kwa ajili ya majaribio baada ya kukamilika kwa asilimia 95.

Meli hizo ni kati ya tatu, ikiwamo ya abiria zinazojengwa kwa gharama ya Sh20 bilioni.

Msese amesema: “Kila (meli) moja itakuwa na uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo tofauti na zilizopo zinabeba tani 720, hivyo kukamilika kwa meli hizi tutakuwa tumeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji wa majini badala ya kuendelea kusafirisha mizigo kwa barabara”.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Saleh Songoro amesema kitakachofuata ni matengenezo madogo na ukaguzi wa ubora kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

Chanzo: Mwananchi
Unampa Mwakyembe pongezi za uongo kwa faida ya nani ? Ni sh ngapi ambazo Mwakyembe binafsi ametoa au amechangisha kwa ajili ya Mradi huu ?

Hakuna nafuu yoyote ya kisiasa ya kutengeneza ambayo Mwakyembe atapata , MTU ALIYESHINDWA KUTATUA KERO NDOGO YA MAJI KYELA ataweza kuleta meli ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom