Hongera MSIGWA, JK, MBOWE, PINDA na wanasiasa wengine kwa mfano huu halisi

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Ile kasumba kwamba siasa ni maneno inabidi ipitwe na wakati. Inatia moyo sana kuona mwanasiasa au kiongozi akiwa mbele kama mfano wa kile anachohubiri. Hawa na wengine wengi wanafaa kupongezwa.

Kama unataka Mali nenda kaipate shambani. Mungu awabariki sana.








Msigwa.jpg

Mchungaji Msigwa akikagua shamba lake la Mahindi.
unnamed%2B(16).jpg

Waziri mkuu mstaafu, alipotembelewa na Maaskofu shambani kwake.
SLAMA1.JPG

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika shamba lake la Mahindi.
1.jpg

Kiongozi wa Chadema Mbowe akikagua Greenhouse yenye zao la nyaya katika shamba analomiliki.
 
Mh Mbowe si walisema anaharibu mazingira?
tunampongeza kwa kushiriki katika kilimo ambacho vijana wengi wanaona bora kulala kwenye mabox kariakoo wakati mito inatiririka na kuishia baharini. Katika kufanya haya kakumbushwa kuna taratibu za matumizi ya maji maana sio sisi tu hata vizazi vijavyo vinatakiwa kuyatumia, tulinde vyanzo na kuvitumia kwa utaratibu. Nadhani watamalizana.
 
tunampongeza kwa kushiriki katika kilimo ambacho vijana wengi wanaona bora kulala kwenye mabox kariakoo wakati mito inatiririka na kuishia baharini. Katika kufanya haya kakumbushwa kuna taratibu za matumizi ya maji maana sio sisi tu hata vizazi vijavyo vinatakiwa kuyatumia, tulinde vyanzo na kuvitumia kwa utaratibu. Nadhani watamalizana.
Hiki kilimo kisikie kwenye tv mkuu, mimi nalima sana toka nikiwa sekondari na elimu nilipata kutokana na shamba, tatizo kubwa ni soko na hatuna vifaa vya kusindika, kaka unaweza kufa na pressure. Serikali yetu iweke mazingira rafiki kwa wakulima. Hawa wanakina Pinda wanaconnection za nje analima anajua bei ya kuuzia hawalimi kama sisi, Hakuna mkulima aliyewahi kutajirika hata mmoja kwa Tanzania isipokuwa ukiwa middleman hapo sawa, kilimo inakuwa kama kisingizio lakini unafanyabiashara huko huko shambani. Asante
 
Hakuna biashara ya uhakika na endelevu kuliko ya uzakishaji mazao ya chakula.

Vita ya kisiasa iliyopo ya kama kuna baa la njaa au la, ni ushahidi tosha. Pia hatujasahau sakata la ukosefu wa sukari.

Hivyo vijana muachane na umachinga, shughuli za sanaa, biashara ya unga, mjikite kwenye kilimo au ufugaji wa kisasa, kwani kila kijiji nchini kina wataalamu, ambao kwa kutokutumika wanakunywa tu pombe.
 
Nilipoona Msigwa nikajua unampa hongeara au pole kwa kaka sijui mdogo wake au mjomba aliyevaa nguo za jeshi la Magereza na kuingia mtaani.
 
Back
Top Bottom